Hawa ndio viongozi bora! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndio viongozi bora!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Mar 7, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Viongozi wengi wa bara la Afrika ni wahuni na waroho wa madaraka ambao wanatumia kila aina ya udhalimu ili wabaki madarakani kwa gharama ya umasikini wa wananchi.Hamna shaka kuwa watu wengi barani Afrika ni masikini sana,huku watawala wakiishi maisha ya anasa na kugeuza ofisi au Ikulu zao kuwa mapango ya wanyangÂ’anyi au madalali wan chi za Magharibi na Marekani.
  Kutokana na hali tuliyonayo,kazi kubwa inayotukabili ni jinsi ya kuwapata viongozi bora kuliko kuwaondoa viongozi wabaya.Je,tutawapataje viongozi bora.Kabla sijajibu swali hili,niseme tu kwamba mara nyingi wanasiasa sio viongozi wazuri kwani wengi wao wanakosa personality,moja ya sifa muhimu sana ya kuwa kiongozi bora.
  Kwa muda mrefu kuna mjadala kwenye mashule au vyuo na hata mitaani kama viongozi bora huzaliwa ama la.Wachambuzi wengi wa mambo ya kisiasa wanasema suala la uongozi haliwezi kuwa la kuzaliwa pekee.Kiongozi lazima awe na maarifa,ujuzi na uzoefu katika Nyanja mbalimbali za maisha.
  Kiongozi au kulongola ni kuonyesha njia na kuijua njia vyema.Uongozi ni kuwafanya watu wengine wakufuate katika kutimiza malengo ya kikundi,jamii au nchi.Kiongozi ni Yule ambaye ana kitu cha kuwafanyia watu wengine katika harakati za kuboresha maisha yao.
  Ubunifu na mwono wa mbali ni moja kati ya nguzo kuu ya uongozi.Nia ya kuongoza pekee haitoshi kumfanya mtu kuwa kiongozi bora.Kiongozi lazima awe na maarifa,ujuzi na uzoefu wa kutosha katika mambo yahusuyo nchi au watu.Maarifa na uzoefu lazima viendane na uzalendo kabambe.
  Haitoshi tu kuwa na maarifa na ujuzi.Kuwa na maarifa na uzoefu ni suala moja,na kutumia maarifa hayo kwa manufaa ya umma ni suala la pili.Maarifa yanakuwa na maana pale yanaposaidia umma au watu.
  Moja kati ya sifa za ndani za kiongozi bora ni kama vile,to be fair (not favour or fear),tabia njema,mpenda amani,mtulivu,mwaminifu,mwenye busara,anayependa kusaidia watu,si mbaguzi,mchapakazi,anayeweza kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati,mtu wa wote,asiyemilikiwa na kikundi chochote,awe na uwezo wa kuwasiliana na watu anaowaongoza,awe tayari kusikiliza pande zote za hadithi kabla hajatoa maamuzi,mkweli na muwazi,asiyehukumu bila ushahidi,awe tayari kukosolewa,awe mcha Mungu n.k
  Kiongozi bora hupenda kuwafunza wengine na kuwaanda viongozi wa baadae.Viongozi bora mara nyingi hawapendi kujitokeza hadharani,wengi wao wanaona uongozi ni mzigo.Viongozi bora hawaandai watoto wao au wana familia kushika madaraka.
  Viongozi wengi wa Afrika wanatumia vibaya nafasi zao za madaraka kwa kujinufaisha.Mifano ya viongozi wabaya imetapakaa kila kona ya Afrika.Kutoka Capetown hadi Cairo,kutoka Dar es Salaam hadi Dakar,kutoka Abuja hadi Algiers,kutoka Lome hadi Luanda,Kutoka Kampala hadi Kinshasa n.k.
  Unafikiri kiongozi bora ni yupi,na tutampataje?Naomba mchango wenu wadau,naomba kuwasilisha.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hakuna kiongozi bora katika jopo la wenye madaraka kwa sasa. Labda tuangalie wale ambao wana chipukia au wale ambao wapo njye ya uongozi.
   
 3. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kama viongozi bora hawapo madarakani kwa sasa,unafikiri tatizo ni nini hasa?Tatizo lipo kwetu wachaguaji au jamii kwa sasa haina viongozi wazuri?Na kama wapo tutawapataje?Je,mifumo yetu ya uongozi ipo salama?
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo wananchi. Tatizo ni mifumo kandamizi iliyowekwa na watawala ya kuchagua viongozi.viongozi walioko madarakani wanatumia njia mbalimbali haramu za kuendelea kuongoza bila kujali matakwa ya wananchi. Mfano mzuri ni hapa kwetu Tanzania. Majimbo ambayo CDM ilishinda ni yale ambayo wapiga kura walijitolea kukesha wengine hata kwa siku mbili ili kuzuia wizi wa kura.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pamoja na mifumo kandamizi, waarabu wametuonyesha kwamba tatizo ni wananchi wenyewe kuukubali au kuukataa. Wananchi wakiamua itakuwa ni habari ingine hata ikiwa dubbed uchochezi wa vurugu cun uvunjifu wa amani kama wasemavyo tendwa na Chiligati & Coy!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba wanaoweza kuwa viongozi bora hawa gombei kwani wanajua Watanzania wana penda zaidi wasanii. Kwa hiyo mtu ana jiamulia akae pembeni tu unless awe na moyo wa kuvumilia. Can you imagine wewe ugombee nafasi zidi ya boya fulani halafu akushinde? Uta jisikiaje?
   
