Hawa ndio wanaomshauri Rais Magufuli

CONSTRUCTIVE THOUGHT

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,158
417
Habari Watanzania wenzangu!

Nivyema tukafahamu kikatiba watu wanaomshauri Rais katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

KATIBA YA TANZANIA YA 1977.

Ibara ya 37.
Ibara ndogo (1)
Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.

Ibara ya 54
ibara ndogo (3)
Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya
Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha
kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji
wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na
litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote
litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo
maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.

Ibara ndogo (5)
Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa
na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.
 
Naam! Ndio maana anafanya ajisikiavyo na sivyo katiba isemavyo. Ona hili la kusitisha ajira, promotion, mishahara na kulipa madeni ya wafanyakazi wa umma lilivyokaa kisha juzi kaajiri wakuu wa wilaya na madas. Wakati mwingine waweza kudhani kuna wakulu wawili tofauti ila wanaongoza nchi moja. Au washauri wake wana double personalities and faces? Kuna shida mahali. Huyo katibu wake awe ananote kwenye journal matamshi ya mkulu na kumkumbusha basi ili kusiwe na mpishano huu ninaouona.
 
Ebhana huyu mtu kama aliweza kutandaza lami kwa staili ya kibabe...sa hvi inabidi awe mbabe zaidi tena saana...kama kawaida washauri wake ni mainjinia na masodier....naamini maendeleo yatakuja japo waliozoea hela za kuokota okota itawawia vigumu sana....piga kazi ngoshaa
 
Back
Top Bottom