Wanabodi nawasalimu.Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari msemo unaopendwa kurudiwarudiwa na baadhi ya viongozi wa nchi hii wale wanaotokana na chama tawala ambao ni huu "CCM INA WENYEWE, NA WENYEWE NDIO SISI (WAO) NA TUNA WANACHAMA KIBAO" Mwisho wa kunukuu.Ukiuangalia huu msemo kuna tofauti kubwa sana kati ya wenye CCM na wanachama.Wenye CCM yao watoto wao hawasomi shule za kata,wanatembelea magari ya kifahari,Wake zao wakiugua kidogo wanapelekwa nje ya nchi kutibiwa na wala hawavai kapelo,tshirt wala kanga zilizoandikwa maisha bora kwa kila mtanzania.Hawa ni baadhi ya wenye CCM wengine utaongezea mwenyewe kimtizamo na wanamiliki CCM kwa kurithishana kama ifuatavyo:-
Moses Nauye Vs Nape Nauye
Kigoma MALIMA Vs Adam Malima
Yusuph Makamba Vs January Makamba
Cleopa David Msuya Vs Matayo David Matayo
S.Sita vs Magret Sita
R.Kawawa Vs VICK KAWAWA
A.H.MWINYI VS Husein Mwinyi.
Job Lusinde VS lusinde.
Kwa mtazamo wangu hawa ni baadhi tu wengine Jazia mwenyewe.