Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 897
- Thread starter
-
- #21
brazameni, wengi tu hapa wanafahamiana, na wengi tu ni watoto wa DAR, ila kama jinsi tulivyo binadamu, wengine wakimya wengine waongeaji sana... hivyo kuna wengine wanayajua haya yote unayo ongelea humu na wanafahamiana na wale unaowataja, ila ndiyo hivyo tena, hayo ni yao na ndugu, jamaa au rafiki zao... siyo ya ku share na kila mmoja hapa ukumbini!
Baadae,
SteveD.
Again, watu wasikuzuge kuongelea siasa hapa ukawaona siyo watu wa mjini.... ni progression tu watu wanafanya katika maisha yao, hivyo unaweza kukuta Mkjj ni mtoto wa mjini kupita... wewe mchokoze akutolee data zako.... he he.
SteveD.
he he he, umeniacha naumwa mbavu hapa brazameni... duuuh, eti jeshini Ruvu au Makutupora... miye nilikimbia hilo..niliepuka!!
SteveD.
Ahh hizo topic za jeshini zikianza mie huwa najisikia veryuncomfortable nikiwa na washikaji sasa matokeo yake huwa nina krem..jina la jeshi,kiongozi mwaka ule allikuwa nani nani yaani niwajue wawili watau...maswali yakinizidi huwa naongopa eti niliomba uhamisho nikapata Dar pale mlalakua ...surprisingly watu huwa wananiamini na saa zingine huwa nawabuly wale ambao hawakuenda jeshini as if mie nilienda
trust me figures nyingi za kule SIASA forums zinasound kama zilipitia huko Jeshini
ebwana hivi uliwahi kuwa member wa USIS katika miaka ya early 90's unajua tena amabo ya TV bongo ilikuwa bado huku Mohammed Farah Aideen alikuwa akipelekana puta na wanyamwezi kule somalia basi USIS walikuwa wanaonyesha 30 minutes video za CBS NEWS ...kama hupajui basi ni pale Tanganyika motors juu ...nadhani mwanakijiji atakuwa anapajua maana yule mwenezu ni mtu wa KLM!
Kuhusu, USIS nilienda mara moja tu kuchukua form za Toefl, mtihani wenyewe sikufanya...si unajua tena, wengine vibonde wa lugha za wenzetu bwanaa.. ila ilikuwa bomba tu kwenda kwenye hilo jengo la vioo tupu na kuonana na mademu wa mule kutoka shule mbali mbali bongo wakitafuta makaratasi ya kuruka viwanja...wakati ule hakukuwepo na jingine kama hilo, na lile la opposite maktaba sijui la mkubwa gani nasikia, lilikuwa bado halijajengwa..
SteveD.
Oyaaa Brazameni mi mtoto wa mjini wewe....ukitaka mambo uswazi mi anga zangu zilikuwa Sinza abajalo, Magomeni kwa macheni, mwenge stendi ya basi, Savei kontena, mlalakuwa ndani ndani kwenye klabu za wanzuki
Wewe Nyani, wanzuki ulikuwa unakunywa kweli au mikwala tuuu...lol
SteveD.
Mie anga zangu zilikuwa Ilala flats, Kariakoo, Msasani, Migomigo...lakini muda mwingi nilikuwa boarding school mikoani( moro na arusha). Ilala flats pale kuna chizi mmoja anaitwa Nadi sijui unamjua?? Martin Kinguruwe, wakina MT na mob nyingine karibu yupo ipo reading!!!!. Mie nilikuwa na mix, mtaani kwa sana wakti wa likizo za zile break za kumaliza shule, lakini kwa ujumla nilikuwa joni kisomo!!.
Nilikuwa Visa ya Mnyamwezi Jo'burg,SA, wakti wa bomu la Osama!!!.
Nitaku-PM siku nikiwa natia timu kwa "wajameni" kuhusu hilo dili la petroli.
Aaah kumbe we kiwanja umeingia karibuni tu..
Hamna noma wala nini masela wangu, nimekuelewa...NN na Steve,
Sawa bwana, sio mabomu ya 9/11.......hiyo ni mabomu ya 1998 Dar na Nairobi, kukawa hakuna visa dar....watu ikawa inabidi waende Kampala, Lusaka, na washkaji wengine waliingia UK kwa gia ya Visa.
Sasa kama 1998 ni juzi na ni "9/11 aftermath" basi juzijuzi haina maana tena!!!!!.
....
nayakati fulani za weekend nilikuwa nazuka kuangalia ngoma za kimakonde kule msasani (zilikuwepo kila jpili).....baadaye jioni nilikuwa najiunga pale nje ya Drive-Inn na washikaji tunapiga mihogo yetu ya kuchoma na pilipili huku tukicheck sinema bubu........wakati huo Julius Nyaisanga anatuburudisha na "Ring my Bell" izaa ya biashara RTD
eee bwana Nyani naikumbuka sana Mande Guest House.....................duuh mshikaji umenikumbusha mbali sana
Ktk ulowataja, Dela soul yupo NYC ana mke mtasha, Sindila yupo Cincinati, OH....Jump Around yupo Columbus, Rhymson mara ya mwisho kumwona ilikuwa Bongo safarini Canada, Y-thang nilimwacha Muhimbili akiwa mwaka wa nne, nadhani ni doctor somewhere...............................baadhi ya wengine nasikia mateja, waliovuta haya, lakini life goes on!!.