Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?
La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...
lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...
Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20
leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?
mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?
tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?
Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....
Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?
hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?
Sasa tuje na maamuzi ya kufunga biashara za wote wanao tuhumiwa kukwepa kodi..
je tukifunga hizo biashara na wanaotegemea hizo biashara kufilisiwa
ndo tumejenga?
Kwanini wasiwekewe utaratibu wa kuanza kulipa hata kidogo kidogo taratibu?
walioajiriwa kwenye biashara hizo je? hatuwajali?....
kama mtu hajalipa kodi miaka 10 je hatuoni ni uzembe pia wa serikali?
kufilisi na kufunga tu kila biashara wakati ukwepaji kodi ulikuwa kama ni utamaduni wa nchi nzima
kunasaidia nini?....si bora walazimishwe kulipa hata nusu ya kodi wanayodaiwa?
na biashara zao zibaki kuajiri na kuchangia uchumi?
Vipi kuhusu biashara kufirisiwa ?Kwa hiyo unataka vyeti vya kughushi vihalalishwe?
Kuna tatizo kubwa tatizo tunafikiri unapomfungia mtu office ndio njia ya kutatua tatizo wakati huyo mtu alikuwa amewaajiri wananchi waliompigia kura Rais akawa hapo alipo ,alafu leo hii Ajira ya yule mtu inakufa yeye moja kwa moja anaanza kuilaumu Serikali.
Tungetengeneza kwanza sheria ya kuwadhibiti kuanzia sasa kodi ilipwe ndani ya mwaka mmoja.
Kwa sababu tulifanya uzembe uko nyuma hata kuna wakandarasi nasika hawajawai kulipa kodi kuanzia miaka 5 iliyopita.
Kuhusu Elimu ni swala gumu kidogo lkn hili la kufunga Biashara siyo gumu kwani kwa kawaida ukiona mtu kafungiwa Biashara yake ujue hiyo ni hatua ya mwisho kabisa kuchukuliwa na Serikali, kuna watu wanadaiwa kwa zaidi ya miaka 10 na siku zote wamkuwa wakionywa na kuandikiwa barua lkn bado hawajali sasa ulitegemea nini kifanyike tena zaidi ya hapo?
Sidhani kama kuna duka la mtu au biashara iliyofungiwa kwa sababu ya tu ameshindwa kulipa kodi ya mwezi/mwaka 1 tu na kwamba hilo lilikuwa ni onyo la kwanza, sidhani kama kuna kitu kama hicho, mara nyingi ni ukaidi wa muda mrefu!
Ujanja ujanja huu walioutumia kupata hivyo vyeti ndio unaolifilisi hili taifa!Tena ni hatari kwa Prof. kuwa na vyeti feki maana kuna uwezekano mkubwa kwamba hata tafiti zake nyingi alifeki ili afike hapo! Tuite spedi spedi, tuache kutetea upuuzi!Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....
Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....
Crime haina expire date, sometimes muhusika anaweza kuwa ame move on but ikigundulika lazima awajibike, huenda aliziba nafasi ya mtu mwingine ambaye kwa kukosa stahili yake haku recover hadi leo.
Mkuu hili zoezi la vyeti 'contradictions' zitajitokeza. Inawezekana huyu mwenye cheti fake aliendelea na vyeti fake mpaka elimu ya juu zaidi au ilikuwa ni juhudi yake kufikia elimu ya juu. Mimi nadhani idara husika ilipashwa kuaangalia hili jambo. Utendaji wa kazi uzingatiwe kuliko kuangalia vyeti peke yake. Ni wazo langu. Ila kuna watu wana Masters PHD unajiuliza aliipata vipi kwani akifungua mdomo kuzungumza utaweka mikono kichwani ukijiuliza aliwezaje kusoma kufikia kiwango hiki!!!???Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....
Ndiyo maana nimesema hili la Elimu ni swala gumu, kwa maana hapa unaongelea udanganyifu, hivyo basi kama umedanganya umefanya kosa ina maana unapaswa kuadhibiwa na haijalishi wewe ni nani au una wadhifa gani!
Nitakupa mifano, kuna Waziri wa Ulinzi wa nchi moja barani Ulaya aliondolewa kwenye wadhifa wake kwa sababu walikuja kugundua kwamba kwenye PhD thesis yake alinakiri kazi ya watu wengine, hali iliyopelekea Chuo Kikuu alichosomea kumvua Shahada yake ya PhD ingawaje ni miaka mingi ilipita na yeye alikuwa tayari amefikia ngazi ya Uwaziri na baada ya hapo Serikali ya nchi yake nayo ikamvua Uwaziri kwa sababu ya udanganyifu alioufanya zaidi ya miaka 10 iliyopita!
Ni kama vile kwa mfano Raisi wa USA Obama (sijui kama mfano unaendana), kuna wanaosema kwamba hajazaliwa USA na kwamba aligushi cheti cha kuzaliwa, sasa Je kama ingekuwa tuseme wanaosema hivyo wako sahihi unafikiri nini kingetokea? Unafikiri Obama angeachwa aendelee na Uraisi wake kwa sababu ni miaka mingi iliyopita au wangemu impeach?
Mkuu hili zoezi la vyeti 'contradictions' zitajitokeza. Inawezekana huyu mwenye cheti fake aliendelea na vyeti fake mpaka elimu ya juu zaidi au ilikuwa ni juhudi yake kufikia elimu ya juu. Mimi nadhani idara husika ilipashwa kuaangalia hili jambo. Utendaji wa kazi uzingatiwe kuliko kuangalia vyeti peke yake. Ni wazo langu. Ila kuna watu wana Masters PHD unajiuliza aliipata vipi kwani akifungua mdomo kuzungumza utaweka mikono kichwani ukijiuliza aliwezaje kusoma kufikia kiwango hiki!!!???
Sheria za kodi zipo lakini zilikuwa hazitekelezwi kikamailifu. Kwa sababu hizo watu walikuwa wanakwepa kulipa kodi au kutolipa kabisa. Serikali ya awamu ya tano haijatunga sheria mpya bali imeamua kufuatilia utekelezaji wa sheria zilizopo. Katika hatua hiyo imegundua wafanyakazi biashara ambao wanatozwa kodi hata miaka 10. Kisheria wana makosa na hatua zinazochukuliwa ni sahihi. Suluhu ni kulipa kodi bila kuingiza siasaKuna tatizo kubwa tatizo tunafikiri unapomfungia mtu office ndio njia ya kutatua tatizo wakati huyo mtu alikuwa amewaajiri wananchi waliompigia kura Rais akawa hapo alipo ,alafu leo hii Ajira ya yule mtu inakufa yeye moja kwa moja anaanza kuilaumu Serikali.
Tungetengeneza kwanza sheria ya kuwadhibiti kuanzia sasa kodi ilipwe ndani ya mwaka mmoja.
Kwa sababu tulifanya uzembe uko nyuma hata kuna wakandarasi nasika hawajawai kulipa kodi kuanzia miaka 5 iliyopita.
Mifanoo ya mtu mmoja mmoja sidhani kama ina apply
nikupe tu mfano halisi
wafanyakazi wa bandari 1500 ambao wengi wanafanya kazi tu za mikono wamekamatwa na vyeti bandia vya form four
je wote wafukuzwe? mtu pengine ni kuli tu
anashiriki kubeba mizigo.....cheti halisi cha form four kinasaidia nini?
Madaktari tuseme wa Muhimbili labda robo yake wagundulike vyeti vya form four ni bandia
wafukuzwe wote?