Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewakosea...
Hivi hawa Manabii wa sasa watu hawajitambui kuwa TULISHAAMBIWA kuwa kutatokea manabii wa uongo?
Kuhusu kufufua km wangekuwa wanafufua kweli si wengi wangekuwa hai?
Pili wagonjwa si wengi wangekuwa hawaumwi, kwanza now ndio idadi ya wagonjwa imezidi kuwa kubwa kuliko awali.
Enzi za Bibi zetu watu walikuwa wema mbona manabii hawakuwepo sasa zama za uovu ndio kibaoo..
Pili kama wewe nabii kweli, hela unayoipata usingezitumia kujenga mijumba ya kifahari, kuendesha magari ya kifahari, ungetumia hela hizo kupeleka vituo vya watoto yatima, kuwasaidia wasiojiweza, kuwasaidia wagonjwa wapo masikini wengi saana Tanzania na nchi nyingine za Africa.
Hawa manabii wa sasa kila kukicha wanaibuka sababu washajua ukiwa nabii unapata hela...Woote wanatafuta ulaji..
Nabii gani anatembea na mke wa mtu....Nabii ni kiumbe safi kisichokuwa na dhambi...
Yaani hizi zama zimeharibika ila baadhi ya watu hawalitambui hili....Omba jiombee mwenyewe...Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe...Sio wewe uombewe...Piga goti mwenyewe