Hawa ndio watunga sheria!, madhulumati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndio watunga sheria!, madhulumati

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mfumwa, Feb 5, 2009.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kama kweli Wabunge wetu ndio tumewachagua, ama kuteuliwa na Rais kutunga Sheria, halafu wao ndio wavunja sheria tuna kazi. Wanapigania kuondoa ufisadi, kumbe nao wanadhulumu wafanyakazi wao. Soma habari chini.

  Zitto amkoromea Cheyo
  • Amtuhumu kunyanyasa madereva

  na Charles Mullinda, Dodoma

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), juzi aligeuka mbogo wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge na kumshambulia kwa maneno Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (DP), akimtuhumu kuwa ni mmoja wa wabunge wanaowanyanyasa madereva wao.

  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka ndani ya kikao hicho, zilieleza kuwa Zitto aligeuka mbogo baada ya kuibuka kwa mjadala wa madereva kudai mishahara na posho zao kutoka kwa wabunge.

  Zitto alichukizwa na taarifa kuwa Cheyo ni mmoja wa wabunge sita waliowafukuza kazi madereva wao waliokuwa wakidai stahili zao ambazo zinatolewa na Ofisi ya Bunge kupitia katika akaunti za wabunge, lakini wamekuwa wakilipwa kiasi kisichojulikana.

  Habari za ndani zaidi zilizolifikia gazeti hili, zilieleza kuwa Zitto alitofautiana pia na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokuwa wakipinga hoja ya kutaka wabunge wote wawalipe madereva wao malimbikizo ya mishahara na posho nyingine zinazotolewa moja kwa moja na Bunge.

  Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokubaliana na Zitto ni Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama na Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, wote CCM, walisisitiza kuwa wabunge wote wanapaswa kulipa malimbikizo wanayodaiwa na madereva wao ili kuepuka kuingia katika kashfa ya kudhulumu.

  Wajumbe wengine wawili, Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid (CUF), ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani, walibaki kimya bila kuunga mkono upande wowote.

  Habari zilidai kuwa Zitto alimshutumu Cheyo kwa kumfukuza dereva wake kwa kosa la kudai malimbikizo ya mishahara na posho zake, jambo ambalo halikumfurahisha Cheyo, ambaye aliamua kujibu mapigo kwa kumtaka Zitto kutoingilia mambo yasiyomhusu.

  Chanzo hicho kinaeleza kuwa baada ya Zitto kuona hoja yake ya kutaka wabunge walipe madeni wanayodaiwa na madereva ili kuepuka aibu ya aina yoyote inayoweza kuwapata inaelekea kugonga mwamba, aligeuka mbogo na kuwatishia wajumbe wenzake kuwa iwapo hawatakubaliana naye, basi atakwenda kuliweka wazi ili kila Mtanzania ajue madereva wanadhulumiwa haki zao na wabunge.

  Tishio hilo la Zitto liliwafanya wajumbe wote kunyamaza, jambo lililobainishwa kuwa ni dalili za wabunge kukubali kwa shingo upande kuanza kulipa malimbikizo hayo.

  Alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani jana asubuhi, Cheyo alihoji sehemu ambayo gazeti hili lilipata habari hizo, kwa kuwa mambo yaliyotokea ndani ya kikao hicho yalikuwa siri.

  Kwa ukali, Cheyo alisema hana ugomvi na Zitto, aliongeza kuwa kutofautiana kimsimamo au kauli ni jambo la kawaida ambalo linaweza kutokea kwa mtu yeyote.

  Hata hivyo alishindwa kukanusha au kukubali madai ya kulumbana na Zitto katika Kamati ya Uongozi ya Bunge na kumfukuza dereva wake kwa kudai malimbikizo ya mshahara na posho zake. Alisema kwa mkato Zitto ni rafiki yake na anaheshimiana naye kwa kiasi kikubwa, kisha akakata simu.

  Gazeti hili lilipowasiliana na Zitto katika viwanja vya Bunge jana asubuhi na kumhoji kuhusu kutokea kwa hali hiyo, alisema hawezi kuzungumzia mambo yaliyojadiliwa ndani ya Kamati ya Uongozi ya Bunge.

