Hawampendi Askofu Gwajima lakini wanakubali hoja zake

kambiko

Senior Member
Jan 12, 2018
155
250
Tanzania ni moja ya nchi ambayo ukidhani wananchi wake wengi wanachokisema ndicho watakitenda basi utakuwa unajidanganya na nafasi yako!

Historia nchini imeonyesha mara zote wanaodhani wana watu nyuma yao hujikuta peke yao!

Sio muda mrefu aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu alijikuta “peke yake” baada ya kuitisha maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020. Hii ilikuja baada ya kuamini huku akisaidiwa na Sheikh Ponda na “Askofu” Mwamakula kuwa kuna kundi kubwa la watu nyuma yake ambalo aliliapisha wakati wa kampeni ili lihakikishe kura haziibwi na kama zitaibwa litaandamana nchi nzima pale atakapoitisha maandamano.

Uchaguzi Mkuu ulifanyika na baada ya matokeo kuanza kutangazwa, Tundu Lissu aliyakataa na kuitisha maandamano nchi nzima akiamini lile kundi lililokula kiapo kutoka kwa Sheikh Ponda na “Askofu” Mwamakula litajitokeza. Alichokishuhudia hakuamini! Mengine ni historia!

Kwa kiwango kikubwa ni kundi hili hili la Watanzania kwa sasa ukilisikia linampinga Askofu Gwajima kuhusiana na mtazamo wake wa chanjo za korona unaweza kudhani linachokisema ndicho linachokitenda!

Mtu anapinga hoja za Askofu Gwajima kuhusiana na chanjo za korona lakini ukimwambia aende kuchanja anakuambia hawezi kuchanja kwa sababu zile zile anazozitoa Askofu Gwajima!

Serikali nayo imejikuta katika hali kama iliyomtokea Tundu Lissu baada ya kusikiliza kelele za watu ambao ilidhani watajitokeza kwa mamilioni kwenda kupata chanjo na matokeo yake mpaka sasa hata laki nne hawajajitokeza.

Serikali imeingia “gharama” ya kuingiza chanjo za watu milioni moja na nusu ikidhani ina watu nyuma yake na matokeo yake ni chanjo nyingi zinaenda kupita muda wa matumizi (expire date) bila kutumiwa hasa ikichukuliwa kuwa chanjo zinaharibika baada ya miezi minne.

Ukichunguza utagundua kwa sasa watu wanaoenda kupata chanjo nchini wanafanya hivyo kwa sababu wanataka kusafiri nje ya nchi kwa vile ni takwa la kisheria na sio kwa sababu ni muhimu katika afya zao.

Siwezi kushangaa hata wale wabunge waliokuwa wanamshambulia Askofu Gwajima bungeni kuhusiana na hoja zake za chanjo ya korona kuna baadhi wanaweza wakawa hawajapata chanjo ya korona kwa sababu zile zile za hoja za Gwajima!

Unafiki nchini umekuwa kama ni sehemu ya maisha!
Usifananishe Serikali Na Wakina Gwajima Au Tundulisu.Serikali ikitaka Watu wachanje Watachanja kwa Lazima .Ishu Ni Kwamba Mpk Sasa Hakuna Amri Yakulazimisha watu Kuchanja.
 

Christine1

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
14,563
2,000
Mie ndiyo maana huwa nawaelewa sana CCM kwa kutegemea dola na kikundi cha watu wachache.

Vinginevyo tungeshakuwa tunaongea lugha tofauti.

Hawa wananchi hawa sio wa kuwaamini hata kidogo. Labda kuanzia 2030 ambapo tutakuwa na watu zaidi ya nusu wenye kuelimika.
Na tutakuwa na kizazi tofauti
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,644
2,000
Mshaambiwa Gwajima si askofu bali wa kujipachika. Kwanini mnang'ang'nia urongo na kujidanganya? Nani anampenda huyu kidhabi na tapeli wa kidini na kisiasa?
Mimi na familia ya Bwana tunampenda sana!!

Una jingine au utaendelea kujiwakia na kujichukia mwenyewe kwa sababu ya Mch. Gwajima?
 

Mwanamkiwi

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
497
500
Hao uliowataja hawakupewa uaskofu wa kiprotestanti na papa, hivyo walijipachika; Uaskofu wao katoliki ulikoma siku walipoasi ukatoliki. Hivyo walipoanzisha madhehebu hayo mapya walijipachika uaskofu.

Kwa taarifa yako katika kanisa Katoliki askofu hapewi transfer kwenda kuanzisha dhehebu lingine.

Hivyo Gwajima yuko on the same footing kama hao maaskofu wa kiprotestanti na pentekosti.
Kama wewe ni mkatoliki hujui mafundisho ya kanisa lako. Maazimio ya mtaguso wa pili na pia matangazo kama Dominus Jesus ya mwaka 2000 hurudia kwamba kuna makanisa yasiyounganika na Roma ( wakitofautisha na "jumuiya za kikristo"). Hao ni hasa Waorthodoksi kwa sababu wametunza mlongolo wa kimitume.
Kuhusu Anglikana alikuwa papa Leo XIII tu aliyettangaza mwaka 1896 kwamba hataki kukubali upako wa Waanglikana tena - katika karne zote tangu farakano hadi Leo XIII wakatoliki hawakupinga. - Leo alidai eti mlongolo wa kimitume ulivunjwa baada ya farakano (lakini wakati wa farakano). Halafu kuhusu Walutheri wa USwidi na Ufini wanaotunza mlongolo wa kimitume, Kanisa Katoliki wameepukana kutoa tamko rasmi.
Katika mfano wa maaskofu kama Lefebr aliyejitenga na Papa, hakuna aliyedai uaskofu wake umekwisha; kinyume chake mapadre aliobariki wanatambuliwa.
 

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
681
1,000
Kama wewe ni mkatoliki hujui mafundisho ya kanisa lako. Maazimio ya mtaguso wa pili na pia matangazo kama Dominus Jesus ya mwaka 2000 hurudia kwamba kuna makanisa yasiyounganika na Roma ( wakitofautisha na "jumuiya za kikristo"). Hao ni hasa Waorthodoksi kwa sababu wametunza mlongolo wa kimitume.
Kuhusu Anglikana alikuwa papa Leo XIII tu aliyettangaza mwaka 1896 kwamba hataki kukubali upako wa Waanglikana tena - katika karne zote tangu farakano hadi Leo XIII wakatoliki hawakupinga. - Leo alidai eti mlongolo wa kimitume ulivunjwa baada ya farakano (lakini wakati wa farakano). Halafu kuhusu Walutheri wa USwidi na Ufini wanaotunza mlongolo wa kimitume, Kanisa Katoliki wameepukana kutoa tamko rasmi.
Katika mfano wa maaskofu kama Lefebr aliyejitenga na Papa, hakuna aliyedai uaskofu wake umekwisha; kinyume chake mapadre aliobariki wanatambuliwa.
Mimi ni mkatoliki na ninafahamu mafundisho ya kanisa kama mlei.

Kanisa katoliki ni moja la mitume ila kuna kanisa la mashariki na magharibi na yote yanatambua mamlaka ya papa. Kanisa lolote lisilotambua mamlaka ya papa hilo halina fungamano na katoliki.

Kukusaidia tu maaskofu wote wa katoliki isipokuwa China wanateuliwa na papa. Je hayo makanisa unayodanganya watu humu maaskofu wake wanateuliwa na papa? Hayo uliyoyataja yaliasi mamlaka ya papa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom