Hawa VoA wanamlisha maneno Rais Magufuli, hakusema chanjo hazifai kama wanavyoripoti wao

NI KWELI HAZIFAI.
sio yeye tu hata mimi nazikataa.
Watumie Kwanza wao wenyewe WAPONE
 
Mleta mada uzalendo hauna maana hiyo, aliongea kweli haifai. Ulitaka waandike vip hao VoA? Hapa jambo la muhimu ni viongoz wetu kutumia hekima na busara waongeapo na sio kila kitu cha kumwambia mwananchi vingine vibaki kwenye makablasha ya kiinterejensia.
 
JPM acha kupambana na mabepari utatuumiza sisi watu wakawaida bure, wewe dili nasisi tumesha kuzoea tu, mambo mengine ni sensitive baki nao utapotosha watu wakati hatuna uwezo wakupambana namajanga yetu.
 
Aliongea hadharani wewe unayekataa ndo unampotosha!! Haka hutaki chanjo tengeneza ya kwako, au uje na majibu ya kitaalam kua chanjo flan ina mapungufu flan au imetengenezwa na kemikali flan ambayo ina madhara....sio kuongea tuu bila kua na uthibitisho wa kitaalamu

Common sense is not also common to everyone.
 
Habari wadau wa JamiForums,

Mara nyingi hivi vyomba vya habari vya kibeberu vinatumika vibaya japo vinafahamu kuwa vinatumiwa vibaya.

Jana Voice of American (VOA) kimeweka chapisho kwenye Mitandao yao ya kijamii na kusikika kwenye vyombo vyao vya habari hasa kwenye social networking vikisema kuwa Rais John Pombe Magufuli amesema chanjo za corona hazifai jambo ambalo sio kweli ila ni upotoshaji kwa ajili ya Malengo yao binafsi.

Jana Rais John Pombe Magufuli hakusema chanjo hazifai ila aliitoa Muongozo ni kwa namna ipi tunatakiwa kuzikubali chanjo kwa kuilekeza Wizara ya Afya kuhakikisha sio kila chanjo wanayoletewa wanaipokea tu bila kufanyia uchunguzi na akatolea mfano Baadhi ya chanjo ambazo zimeshatolewa na badala ya kuwa tiba ikawa tatizo.

Pia akatoa mfano mwingine wa chanjo ya kansa kwa kusema wao ndio Wanaongoza kwa kufa na Kansa kwanini hizo chanjo wasijidunge kwanza wao na badala yake wazilete kwetu.

Kwa sauti ya Marekani mnapotoa sauti zenu muwe mnajaribu kutoa na za wizi wa kura wa Trump sio kupotosha Rais Magufuli kasema Wizara ya Afya iwe makini kwenye kuzipokea chanjo isikubali kila chanjo inayoletewa kwani zingine sio nzuri.

Serikali kwani hamna uwezekano wa kuwawajibisha hawa watu wanaomuwekea Rais Maneno Mdomoni?

View attachment 1687900
Mkuu yasome kwa umakini sana haya maneno ya Mr MALCOLM X utakuja kunishukuru baadae.

3d88490cc674257c79eac669553d32e3--malcolm-x-quotes-black-panther.jpg
 
Mimi hua namuelewa sana JPMView attachment 1687910
Kwa maoni yangu, hata vitabu huwa vina"categorise not for use in....but in...." Kwa kusema hivyo huwa maudhui yake yamelenga uhalisi wa nchi hizo au bei zimepunguzwa au kuongezeka kwa kutegemea na package yake. Hata kuna baadhi ya products zimetengenezwa kwa kufuata hali ya hewa ya nchi.

Mfano, products zinazotumika katika nchi ambazo temperature inashuka hadi minus (-) Celsius ni tofauti na zile ambazo temperature yake ni always above 25 Celsius.
 
Tanzania inajiamini kwa kuwa kuna mchina nyuma yake

Kama tutachukua chanjo ni lazima tu itatoka China

Rais Mtanzania anajiamini kuongea anavyotaka kwa kuwa mchina yuko nyuma
 
Mimi hua namuelewa sana JPMView attachment 1687910
Duh uelewa nao ni tatizo. Hivi unajua madawa huwa ni gharama sana na kampuni zinatumia mamilioni ya pesa kwenye research, na return on investment mara nyingi inategemea nchi zenye buying power waweze kununua, kwahio huwa kuna dawa wanazitoa kama ruzuku kwa nchi masikini.

Pia nchi kama india huwa wanatoa dawa kama zile za wadau waliofanya research na kutumia mapesa (wao gharama yao huwa ni ndogo) hivyo kisheria dawa nyingi zinaweza zikawa zilezile zikapatikana india au hata mexico ila haziruhusiwi kuingia Canada au USA (kule kuna alternatives ya bei kubwa)

Kuna Documentary moja watu walikuwa wanatoka USA kwenda MEXICO wana-smuggle dawa ili wawaletee ndugu zao US, as they are cheaper there.

