Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,445
Kuna mambo yananitatiza kidogo, ni kwamba kuna mawaziri ambao wizara zao zimo ndani ya muungano kama ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje n.k na kuna wizara ambazo mambo yake si ya ki muungano kama elimu, michezo n.k. kwakuwa zile wizara za muungano zinaitwa wizara katika serikali ya JMT.
Je hizi ambazo zinashughulikia masuala ya bara tu zenyewe zimo ndani ya serikali ipi? Hii ni kwa sababu kule Zenji kuna wizara ambazo zinahusika tu huko na si bara nazo ni wizara katika SMZ.
Na je baraza la mawaziri linaundwa na mawaziri wa serikali ngapi?
Katiba inasemaje kwenye hili?
Na je katiba hii chakavu inaruhusu Rais wa Zanzibar kuteua mbunge toka bara kuwa waziri kule visiwani?
Hata ile walio fanyia marekebisho kwa kuita serikali ya umoja wa kitaifa SUK je inaruhusu?