Hawa Zoom Tanzania Ni Namna Gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa Zoom Tanzania Ni Namna Gani

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mtanzania in exile, Feb 17, 2012.

 1. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Habari zenu watanzania wenzangu. Mimi ndio kwanza nimejiunga leo na ukumbi huu.

  Nimeona matangazo ya kazi kadhaa ambayo yanatumwa hapa kutoka kwa Tanzania Directory for Business, Entertainment & Travel Info jambo
  ambalo lilinifanya kuitemebelea website yao kuona nafasi za kazi zaidi. Cha kusahngaza ni namna website hii
  inavyoanika wazi CV za watu wanao submit kwenye website yao

  Hii mimi sijapata kuiona na naamini wengi watakubaliana nami. Unapo upload CV katika recruitment site hutegemei
  hata siku moja CV yako kuwekwa public, yaani kila anaeitembelea website hiyo anaona ulichoandika. CV ni private thing
  na mtuma cv anategemea kuwa wanaotafuta wafanyakazi ndio pekee wanaopewa access ya kuona cv zao. CV ni chombo
  cha kuuza talent yako ili uajiriwe, kuna competition nyingi na kila mmoja anapenda kuwa CV yake iwe kivutio zaidi kwa
  mwajiri na kuitwa kwa interview.

  Sasa kama hawa zoomtanzanaia.com wanziweka wazi cv za watu, hapo wanatowa chance kwa watu wengine kukopi cv za watu
  na kuzifanya zao, jambo ambalo halipendezi na sio zuri. Ningeliomba wahusika wa website hii wasite mtindo huu.

  ahsanteni
   
 2. t

  thinka JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Acha uoga cv hata mtu akikop atathibitisha vp kaama ni yake.zinawekwa waz kwasababu mwajir anaetaka mtu anapita website hyo akiipenda cv yako anakuita.me sion shida hapo
   
 3. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,719
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Shida ipo si sahihi kuexpose information ya mtu. Anything can be done kutumia information za mtu kwa hivi aliyeleta mada yupo sahihi kabisa.
   
 4. Myelife

  Myelife Senior Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ee bwana umenishangaza sana, yaani hii ni kesi kubwa sana na hatari kwa kampuni husika, sasa wewe unasema hakuna!!! Sitaki kukutukana lkn naamini hujui haki zako, kisheria mtu kuanika hadharani nambari yako yako ya vm bila ridhaa ni kesi yaweza kuamuliwa na mahakama kuu, sasa je cv ni vp!! Km upo karibu na vyombo vya habari soma kuhusu issue ya wajumbe wa baraza la senate na carrier IQ, serikali ya singapore na hath, serikali ya uingereza na News of the World Corporation na mawaziri na wakurugenzi wangapi wamepoteza kazi, jana paliibuka nyingine ya gazeti la Sun huko UK, kesi zote ni kuhusu privacy of clients,
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwani terms and conditions za kutumia hiyo website zinasemaje kuhusiana na hilo suala? Always read the small prints
   
 6. Myelife

  Myelife Senior Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tafadhali tambua kuwa HR wako anaweza kuadhibiwa vikali kama ataanika taarifa zako hadharani hii ni kwa sababu taarifa zako ni muhimu sana, ni km vile dk kuweka taarifa za mgonjwa wake hadharani ni kusa kubwa kitabibu, ukitaka kujaribu uzito wa kosa nenda kachukue mobile no ya Rais, mkuu wa majeshi, jaji, au balozi halafu kaichapishe gazetini bila ridhaa ya maandishi toka kwao, naamini nimekuelisha vya kutosha na tangu leo tambua, taarifa zako binafsi yaani biographical data ni siri kati yako na mwajiri,
   
 7. Candy kisses

  Candy kisses JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  but mmesoma kwanza terms and condition ya huo mtandao au uvivu kusoma kiingereza
   
 8. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  wewe thinka, usijifanye mjuaji, sina lengo la kuanza kugombana na mtu au kuanza kutukanana, hasa ukizingatia ndio kwanza naanza katika huu ukumbi. Tabia ya kumwita mwenzako muongo sio nzuri, hususan ukizingatia hata hunijui kabisa. Sijui mwenzangu una umri gani, inaonyesha kuwa huko mature kwa tabia ya kuwaita watu majina kwa sababu tu hukubaliani na wanayosema. Grow up.