 7. W

  Wangu Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio maana Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kutokwa na machozi siku azimio la Arusha lilipovunjwa kule Zanzibar hasa ilke misingi yake, kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. BADO HATUJAPATA VIONGOZI BORA. waliopo ni BORA VIONGOZI!
   
 8. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Michango yenu wadau ni mizuri,na kwa kiasi kikubwa wote mnakubaliana nami kwamba kwa sasa taifa letu linakabiliwa na ombwe la uongozi.Hivyo ni jukumu la kimsingi kwa sisi wananchi kujua hatima za maisha yetu.Hii ni nafasi ya pekee kushiriki kuhakikisha tunakuwa na viongozi wanaosimamia masirahi ya umma.Wakati mwingine uchaguzi wa mara kwa mara na unaoweka ukomo wa madaraka hauwezi kutusaidia sana kama hatutaweka mifumo dhabiti ya kuwafanya viongozi wawajibike kwa umma.Chaguzi nyingi zinazofanyika Afrika ni chaguzi bila chaguo,vyama ndivyo ni sauti ya kutuamulia tuongozwe na nani.Sasa ni wakati wa kukataa kuongozwa na watu wasiotumikia umma.Ni kazi yangu,ni kazi yako kuhakikisha viongozi wanakuwa accountable kwa umma.
   
 9. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mengi yamesha ongelewa, cha zaidi kiongozi mzuri awe mzalendo wa kweli, asiyeweza kununuliwa na mafisadi, awe na uthubutu, mbunifu, msikivu wawatu na mpenda maendeleo.
   
 10. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kihistoria kuna wale viongozi wa kijadi na kimila, ambao wengi wao walikuwa wakipatikana kwa kupendekezwa na wazee au wananchi wenyewe moja kwa moja bila kupitia chama chochote....! Wengine walikuwa wanaandaliwa kwa muda mrefu unaotosha kumsoma vizuri mwenendo wake na matarajio yake dhidi ya matarajio ya wale anaotegemewa kuwaongoza....! Changamoto kubwa ni kwamba, kiongozi bora hutawaliwa na fikra zifuatazo:

  1. Huwa ni mtu asiyetaka kufeli, na hivyo mara nyingi hutawaliwa na hofu ya kushindwa kuongoza....! hii hutokea kwa kuwa hana kundi lolote linalomuahidi kumlinda hata akiteleza....!
  2. Huelewa fika kuwa awapo madarakani, rafiki yake ni mnyonge, asiye na sauti, na masikini. Na maadui wake ni wale wenye nguvu, sauti, na matajiri.... hujua kuwa anaenda vitani kupambana na wenye nguvu, sauti na matajiri kwa manufaa ya wanyonge, masikini, na wasio na sauti....!
  3. Hujitambua kuwa ni binadamu mwenye kukosea, ilhali hayupo tayari kupata hati au historia chafu maishani mwake.... hivyo anaelewa kuwa ni kazi ngumu kujihakikishia hili akiwa kiongozi....!
  Kutokana na hayo, basi huwa hapendi kujitokeza kuongoza, lakini akifuatwa na watu na kumuomba awaongoze anakuwa tayari, japo huzungukwa na hofu kwa kuwa hana kundi lolote mwenye ajenda ya siri nayo na hivyo haelewi vema kwa nini watu wamemfuata yeye.... Hii ni kwa sababu mara zote yeye hujifananisha na watu wengine wote na hivyo yeye haoni unique characters ambazo zingemfanya yeye apendekezwe badala ya fulani ndani ya ile jamii....!

  Lakini kutokana na busara, hekima na kauli zao, siku zote wanakuwa wakisikika ndani ya jamii hata kama wapo nje ya utawala wa jamii husika...! Ni kwa sababu hii, mara nyingi huweza hata kutumika na viongozi wabovu kwa kujenga urafiki nao, na kupretent kama wao ilimradi tu wafanikishe kupata uongozi wanaotaka kwa maslahi yao....!

  Hivyo basi, kama walivyosema wahenga kuwa; "kibaya chajitembeza, kizuri chajiuza", hata hivyo viongozi wabovu hutembea huku na huko kujitangaza na kujinadi, hata kwa kutoa vishawishi kama vile usafiri, zawadi mbalimbali, vitumbuizo, attractive sitting arrangements, etc. Huku wale bora wakishtukia tu sisimko kubwa likitokea kwa jamii kuonesha kukubalika kwao. Mikusanyiko yao huwa havina gharama zisizo za lazima kama vile maigizo, matangazo ya ziada kuhusu kuja kwao, ulinzi wa kupindukia, nk.

  Hivyo, katika kizazi chetu sio kweli kwamba viongozi bora hawapo, bali viongozi hawa ni watu wasiopenda kujitokeza na hivyo kuwa vigumu kupatikana, ilhali wamejaa tele....! Wamefunikwa na kunyimwa nafasi na mifumo inayotumika sasa ya kutangaza nia mwenyewe au kutangaziwa na kikundi fulani cha watu....! badala ya kutangaziwa na jamii yenyewe....!

  Haya ni maoni tu....!
   
 11. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  good analysis,thanks
   
Loading...