Hawa VoA wanamlisha maneno Rais Magufuli, hakusema chanjo hazifai kama wanavyoripoti wao

Wewe ndio wale wale wa peoples power ni wapi alisema chanjo ya corona haifai?
Akhiy mimi sikusikiliza hotuba yake ila kuna mtu ametuma clip hapo juu nimesikia.. anasema.. kuna watanzania walienda kupata chanjo nchi fulani halafu wakaja na corona mbaya
Pia anasema kama wazungu wangekua na uwezo wa kutoa chanjo mbona hakuna chanjo za magonjwa mengine
Camera and Video are not lying
 
jpm ni nabii,tatizo liko wa majinga machache yasiyojitambua.

kama yanhekuwa na akili hata za kuvukia barabara ilivaa yachutame baada ya kuvuliwa nguo kwenye covid awamu ya kwanza.
 
Duh uelewa nao ni tatizo...., Hivi unajua madawa huwa ni gharama sana na kampuni zinatumia mamilioni ya pesa kwenye research, na return on investment mara nyingi inategemea nchi zenye buying power waweze kununua..., kwahio huwa kuna dawa wanazitoa kama ruzuku kwa nchi masikini..., pia nchi kama india huwa wanatoa dawa kama zile za wadau waliofanya research na kutumia mapesa (wao gharama yao huwa ni ndogo) hivyo kisheria dawa nyingi zinaweza zikawa zilezile zikapatikana india au hata mexico ila haziruhusiwi kuingia Canada au USA (kule kuna alternatives ya bei kubwa)

Kuna Documentary moja watu walikuwa wanatoka USA kwenda MEXICO wana-smuggle dawa ili wawaletee ndugu zao US, as they are cheaper there...

Kuhusu kufanyiwa research Africa (hii inatokea sana) as its cheaper kwa corporation kuwafanyia watu masikini hakuna implication kama wakifanya research huko kwao, implication ni kubwa sana (huko inabidi mtu asign akubali kufanyiwa research na kwa gharama kubwa) Africa ni swaga twende (sio kwamba ni ubaguzi bali it makes economic sense kwao)

Cha kufanya na sisi tuanze kufanya research na kutengeneza zetu, pia hatukatazwi kuzifanyia research zilizopo ila side effects mara nying it takes miaka (no body knows ni try and error) kwahio mwisho wa siku choice is yours either you definitely die now...., au maybe in the many years down the line.....
Paragraph ya mwisho ndio nimeilewa zaidi ingawa sina uhakika kama resources zinazohitajika tunazo na zenye viwango stahiki.
 
Habari wadau wa JamiForums,

Mara nyingi hivi vyomba vya habari vya kibeberu vinatumika vibaya japo vinafahamu kuwa vinatumiwa vibaya.

Jana Voice of American (VOA) kimeweka chapisho kwenye Mitandao yao ya kijamii na kusikika kwenye vyombo vyao vya habari hasa kwenye social networking vikisema kuwa Rais John Pombe Magufuli amesema chanjo za corona hazifai jambo ambalo sio kweli ila ni upotoshaji kwa ajili ya Malengo yao binafsi.

Jana Rais John Pombe Magufuli hakusema chanjo hazifai ila aliitoa Muongozo ni kwa namna ipi tunatakiwa kuzikubali chanjo kwa kuilekeza Wizara ya Afya kuhakikisha sio kila chanjo wanayoletewa wanaipokea tu bila kufanyia uchunguzi na akatolea mfano Baadhi ya chanjo ambazo zimeshatolewa na badala ya kuwa tiba ikawa tatizo.

Pia akatoa mfano mwingine wa chanjo ya kansa kwa kusema wao ndio Wanaongoza kwa kufa na Kansa kwanini hizo chanjo wasijidunge kwanza wao na badala yake wazilete kwetu.

Kwa sauti ya Marekani mnapotoa sauti zenu muwe mnajaribu kutoa na za wizi wa kura wa Trump sio kupotosha Rais Magufuli kasema Wizara ya Afya iwe makini kwenye kuzipokea chanjo isikubali kila chanjo inayoletewa kwani zingine sio nzuri.

Serikali kwani hamna uwezekano wa kuwawajibisha hawa watu wanaomuwekea Rais Maneno Mdomoni?

View attachment 1687900
Kwa hiyo ALISEMA ZINAFAA?
 
Utawala wa anko umeibua wehu wengi sana wanaojivisha ujasusi mashudu..... Babaako kaongea kabisa hizo pumba wewe unakuja spidi unapinga... Haya nenda bungeni umeshateuliwa
 
Naunga mkono hoja. JPM kaongea kitu very sensitive kwenye jukwaa la kawaida sana. Kwa maoni yangu hayo aliyoyaongea yalipaswa kuongelewa kwa kina zaidi kwenye vyombo vyetu vya usalama wa taifa. Anyway inawezekana kafanya vile ili na wenye akili waelewe sababu za msimamo wake kuhusu hili janga.

.... ongeza na za kwako.
asante kwa comment yako jamaa. kuna watu yaani hata wakiambiwa kuna sumu katika hizo chanjo watazikimbilia tu kwasababu zimetoka kwa weupe. ugonjwa mmoja c19 sasa mbona chanjo ziwe na mipaka,? kunanini?
 
Back
Top Bottom