  Unauliza suali la kitoto hasa. Labda nikupe mfano ili niweze kukujibu suali lako. Mfano mimi na wewe tumesoma fani moja iwe chuo kimoja au vyuo mbali mbali. Mimi nimekaa chini kwa muda mzuri na kuandika CV ya nguvu, wewe umekwarupuka tu na kuandika cv mbovu ile mbaya. lakini ulipotembelea zoomtanzania website ukaiona cv yangu na kukuipenda, ukaamua kuikopi (copy and paste) neno kwa neno. ulichobadili ni personal details zangu kuwa zako na chuo nilichosoma ukaweka chako. That is it, ni CV ya nani hiyo? ni yako au yangu sasa ambayo ipo mbele yako? Vipi tukusaidie jawabu hapo?

  Hivyo ndivyo nilivyosema, watu wanaweza kukopi idea za cv za watu wengine na kutumia maneno na style za watu wengine kwenye cv zao. Tatizo ni kuwa wakati sisi wengine hukaa na kupoteza muda mrefu kuandika cv zetu kuna wengine wavivu kama wewe hujipatia cv nzuri kwa kukopi za watu wengine.

  I hope umenifahamu.
   
 9. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Acheni kupiga kelele za term and condition. Ndio sikusoma term and condition. Kwa sababu mara tu ya kuona namna wanavyowacha wazi taarifa za watu nikaamua kuto-upload cv yangu. Ingawa sijasoma term and condition zao, siamini kama wameweka wazi hilo, na kama wameweka wazi basi ni jambo la kushangaza sana. Sijawahi kuona site yeyote ile duniani yenye utaratibu huo.
   
 10. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nimesahau issue moja yako wewe thinka na nimeamua kurudi kwani unahitaji kuelimishwa kidogo. CV haziwekwi wazi kinamna hii wanayofanya zoomtanzania, wenye site ambazo watu wanaweka cv zao huwa wanaweka sehemu ambayo waajiri wanapewa access ya kuona cv za waombaji kazi, hii inazuia kuwacha cv za watu kila mtu kuziona kiholela holela. Ni kwa mfumo huo ndio website hujipatia kipato kwa kwa muajiri kuweza kuona cv za watu anatakiwa kujisajili na kulipa fidia. Sijui mwenzagu upo nchi gani lakini labda jaribu kuona mifano ya website za nchi nyengine mfano UK Jobs - The UK's Leading Job Search - CV-Library.co.uk, Find Jobs. Build a Better Career. Find Your Calling. | Monster.com, cwjobs.co.uk, Find your next job with JobServe na utaona zote haziweki cv za wazi.
   
 11. T

  TUMY JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana mkono mia kwa mia na ulichokisema mkuu, watu wasome terms and condition kama zinaruhusu ama la na kama haziruhusu ni kosa kubwa sana hilo ila kama hamkusoma terms and condition na wao labda wameeleza basi ni funzo tosha siku nyingine
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, international job sites wanachofanya ni kutoa option ya ikiwa CV yako iwe public or viewable on request. Hata hivyo, wao huwa wana-advice kwamba CV yako iwe public. Lakini pamoja na yote hayo; hata kama CV yako itakuwa public, bado ur personal infos haziwezi kuwekwa public!
   
 13. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  NasDaz, usemayo si sahihi kabisa. Kwanza ningelikuuliza kama umeangalia hii website tunayoijadili? umeona cv za watu zilicyowekwa wazi wazi? sasa niambie ni international jobsite gani inayofanya utumbo huo?

  Nadhani pia umeshindwa kuelewa wanaposema uweke cv yako public. Hiyo wana maanisha kuwa unapoweka public ndio recruiters wanaiona cv yako, sio kila mtu. Yaani mimi na wewe tumekwenda kwenye website kutafuta kazi au kuweka cv zetu hutuoni kabisa cv za watu wengine zikiwa public au sio public.

  Jaribu kwenye site yeyote ile utaona kuna link ya recruiter, ukibonyeza hapo ni lazima uwe na jina na password ndio uingie. Recruiters hulipia kupata access hiyo. Narudia tena hakuna hata international jobsite wanaoweka cv za watu nje nje kwa other job seekers to see them. nenda site hii hapa kwa mfano https://www.cwjobs.co.uk/Authenticated/Login.aspx?ReturnUrl=%2f utaona kuna option ya recruiter ku-log in.

  Sababu kuu mbili za kufanya hivi ni kwanza privacy ya candidates ikijumuisha personal details zao, ambazo si ruhusa kuziweka wazi mtandaoni, pili hio ndio moja ya njia ya job sites kujipatia pesa kwa kuwa charge wanaotafuta watu wa kazi.
   
