Hawa ndio wanaoiua Radio One na brand yenu

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Hakuna ubishi Radio one iliweza kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari nchini Tanzania, miaka ya nyuma mtu ukisikia hii Radio unapata kitu hasa.

Kituo kilifanya usajili wa maana sana kwa kuibomoa RTD(TBC CCM) na kukonga mioyo ya wasikilizaji wa Radio. Lakini kinachoikumba hii Radio hivi sasa na mapito inayopitia nadhani muda ni rafiki. Kusikiliza Radio one hivi sasa sijui unatafuta nini. Juzi siku ya alhamis nikasema acha nisikilize hii radio hasa kutokana na mimi kuwa mdau wa muziki wa Dansi!

Kukawa na mada sijui Malumbano ya hoja wakiwa wamealika waongeaji akina Julio na wengine mara baada ya kipindi kumalizika nikasema ndio muda umewadia wa kusikiliza muziki wa dansi kipindi Afro Tz mwendokasi sijui wa nini huko. Nilichokisikia nikajisemea hivi hii Radio hivi sasa inaendeshwa kishikaji hivi, hakuna usimamizi wa utaratibu wa kutangaza kipindi Afro Tz kikarindima na akina Julio tena na sijui Maufi kilichoongelewa ni ujinga mtupu. Joyce na Deo inakuwaje saa 3 mnampa mtu ambaye hana elimu ya utangazaji analeta ushikaji kwenye Radio.

Julio anajisifu kabisa kuwa yeye ni CCM! Kwenye kipindi cha muziki wa dansi? Kweli Radio One mmeamua kuizika wenyewe. Kipindi kimejaa kutajana majina ya watu kipindi hakina utayarishaji wa kiaundishi, ni bora saa 3 mnazopoteza kutajana majina ni bora mfikirie biashara ya kufanya. Endeleeni na uzembe wenu mnapokimbilia ni kuwa TBC Taifa namba 2.
 
Joy Mhavile alipaswa kuwa ameachia siti mapema. Zama zake zimefubaa, ngoja vituo vifubai ndio akili itakaa sawa.
 
Redio one ilibamba sana kipindi kile 90's na mwanzoni mwa 2000's! Sasa hivi imeshajifia.....
 
Hapa hoja ni Julio. Huyu jamaa kachokwa kila mahali. Watu hawataki hata kumsikia.
Angekaa mbali na media hata kwa miaka 2 tu watu wamkumbuke.
 
Back
Top Bottom