Kuhusu kufanyiwa research Africa (hii inatokea sana) as its cheaper kwa corporation kuwafanyia watu masikini hakuna implication kama wakifanya research huko kwao, implication ni kubwa sana (huko inabidi mtu asign akubali kufanyiwa research na kwa gharama kubwa) Africa ni swaga twende (sio kwamba ni ubaguzi bali it makes economic sense kwao)

Cha kufanya na sisi tuanze kufanya research na kutengeneza zetu, pia hatukatazwi kuzifanyia research zilizopo ila side effects mara nying it takes miaka (no body knows ni try and error) kwahio mwisho wa siku choice is yours either you definitely die now, au maybe in the many years down the line.
 
Habari wadau wa JamiForums,

Mara nyingi hivi vyomba vya habari vya kibeberu vinatumika vibaya japo vinafahamu kuwa vinatumiwa vibaya.

Jana Voice of American (VOA) kimeweka chapisho kwenye Mitandao yao ya kijamii na kusikika kwenye vyombo vyao vya habari hasa kwenye social networking vikisema kuwa Rais John Pombe Magufuli amesema chanjo za corona hazifai jambo ambalo sio kweli ila ni upotoshaji kwa ajili ya Malengo yao binafsi.

Jana Rais John Pombe Magufuli hakusema chanjo hazifai ila aliitoa Muongozo ni kwa namna ipi tunatakiwa kuzikubali chanjo kwa kuilekeza Wizara ya Afya kuhakikisha sio kila chanjo wanayoletewa wanaipokea tu bila kufanyia uchunguzi na akatolea mfano Baadhi ya chanjo ambazo zimeshatolewa na badala ya kuwa tiba ikawa tatizo.

Pia akatoa mfano mwingine wa chanjo ya kansa kwa kusema wao ndio Wanaongoza kwa kufa na Kansa kwanini hizo chanjo wasijidunge kwanza wao na badala yake wazilete kwetu.

Kwa sauti ya Marekani mnapotoa sauti zenu muwe mnajaribu kutoa na za wizi wa kura wa Trump sio kupotosha Rais Magufuli kasema Wizara ya Afya iwe makini kwenye kuzipokea chanjo isikubali kila chanjo inayoletewa kwani zingine sio nzuri.

Serikali kwani hamna uwezekano wa kuwawajibisha hawa watu wanaomuwekea Rais Maneno Mdomoni?

View attachment 1687900
Sio VOA tu,
Hata Millard Ayo pia alimnukuu vibaya,
Screenshot_20210128-102845.png
 
Mimi hua namuelewa sana JPMView attachment 1687910
Kuna watu wana viwiliwili ,vichwa wamewapa wazungu wanafikiria kwa maneno ya wazungu,wanacho ongea wanakichukua kama kilivyo huwezi kuwaambia kitu.

Plus na hizi siasa kila saa wao watu wa kupinga,kidogo "US kasema. UK kapanga, EU wameamua, UN wamekasirika".Hawa hata uwambie hawakuelewi basi unawaacha.

Kama hizi dawa za malaria vurugu tupu mara klokwini unaambiwa hii haifai,mnaletewa Orodar nayo unaambiwa hafai,mara Fansida nayo haifai mara eheeeeeee.....Mseto sijui kesho watakuja na dawa gani ya Malaria,yaani tabu tupu na sisi tena tunabugia tu........

Mpaka sasa kuna chanjo Kutoka Russia,US,UK,China na India,ila bado hatujui chanzo ipi inatibu type ipi ya Corona,manake kuna ile ya type ya kwanza kutoka China,kuna Corona kutoka UK,kuna corona kutoka South Africa na type nyingine kutoka Brazil,yaani full kubet mpaka kwenye afya zetu tunazi chezea kamari.

South Africa wa shaagiza chanjo kwa ajili ya watu wao lkn kutoka na sitofahamu na huu mkanganyiko,wataalam wao wanaona kuna probability ndogo hizo chanjo kufanikiwa.
 
Wewe mleta mada ni mpumbavu! Magufuli kasema wazi kwamba endapo hao wazungu wangekuwa wana uwezo wa kutengeneza chanjo tayari ingekuwa wameshatengeneza chanzo cha TB, UKIMWI, na Kansa! Nini maana ya hiyo kauli?!

Msikilize kuanzia dakika ya 1:30 amesema nini hapo!!

Sikufahamu wala sikuwahi kuwa Mwalimu wako ila naweza nikakuambia for sure kwa nini ulifeli shule...
 
Sikufahamu wala sikuwahi kuwa Mwalimu wako ila naweza nikakuambia for sure kwa nini ulifeli shule...
Na haiwezekani nikawa na wanafunzi vilaza aina yako manake ni kilaza tu ndie anaweza kupinga suala la Mheshimiwa Rais kusema "chanjo ya corona haifai"!
 
JPM lijanja sana
Usidanganyike na hiyo screenshot! Hiyo hapo sio chanjo bali ni dawa na ipo tangu June ay july mwaka jana. Sema kama unavyojua internet hoax, hivi sasa ndo wakaanza kusambaza na kusema eti chanjo wakati imeanza kutumika India tangu mwaka jana manake ndiko inatengenezwa
 
Back
Top Bottom