 14. t

  thinka JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  @mtanzania in exile.so sory nahisi nimekuudhi sana.samahan mkuu sikukusudia kukuudhi
   
 15. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Hakuna tatizo hapa, kila mtu ameweka CV yake kwa hiari na CV sio kitu cha siri anyway.
   
 16. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  bwna hata mm cion km kuna tatzo hapa ila watu wanaona kila kitu kibovu hapa TZ.kuna mtu kabisa hapa JF anamaliza mwaka hajasifia kitu.swala la cv yko kua xposure hakuna ishu ikiwa kuna watu cv zao ukigoogle tu unazipta then hata km ni ishu mwisho wa siku kuna vyeti vinavyohitajika pale bana.
   
 17. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Baada ya kusoma post za wengi hapa, nigundua na kufahamu kuwa wengi wanaamini kuwa hapana issue yeyote kwa recruitment agency au job site kuweka wazi details za mtu. Nimehisi huo ndio mtizamo au ndio mwelekeo wa ndugu zetu nchini Tanzania. Labda nchini Tanzania hakuna sheria juu ya suali hili la kuweka hadharani personal details za mtu na ndio maana hata wananchi nao hawaoni lipo wapi kosa hapo.

  Kwanza niwajibu wale wanaosema kuwa uki google unaona CV za watu. Sikatai hilo. Nadhani mnashindwa kufahamu ninachokisema. Kuna tafauti kubwa baina ya mtu kuweka details zake mtandaoni na kuweka details za mtu mwengine mtandaoni bila ya idhini yake. Ikiwa mtu kaweka details zake mwenyewe hapo hapana kosa kwani ni uamuzi wake. Lakini mtu mwengine kuweka details za mtu huyo huyo bila ya idhini yake ni kosa.

  Labda kwa kuwa nyumbani hakuna watu wenye akili za ajabu kama stalkers au watu wanaowatafuta watu kuwalipiza kisasi kwa sababu zozote zile au hata hitman/assassins na ndio maana watu hawajali kuweka personal details za watu hadharani. Hiyo ni moja tu katika sababu nyingi za sheria ya data protection na privacy ya personal details ambayo inasisitizwa duniani kote

  Katika mataifa mengine hilo ni kosa kubwa mno. Na kwa mtu kama mimi au yeyote ambae yupo nje ya nchi (samahani sikusudii kujisifia kuwa niko nje, yeyote anaweza kuwepo nje ya nchi, ni mfano tu wa kuweza kueleza point yangu) na ameshaelewa juu ya issue ya siri ya personal details za mtu, inakuwa vigumu unapojaribu kutafuta kazi nyumbani kwa kutumia mtandao unagundua kuwa details zako zinawekwa wazi kwa kila mtu kuziona badala ya recruiters only.

  Itawashangaza sana ndugu wengi kuwa hata kumpa mtu number ya simu ya mtu mwengine bila ya ridhaa yake (mwenye number) huweza kukufikisha pabaya, na ndio maana wafanyakazi wa mapokezi maofisini daima hawakupi number ya mobile ya wafanyakazi wao bali anakupa number yao ya ofisini (mapokezi). Hilo tena huenda nyumbani halifanyiki hili pia.

  Kwa ufupi nasema kuwa nimeelewa kwa nini wenzangu mnaona hakuna kosa walilofanya zoomtanzania, nilichojaribu leo ni kueleza kwa nini mimi nimeona hilo ni kosa ukizingatia sheria za kimataifa za data protections na personal privacy issues.

  Ahsanteni. Nadhani umefika wakati wa mimi kuufunga mjadala kwa upande wangu na nategemea nimeeleweka kwa kiasi fulani sababu za kushangazwa na nilichokiona zoomtanzania.
   
 18. YUSHIN

  YUSHIN Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Anachosema jamaa ni kweli kabisa, anayetakiwa kuiona CV yako ni yule mlengwa(mwajiri)
  na sio mtu mwingine yeyote.
   
 19. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  ni kosa kubwa kuanika CV ya mtu hadharani bila ridhaa yake. Kam recruitment agency kwa kawaida wao ndio ambao wanawainterview na watakaoridhika nao wanakwenda kuwauza kwa company ambazo zina contract now au ambao watapenda wao wawatafutie watu.
   
 20. Oneya Fuko

  Oneya Fuko Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo watz hawachukulii vitu vya msingi serious. Wengi wao wanachukulia vitu kwa uwepesi!!
   
Loading...