Hawampendi Askofu Gwajima lakini wanakubali hoja zake

Hawampendi Askofu Gwajima lakini wanakubali hoja zake

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Tanzania ni moja ya nchi ambayo ukidhani wananchi wake wengi wanachokisema ndicho watakitenda basi utakuwa unajidanganya na nafasi yako!

Historia nchini imeonyesha mara zote wanaodhani wana watu nyuma yao hujikuta peke yao!

Sio muda mrefu aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu alijikuta “peke yake” baada ya kuitisha maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020. Hii ilikuja baada ya kuamini huku akisaidiwa na Sheikh Ponda na “Askofu” Mwamakula kuwa kuna kundi kubwa la watu nyuma yake ambalo aliliapisha wakati wa kampeni ili lihakikishe kura haziibwi na kama zitaibwa litaandamana nchi nzima pale atakapoitisha maandamano.

Uchaguzi Mkuu ulifanyika na baada ya matokeo kuanza kutangazwa, Tundu Lissu aliyakataa na kuitisha maandamano nchi nzima akiamini lile kundi lililokula kiapo kutoka kwa Sheikh Ponda na “Askofu” Mwamakula litajitokeza. Alichokishuhudia hakuamini! Mengine ni historia!

Kwa kiwango kikubwa ni kundi hili hili la Watanzania kwa sasa ukilisikia linampinga Askofu Gwajima kuhusiana na mtazamo wake wa chanjo za korona unaweza kudhani linachokisema ndicho linachokitenda!

Mtu anapinga hoja za Askofu Gwajima kuhusiana na chanjo za korona lakini ukimwambia aende kuchanja anakuambia hawezi kuchanja kwa sababu zile zile anazozitoa Askofu Gwajima!

Serikali nayo imejikuta katika hali kama iliyomtokea Tundu Lissu baada ya kusikiliza kelele za watu ambao ilidhani watajitokeza kwa mamilioni kwenda kupata chanjo na matokeo yake mpaka sasa hata laki nne hawajajitokeza.

Serikali imeingia “gharama” ya kuingiza chanjo za watu milioni moja na nusu ikidhani ina watu nyuma yake na matokeo yake ni chanjo nyingi zinaenda kupita muda wa matumizi (expire date) bila kutumiwa hasa ikichukuliwa kuwa chanjo zinaharibika baada ya miezi minne.

Ukichunguza utagundua kwa sasa watu wanaoenda kupata chanjo nchini wanafanya hivyo kwa sababu wanataka kusafiri nje ya nchi kwa vile ni takwa la kisheria na sio kwa sababu ni muhimu katika afya zao.

Siwezi kushangaa hata wale wabunge waliokuwa wanamshambulia Askofu Gwajima bungeni kuhusiana na hoja zake za chanjo ya korona kuna baadhi wanaweza wakawa hawajapata chanjo ya korona kwa sababu zile zile za hoja za Gwajima!

Unafiki nchini umekuwa kama ni sehemu ya maisha!
 
😂🤣

Hizi mambo hizi basi ngoja tukae kimya na kuangalia mwisho wa huu mchezo.

Yaani wao wenyewe ni waoga kupita maelezo na wanashindwa kumtaja mzee baba late Magufuri kuwa aliwasababishia hofu plus haya ma_online story ndiyo kabisaaa wanapata hofu kubwa!.
 
Umefanya kosa kubwa sana la kiufundi kulinganisha scenario ya serikali/CCM kupuuzwa na wananchi kwenye ishu ya chanjo ya UVIKO 19 na hiyo uliyoita "Tundu Lissu kukataliwa na wananchi"...

Ni kwa sababu ishu ya maandamano ya CHADEMA kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020 ya udiwani, ubunge na Urais ilikuwa ni vita ya jeshi lenye silaha zote (serikali) dhidi ya wananchi/umma (usio na silaha yoyote)...

Ukiwa kama kiongozi makini wa aina ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu, ukiona hivi ni bora ku - retreat na kuwashawishi wananchi wanaokuunga mkono ku retreat pia ili kuepusha maafa na vifo na kisha kujipanga upya kwa namna nyingine...

This is what was done by CHADEMA/Tundu Lissu/Freeman Mbowe last year....

Ni mwendawazimu pekee anaweza kumfanyia hivi mpinzani wake kisha akaja na hoja kujitapa na kutamba barabarani kuwa;

" ....mnaona eeeh, wameniogopa au amekosa watu au watu wamempuuza...!"

Utakuwa unafanya propaganda za kijinga, za kitoto na za kipumbavu kabisa....

Sasa na wewe hebu tuambie, mtifuano wa Ant COVID 19 Vaccine Movement inayoongozwa na Rev. Bishop Gwajima vs Pro COVID 19 Vaccine Movement inayoongozwa na Rais Samia, Bunge la Ndugai, Dr Dorothy Gwajima wapi polisi au JWTZ imeingilia...?

Jibu ni HAKUNA. Bali ni hoja tu zinatawala kwa pande mbele kama ambavyo wewe mwenyewe umekiri ktk andiko lako. Rev. Gwajima kaishinda kwa hoja serikali yote na umma karibu wote uko nyuma yake...

Huu ni uthibitisho mdogo tu kuwa, hata mwaka jana kwenye uchaguzi mkuu, kama hoja ndizo zingeamua nani awe duwani au mbunge au Rais wa nchi hii, CCM mngeangukia pua zetu vibaya sana...!!
 
[emoji23][emoji1787]

Hizi mambo hizi basi ngoja tukae kimya na kuangalia mwisho wa huu mchezo.