  Wabunge wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na madereva wao ambao wanadai kudhulumiwa mishahara na posho zao zinazopitia kwenye akaunti za wabunge.

  Ofisi ya Bunge ilikwishatoa maelezo kwa wabunge kuwalipa madereva wao mshahara wa sh 100,000 kwa mwezi na posho ya sh 30,000 kwa siku wanapokuwa vijijini, katika majimbo ya uchaguzi wa wabunge, ambapo kwa mwezi wanapaswa kulipwa sh 300,000.

  Habari zinaeleza kuwa maelezo ya Ofisi ya Bunge kwa wabunge, yanawataka kuanza kutoa mshahara na posho kwa kiwango hicho kwa madereva wao tangu Julai mwaka jana, hata hivyo, baadhi ya madereva wamekuwa wakiwatuhumu wabunge kwa kukaidi agizo hilo na kuwadhulumu stahili zao kama zilivyoanishwa na Ofisi ya Bunge.
   
 2. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Let's wait na see kama hii habari ina ukweli wowote ndani yake maana bado imekaa ki-trapezium
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi hawatoi ripoti ya matumizi ya fedha hizo mwisho wa mwaka? Halafu wengine wameajiri ndugu zao kama madereva lakini bado wanataka kuwadhulumu? Napendekeza yafuatayo:

  1.Wabunge wenaodaiwa malimbikizo wakatwe kwenye mishahara yao ili waliodhulumiwa walipwe.

  2.NSSF iangalie kama madereva hawa wanalipiwa stahili yao.

  3.Mwisho wa term ya bunge lazima hesabu zote ziwekwe sawa kabla mbunge hajalipwa mafao yake.

  4.Majina ya madereva wote waliojariwa na wabunge kwa mpango huu yapelekwe Ofisi ya Bunge.
   
 4. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280

  Fundi TZ yetu inasikitisha sana,

  Kuna watu wanaonyanyasika sana. Ingawa ukiangalia wao ndo wanaofanya kazi sana (wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala): mahouse girl, mahouse boy, madereva, wahudumu wa bar, wafanya kazi wa viwandani (casual labourers, the list goes on..). Inasikitisha sana, maana hawa sijui wanaonewa kwa sababu shule yao ni fupi..unaweza kukuta wanadai malimbikizo ya hadi miaka mitano...siku wakiinua kinywa kudai haki yao wanafukuzwa! Sasa sijui hawa waajiri wanafikiria hawa watumishi wanaishi vipi na familia zao. Its so sad. I have witnessed tens of such cases. Infact kuna moja hiyo..mama alifanya kazi kiwandani kwa mhindi...for twenty years, alikuwa analipwa around 25,000Tshs kwa mwezi..bwana....nilijaribu kumsaidia kadri ya uwezo wangu. Lakini cha ajabu mhindi alikuwa radhi ku-hire lawyer na kumlipa millions kwa kesi ambayo hata angetumia nusu ya legal fee basi mama wa watu angeridhika. Hii dunia ioneni hivyo hivyo..hakuna fairness kabisa!

  I would suggest, kwa kweli watu wenye uchungu kama wabunge (just wonder if they cant pay their drivers will they help housegirl?)..The government need to look at this issue critically. There are millions of silent voices ambao wanaonewa na kudhulumiwa haki zao na hawana wa kuwatetea. Mwishoni ndo unasikia mtu anakufa kwa kukataa tamaa...Jiulize barmaid unamlipa elfu kumi na tano! Inabidi apange chumba, awasaidie wazazi huko nyumbani..duh!WATU TUNAISHI KWA KUDRA ZA MWENYEZI MUNGU TUU! NO WONDER WE AFRICANS TUNAOKOKA SANA SIKU HIZI..MATATIZO YAMEKUWA MENGI MNO!

  Kama serikali ikiweka mkakati maalumu wa kuwasaidia hawa watu..basi naamini, hii sector itaheshimika na itawasaidia wengi ambao hawana elimu ndefu.

