Umefanya kosa kubwa sana la kiufundi kulinganisha scenario ya serikali/CCM kupuuzwa na wananchi kwenye ishu ya chanjo ya UVIKO 19 na hiyo uliyoita "Tundu Lissu kukataliwa na wananchi"...
Ni kwa sababu ishu ya maandamano ya CHADEMA kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020 ya udiwani, ubunge na Urais ilikuwa ni vita ya jeshi lenye silaha zote (serikali) dhidi ya wananchi/umma (usio na silaha yoyote)...
Kama kiongozi makini aina ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu, ukiona hivi ni bora ku - retreat na kuwashawishi wananchi wanaokuunga mkono ku retreat pia ili kuepusha maafa na vifo na kisha kujipanga upya kwa namna nyingine...
This is what was done by CHADEMA/Tundu Lissu/Freeman Mbowe last year. Itakuwa ni mwendawazimu pekee anaweza kumfanyia hivi mpinzani wake ktk hoja, halafu kisha atoke aanze kutamba kuwa;
" ....mnaona eeeh, wameniogopa au amekosa watu au watu wamempuuza...!"
Utakuwa unafanya propaganda za kijinga na kipumbavu kabisa....
Sasa na wewe hebu tuambie, mtifuano wa Ant COVID 19 Vaccine Movement inayoongozwa na Rev. Bishop Gwajima vs Pro COVID 19 Vaccine Movement inayoongozwa na Rais Samia, Bunge la Ndugai, Dr Dorothy Gwajima wapi polisi au JWTZ imeingilia...?
Jibu ni HAKUNA. Bali ni hoja tu zinatawala kwa pande mbele kama ambavyo wewe mwenyewe umekiri ktk andiko lako. Rev. Gwajima kaishinda kwa hoja serikali yote na umma karibu wote uko nyuma yake...
Huu ni uthibitisho mdogo tu kuwa, hata mwaka jana kwenye uchaguzi mkuu, kama hoja ndizo zingeamua nani awe duwani au mbunge au Rais wa nchi hii, CCM mngeangukia pua zetu vibaya sana...!!