Hawa Wabunge wa Rungwe wanastahili viboko kwa kuwaweka kina mama katika hali hii

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,415
22,026
Kuna video inazunguka ikionyeshwa hali ambayo katika kijiji fulani huko Rungwe, Tukuyu wanaikabili. Kina mama wanalazimika kuning'ninia kwenye kamba kama nyani ili kuvuka mto, wakiwa na hatari sana ya kutumbukia mtoni hata kupoteza maisha! Hivi wabunge wao wanafanya nini?

Hebu angalia hii clip ufanye judgement yako mwenyewe. Labda utaelewa kwa nini Magufuli anasema ni lazima tuwe na uchungu na wananchi wetu wanaoteseka.

v1.png

v2.png
 
Kuna sehemu moja pia ipo maeneo ya iyovi Iringa msituni kuna watu wanavuka kwa namna hiyo
 
Unaweza kukuta wabunge wa maeneo hayo waliwa bungeni wanatumia muda mwingi kupingana na hoja za wenzao badala ya kutetea na kuoji kuhusu ni lini karaha ka hiyo ya fudhehesha taifa Zima kwa ujumla itaisha lini.
Agekuwa JKN hakika asingeruhusu ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati kwa wananchi wake pana hali kama ile!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna video inazunguka ikionyeshwa hali ambayo katika kijiji fulani huko Rungwe, Tukuyu wanaikabili. Kina mama wanalazimika kuning'ninia kwenye kamba kama nyani ili kuvuka mto, wakiwa na hatari sana ya kutumbukia mtoni hata kupoteza maisha! Hivi wabunge wao wanafanya nini?

Hebu angalia hii clip ufanye judgement yako mwenyewe. Labda utaelewa kwa nini Magufuli anasema ni lazima tuwe na uchungu na wananchi wetu wanaoteseka.

Kama hali ndo hii basi daraja la kigamboni ni anasa.
 
na wabunge wa rungwe tangu nchi ipate uhuru viongozi ni mafisiemu tuuuuu.wananchi wanapata shidaaa but acha tu waendeleee kuisoma nambaaaa
 
mboi kuchukua ruzuku zote 2006/2007 na kisha kutoa kwa chama kama mkopo na chama kikarudisha kwa riba sii ufisadi. unaposema ufisadi ni mfumo ni mfumo upi zaidi ya huuu
 
Kuna video inazunguka ikionyeshwa hali ambayo katika kijiji fulani huko Rungwe, Tukuyu wanaikabili. Kina mama wanalazimika kuning'ninia kwenye kamba kama nyani ili kuvuka mto, wakiwa na hatari sana ya kutumbukia mtoni hata kupoteza maisha! Hivi wabunge wao wanafanya nini?

Hebu angalia hii clip ufanye judgement yako mwenyewe. Labda utaelewa kwa nini Magufuli anasema ni lazima tuwe na uchungu na wananchi wetu wanaoteseka.

Mimi nafikiri ungesema serikali maana wabunge wameyakuta hayo na mwenye kujenga daraja ni serikali kutokana na kodi za wananchi
 
Jawabu wananchi wakae karibu karibu! sasa kama kijiji ni mbali na hapafikiki ni jukumu la nani kuwaletea maendeleo?

Namkumbu sana Mwalimu na Kawawa juu ya Vijiji vya ujamaa!!
 
Mimi nafikiri ungesema serikali maana wabunge wameyakuta hayo na mwenye kujenga daraja ni serikali kutokana na kodi za wananchi

Mkuu, serikali inachochewa kutenda na wabunge. Hapa simaanishi wabunge watatue hili tatizo kwa uwezo wao.

Hata hivyo, nasikia hili ni eneo la mbunge anayeitwa Sauli sijui, ambaye ni mmiliki wa hoteli kadhaa zinaitwa Landmark. Nasikia wakati wa kampeni alikuwa akitamba kwamba matatizo madogo madogo kama haya hatakuwa anahitaji fedha za serikali atatatua kwa fedha yake mwenyewe. Sasa kiko wapi?
 
P0le ndugu yangu inaelekea hujui chochote
Wewe ulitaka niseme wabunge wa sasa sivyo? Ina maana hao wabunge wa zamani hawakuona hili tatizo, au huu mto umejitokeza wakati wa wabunge wa sasa?

Najua tatizo lako. Una mapenzi sana na maprofessor Mwandosya na Mwakyusa, hufikirii kwamba wanapaswa kuhusishwa. Lakini kumbuka pia Prof Mwandosya japo alikuwa wakati fulani waziri wa maji, kuna sehemu katika halmashauri ya Rungwe zina tatizo kubwa la maji, pamoja na kwamba wana maji ambayo yanakuja mjini kwa njia ya gravity, ambapo ina maana gharama yake ni ndogo sana, ni ni moja wapo ya mifumo michache sana nchini inayosambaza maji toka chanzo kwa njia ya gravity. Hivyo utaona pamoja na kazi nzuri walizofanya watu kama kina Mwandosya, kina viporo waliacha na hadi leo hatuelewi kwa nini waliamua "kwa makusudi" kuacha viporo hivyo.
 
iulize serikali ya ccm kwa zaidi ya miaka 50 iliyokuwa madarani imefanya jitihada gani za katika kutatua tatizo kama hili?
 
Yaani huko viteputepu ndio nyumbani kwake na utaweka madaraja mangapi hiyo rungwe na kyela yake kwa idadi ya mito waliyonayo acha waboreshe ukakamavu wao wakati mipango mkakati inaendelea.
 
Yaani huko viteputepu ndio nyumbani kwake na utaweka madaraja mangapi hiyo rungwe na kyela yake kwa idadi ya mito waliyonayo acha waboreshe ukakamavu wao wakati mipango mkakati inaendelea.

Sawa Mkuu, tuwaache waboreshe ukakamavu hadi hapo mkeo, au mwanao au hata mama yako atakapovunja kiuno akijaribu kutumia hizo daraja za kamba ndio ttutakapowawekea madaraja ya kudumu ili wavuke kwa usalama.
 
kuvuka kwa kamba.png
mto wa kamba.png
wananchi wavuka kwa kamba.png

Habari‬:Kukosekana kwa daraja katika mto Mbaka unaotenganicha kitongoji cha Kibundugulu na kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe kumekuwa kukisababisha maafa ya mara kwa mara kwa wananchi ambao hulazimika kuvuka mto huo kwa kamba na wengine kupiga mbizi kwa ajili ya kufuata huduma muhimu za kijamii ng’ambo ya mto huo.
 
Back
Top Bottom