  But change should begin with us. Jamani wenye mahouse girl na madereva, try to pay these people decent living wage jamani..they also have families..kama wewe unavyoamka na kwenda kazini..hata yeye anatamani iwe hivyo. Infact I have seen some people..wanawapa house girls shilling 10,000Tshs! Kisa eti :"si anakula kwangu na kulala kwangu". Lakini unasahau kwamba mtu kama huyo katoka mkoani ana wanaomtegemea ambao na wao wanahitaji kusaidia na ndugu yao "anayefanya kazi mjini". nA HATA MABABA AMBAO MKO BUSY..TRY TO CROSS CHECK HOME , KAMA KWELI HAWA WAFANYAKAZI WA NDANI WANALIPWA...MAANA KUNA MAMA ZETU WAKOROFI, UNAACHA HELA HOME..HAWALIPI!

  Tushirikiane kupunguza (maana hatuwezi kuondoa) hizi dhuluma!

  Its a critical problem which needs our collective efforts.

  Masanja,
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Masanja. Mbaya zaidi ni kuwa hawa waheshimiwa wanalipwa hizo fedha mahsusi kwa ajili ya malipo ya madereva wao. Wao ni conduits tu. Au pengine ilikuwa ni njia ya kuwaongezea kipato. Kama ni hivyo, basi iwekwe wazi kama mshahara wa mheshimiwa na yeye ndiye aamue kama anahitaji dereva au la. Lakini as long haya malipo ni kwa ajili ya kuajiri dereva, wanawajibika kutoa ripoti ya matumizi yake.

  Nakubaliana na wewe kuwa jamii yetu inaona kuwa ni haki kuwadhulumu tunaowazidi. Pengine huu utakuwa mwanzo wa kuikomesha tabia hiyo ya kiovu.

  Amandla.......

  Fundi Utumbo
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Huo ni ulaji tu wa kupeana! Kuna sababu gani mshahara wa mtumishi kuupitisha kwa mwingine. Kama madereva wanatambuliwa kuwa ni watumishi wa bunge na wanastahili kulipwa na bunge kwa nini wasipewe pesa zao moja kwa moja??

  Nilipata kuongea na jamaa aliyekuwa dereva wa mbunge mstaafu, na huyo mbunge alikuwa ni mwenyekiti wa bodi ya shirika la umma. Huyo dereva anasema ilikuwa taabu kupata hata 10% ya pesa ambaye huyo mbunge alikuwa analipwa na shirika kwa ajili yake. Haya mambo yapo siku nyingi na waheshimiwa walio wengi wametumia hiyo nafasi kuwaibia. Hata hivyo tunatakiwa kulaumu watunga sera na sheria kwa kutoweka kila kitu kinachohusiana ajira wazi. Watumishi wote (wakiwemo barmaid, housegirls n.k) walitakiwa kuajiriwa kwa utaratibu unaoeleweka ili wapewe mshahara unaotambulika kisheria na kwa hiyo hata walipe kodi, na mengineyo kama NSSF.
   
 7. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  vipi kuhusu madereva wengine wa taasisi za serikali?
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ni vema kama serikali itarudisha utaratibu wa zamani wa wabunge kutumia magari yserikali, hivyo kuendeshwa na madereva wa serikali. Hizi vurugu zilianza baada ya Mwinyi na genge lake kuanza kugawana mali ya uma wakijigawia magari kwa bei ya basikeli. Wabunge walivyoona hayo na wao wakaamua kutobaki nyuma. Utaratibu huu umekomba resources lukuki za taifa pasipo ulazima wowote.
  Nakumbuka mzee Mwasakafyuka alivyonyanyaswa kisa kuzuia gari lililotakiwa na Amina Salum Ali.
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Kwanini mshahara wa dereve upitie kwa mbunge? Si kila siku naskia maofisini wakisema 'mshahara wa mtu ni siri'? Kwanini ofisi ya bunge isiwaajiri hawa madereva na kuwalipa badala ya kuwapa mwanya wabunge kuwanyonya? Kuna uwezekanao mkubwa hata huo mshahara ni wabunge wenyewe ndo wanaamua walipe kiasi gani. Hivi tutaacha lini kufanya mambo 'kienyeji?'
   
