Hawa wadudu wanao wakawaka usiku

Hawa wadudu wanao wakawaka usiku

Ahsante mkuu!
Nikiwahi kuona makala Youtube ikiwaelezea.Kuna mfumo wanatumia ambapo kemikali maalumu hupambana na kutoa mwanga. Kitu kama oksijeni na calicium(sina hakika sana).

Lakini mwanga inadaiwa mwanga unaozalishwa hauzalishi joto kama bulb yako sebuleni maana itakuwa hatari kwa kiumbe huyu.

Mwanga huwasaidia yafuatayo:
1. Kutambuana kati ya jinsi moja na nyingine. Maana yake me na ke hutoa mwanga wenye nguvu tofauti.

2.Ni namna ya kuvutiana kufanya "ngono." Inasemekana madume ndiyo hushindana kutoa miali mikali. Jike atavutiwa na dume mwenye tochi ya ukweli.

3.Jamii moja na nyingine hutofautiana kwa mwanga. Hivyo,husaidia kutambuana


Wadudu hawa ni "nocturnal" , yani huwa active usiku kama vile mende na panya.

Wenye fani zao watadadavua zaidi


Ninawasilisha
 
[emoji41][emoji41][emoji41]
Tunaoishi vijijini tunawafurahia sana hapo viumbe ikiwa unakatiza zako usiku baada ya mvua kunyesha unapishana nao afu kwa mbele unapishana na konokono na kwa mbele zaidi unapishana na jongoo na mwenzake mnyoo..
Napita
 
Wakuu naombeni mnijuze kiundani kuhusiana na hawa wadudu, kuna sehemu wanaitwa vimulimuli[emoji856][emoji856]

Huwa wanakuwa wengi msimu wa mvua hasa majira ya usiku, huwa utawaona wengi wanawaka waka fulani hivi......

Mimi huwa siwaelewi kabisa, inakuwaje wanatoa mwanga mithiri ya indicators za gari?

Je huo mwanga unazalishwaje katika mwili wao? Au wanauakisi mchana? [emoji848][emoji848]

Siwaelewagi kabisa! Mnijuze aiseee[emoji41][emoji41]

Hawa ni aina gani ya wadudu, na wanaitwaje kitaalam(kisayansi/kiingereza)?
Mkuu mi mwenyewe nimekua nikijiuliza hili swali kwa miaka sasa bila majibu. Umenifurahisha sana mkuu nikahisi ni Mimi tu ninaesumbuka na hili jambo, kumbe tupo wengi.
 
Hiyo ni bioluminescence, ni kitendo cha kuzalisha mwanga kutokana na metabolic chemical reactions mbali mbali zinazondelea ndani ya miili yao
 
Back
Top Bottom