Hawa ndio binadamu bana!

Jplus Jr

Senior Member
Dec 29, 2018
124
147
Ukiwa na pesa binadamu watakuheshimu, watakusiliza, watakunyenyekea, watakupenda si kwa sababu ni upendo wa moyoni ila ni kwasababu una pesa.

Lakini pia ni binadamu hao kama huna pesa yote niliyotaja hapo juu na mengine mengi kamwe huwezi yapata toka kwa binadamu ni nadra sana.

Ni binadamu hao hao ambao ukiwa na pesa na ukaja kuishiwa wanabadilika pia na hawakuthamin wala kukujal tena. Ni ni hao hao binadamu ambao hawaweza tena kukusaidia kwakuwa tu ulishafulia.

Ni binadamu hao hao ukiwa na shida tu kama ugonjwa au uhitaji wa kitu fulani ukiomba kusaidiwa hakuna anaejali hata kidogo, na ni binadamu hao hao ambao yakikukuta majanga sasa baada ya uhitaji uliokuwa nao, mfano ukafiwa au kufariki ww mwenyewe utaona wanasikitika sana na kutoa michango ya kujionesha. Ilihali wakati uko hai na una uhitaji hakuna hata aliyekusikiliza wala kukusaidia.

Nini unachojifunza wewe toka kwa binadamu kwa hizo tabia?
 
Ben R Mtobwa alituusia Pesa zako zinanuka
Marijani Rajabu alisema Dunia sasa imani imekwisha. Si Wanawake, si wanaume, si kwa wazee Wala si vijana. Kwenye watu kumi binadamu mmoja.
 
Ndiyo maana wazungu wana taratibu na sheria ya kusaidia a na serikali, unachopewawni haki yako. Hata ndugu na marafiki wasiookuthamini utaishi.
 
Kabisa yaan
Ben R Mtobwa alituusia Pesa zako zinanuka
Marijani Rajabu alisema Dunia sasa imani imekwisha. Si Wanawake, si wanaume, si kwa wazee Wala si vijana. Kwenye watu kumi binadamu mmoja.
 
Back
Top Bottom