 10. K

  Koba JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....haya ni mambo ya aibu kabisa eti wabunge hawawezi kuendesha magari yao na wanatumia pesa za walipa kodi kulipa madereva wao,huu kama sio ufisadi ni nini? huu ni upumbavu kabisa na wizi wa mchana kwa walipa kodi,hapa lazima raisi aingillie kukata matumizi ya kikoloni kama haya au wewe Zitto mwenyewe lazima uweke bill hapo bungeni ya kuzuia huu wizi wa mchana...cant believe huu upuuzi unafanyika 2009,hawa lazima waendeshe magari yao wenyewe huu upuuzi lazima uishe!
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkulu hili suala si kwa wabunge tu! Hata kwenye ofisi za serikali na mashirika, ofisa anayestahili kupewa gari haruhusiwi kuindesha mwenyewe. Wanadai ni kulinda ajira lakini ni mwanya mkubwa wa wizi. Mfano ofisa huyo akitoka Dar akaenda Moro (km 192), analipwa night kuanzia shs 65000/- kwa siku na dreva analipwa shs 45000 kwa siku moja. Wakikaa wiki 2 kwenye mkutano kila mmoja anapata karibia au zaidi ya mshahara wake wa mwezi mzima! Na kama ofisi moja ina mabosi zaidi ya 2 wa namna hiyo, wote wanaweza kwenda na madreva wao! Hiyo nayo ni aina nyingine ya Bongo Dar!!!
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Yaelekea Waheshimiwa hawa wana tabia ya kudhulumu madereva wao.
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Naona Zitto anakuja na mtindo wa kutetea wanyonge mpaka katika kilabu chao cha bunge, wengine wanaweza kusema "he has got bigger fish to fry" na angeweza kutumia muda na mtaji wa kisiasa vizuri zaidi kama angetafuta sauti ya pamoja, hususan na viongozi wenzake wa upinzani.

  Wengine wanaweza kusema ni kibaraka wa CCM ametumwa kuwamaliza kisaikolojia wabunge wenzake wa upinzani katika mambo ambayo yanaweza kuwa kweli lakini yametumika kisiasa zaidi.

  Wengine wanaweza kusema kama anasema kweli ni vizuri, na kwamba wabunge hawawezi kuisafisha serikali dhidi ya ufisadi kama wao wenyewe ni wanafiki.

  Kana,

  Kuna mambo mengine wanasema wenzetu ni "a recipe for disaster". Inabidi tujiulize madereva ni waajiriwa wa nani? Nani analipa mishahara yao? Hawa ni waajiriwa wa mbunge au wa ofisi ya bunge?

  Kama ni waajiriwa wa mbunge, na mbunge hapati hela za kuwalipa kutoka ofisi ya bunge then mbunge ana haki ya kupanga mishahara na marupurupu vyovyote atakavyo, almuradi anafuata sheria.

  Kama ni waajiriwa wa ofisi ya Bunge basi kwa nini mbunge anahusika sana katika mshahara? Ningetegemea the most ambacho mbunge angehusika labda ni kuhakiki muda wa dereva kufanya kazi.
   
 14. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kama utata unajitokeza nadhani mishahara,posho na malipo mengineyo si lazima yapitie kwa mbunge mwenyewe. Ofisi ya Bunge ikiamua yaweza kupanga utaratibu mzuri tuu unaokubalika. tuepushe migogoro isiyo lazima.
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Yale yale yaliyowapata waliokuwa wafanyakazi wa EAC. Crown Agents ya Uingereza waliitumia serikali ya Tanzania kama conduits tu kwa ajili ya kuwafikishia malipo wastaafu wake lakini serikali ikabana. Kumbe ndio maana wabunge wetu wako kimya wakati wote hawa wazee wanadai haki zao mpaka kufikia kulala barabarani. Kansa ya dhuluma imeota mizizi tangu serikalini hadi bungeni na inaenea, aibu tupu.
  Wow !!!!
   
Loading...