Yaani wao wenyewe ni waoga kupita maelezo na wanashindwa kumtaja mzee baba late Magufuri kuwa aliwasababishia hofu plus haya ma_online story ndiyo kabisaaa wanapata hofu kubwa!.

Mkuu;
Hoja yako imeonyesha hujakaa kimya!
 
Juzi kati hapa kuna mtasha mmoja anakwambia hizo dawa zina chembe chembe flani zitakazo weza kufanyiwa usimamizi kutoka sehemu moja.

So mheshimiwa mbunge flani akisoma na kuangalia video ya article kama hizo unadhani ataenda kuweka bega lake pale kwa dada nesi kweli😁?.
 
Tanzania ni moja ya nchi ambayo ukidhani wananchi wake wengi wanachokisema ndicho watakitenda basi utakuwa unajidanganya na nafasi yako!

Historia nchini imeonyesha mara zote wanaodhani wana watu nyuma yao hujikuta peke yao...
Nakubali suala la unafiki kwa watanzania wengi na sio tu watu kuisaliti serikali,nina uhakika pia wale wa upande wa Gwajima wapo waliofanya kinyume.

Kifupi ukweli kuhusu maisha ni kwamba hakuna kitu kitakachoanzishwa duniani kikapata waungaji mkono wote au wa kukataa wote.Na hii ndio tofauti kubwa ya wanaofanikiwa na wasiofanikiwa.

Wanaofanikiwa wakianzisha jambo lao kwa misingi wanaoiona wao kamwe hawadanganyiki na wanaowafuata au kuwazunguka kwasababu ukweli ni kwamba kila nayekufuata hakufuati kwa maono yale unayoyaona wewe,huenda anakufuata kwa manufaa fulani ambayo anahisi binafsi atayapata.Ndivyo ambavyo hata vyama vya siasa vinafeli nchi hii
 
Tanzania ni moja ya nchi ambayo ukidhani wananchi wake wengi wanachokisema ndicho watakitenda basi utakuwa unajidanganya na nafasi yako!

Historia nchini imeonyesha mara zote wanaodhani wana watu nyuma yao hujikuta peke yao...
Ccm inafanya watu wawe wanafiki, wengi wanataka katiba mpya lakini wanaongelea pembeni,
 
Umefanya kosa kubwa sana la kiufundi kulinganisha scenario ya serikali/CCM kupuuzwa na wananchi kwenye ishu ya chanjo ya UVIKO 19 na hiyo uliyoita "Tundu Lissu kukataliwa na wananchi"..
Hakuna tofauti!

Kwani wakati Tundu Lissu, “Askofu” Mwamakula na Sheikh Ponda wanawaapisha wananchi kwenye mikutano yao hawakujua kama wataenda kupambana na vyombo vya ulinzi na Usalama?

Hukusikia maneno waliyokuwa wanatamka wakati wanakula viapo?

Walikuwa wanasema wako tayari kupambana na chombo chochote cha ulinzi na kama mauwaji yatatokea, wahusika watawajibika ICC kujibu mashitaka
 
Mshaambiwa Gwajima si askofu bali wa kujipachika. Kwanini mnang'ang'nia urongo na kujidanganya? Nani anampenda huyu kidhabi na tapeli wa kidini na kisiasa?

Kwani kuna viongozi wa dini hapa duniani ambao hawakupachikwa?

Au unataka kutuambia Askofu huzaliwa ni Askofu bila kusomea mambo ya dini na kupachikwa.

Lazima pia ujue kuwa atoea hukumu ya imani za kidini ni Mwenyezi Mungu na sio binadamu ambaye ni mdhambi.

Wewe mwenyewe unasema Askofu Gwajima anatenda dhambi wakati kuna uwezekano wewe ni zaidi yake.

Acha kuhukumu watu katika imani ya dini.
 
Tanzania ni moja ya nchi ambayo ukidhani wananchi wake wengi wanachokisema ndicho watakitenda basi utakuwa unajidanganya na nafasi yako!

Historia nchini imeonyesha mara zote wanaodhani wana watu nyuma yao hujikuta peke yao...
CCM ni matapelii.

Wewe ni CCM,hivyo wewe ni tapeli.

Jana ulimuunga mkono mwendakuzimu kukataa chanjo, kisa tu ni bosi wako. Leo unamuunga mkono Mh. Samia kuhusu watanzania kuchanjwa, kisa tu ndio bosi wako.

Wewe ni "ma..ya " .
 
Kwani kuna viongozi wa dini hapa duniani ambao hawakupachikwa?

Au unataka kutuambia Askofu huzaliwa ni Askofu bila kusomea mambo ya dini na kupachikwa.

Lazima pia ujue kuwa atoea hukumu ya imani za kidini ni Mwenyezi Mungu na sio binadamu ambaye ni mdhambi.

Wewe mwenyewe unasema Askofu Gwajima anatenda dhambi wakati kuna uwezekano wewe ni zaidi yake.

Acha kuhukumu watu katika imani ya dini.
Hawapachikwi. Kwanza, wanasomea. Pili, wanatawazwa kwa mujibu wa taratibu za wahusika hata kama hatukubaliani nazo tokana na ukoloni wake.
 
Mie ndiyo maana huwa nawaelewa sana CCM kwa kutegemea dola na kikundi cha watu wachache.

Vinginevyo tungeshakuwa tunaongea lugha tofauti.

Hawa wananchi hawa sio wa kuwaamini hata kidogo. Labda kuanzia 2030 ambapo tutakuwa na watu zaidi ya nusu wenye kuelimika.
 
Back
Top Bottom