Satuuuu
JF-Expert Member
- Dec 3, 2015
- 1,849
- 1,993
Hivi karibuni kuliwekwa Video humu JF ikionesha wakina mama wakivuka ktk mto Mbaka kwa kupita juu ya kamba huko Rungwe.
Uzi wenyewe ni huu: Hawa Wabunge wa Rungwe wanastahili viboko kwa kuwaweka kina mama katika hali hii
Habari njema ni kuona leo Mh. Jenista Mhagama pamoja na mbunge wa huko kufika eneo husika na kuahidi kivuko katika mto Mbaka.
Kukosekana kwa daraja katika mto Mbaka unaotenganicha kitongoji cha Kibundugulu na kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe kumekuwa kukisababisha maafa ya mara kwa mara kwa wananchi ambao hulazimika kuvuka mto huo kwa kamba na wengine kupiga mbizi kwa ajili ya kufuata huduma muhimu za kijamii ng’ambo ya mto huo.
Kero ya kukosekana kwa kivuko kwenye mto Mbaka imesababisha athari kubwa kwa wananchi wa kitongoji cha Kibunduguru, hali ambayo imemlazimu mbunge wa jimbo la Rungwe Sauli Henry Amon kutoa taarifa katika ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ili serikali iweze kuchukua hatua za kuwasaidia wananchi hao.
Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia maafa, Mheshimiwa Jenesta Joachim Mhagama amelazimika kutembelea eneo hilo na kutoa agizo kwa mwenyekiti wa kamati ya maafa mkoa wa Mbeya, kufanya tathimini ya athari za mto huo na kupeleka taarifa ofisini kwake ili serikali iwezi kuchukua hatua za haraka.
Hata hivyo afisa mipango wa wilaya ya Rungwe, William Makufwe amesema kuwa tayari Halmashauri yake imeanza kuchukua hatua za kujenga kivuko cha miguu kwenye mto huo, mradi ambao hata hivyo haujawahi kupata fedha za kuukamilisha.
Congrats to JamiiForums.