Hawa mawaziri ni wa serikali ipi?

Kuna mambo yananitatiza kidogo, ni kwamba kuna mawaziri ambao wizara zao zimo ndani ya muungano kama ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje n.k na kuna wizara ambazo mambo yake si ya ki muungano kama elimu, michezo n.k. kwakuwa zile wizara za muungano zinaitwa wizara katika serikali ya JMT.

Je hizi ambazo zinashughulikia masuala ya bara tu zenyewe zimo ndani ya serikali ipi? Hii ni kwa sababu kule Zenji kuna wizara ambazo zinahusika tu huko na si bara nazo ni wizara katika SMZ.

Na je baraza la mawaziri linaundwa na mawaziri wa serikali ngapi?

Katiba inasemaje kwenye hili?

Na je katiba hii chakavu inaruhusu Rais wa Zanzibar kuteua mbunge toka bara kuwa waziri kule visiwani?
Hata ile walio fanyia marekebisho kwa kuita serikali ya umoja wa kitaifa SUK je inaruhusu?
 
Hivi humu ndani hamna wana sheria pamoja na wataalamu wa katiba?
 
Hapa sasa kichwa kitaanza kuuma tena ila maadamu mambo yanaenda bila kujali yanaendaje poa tu
 
"mkataa asili ni mtumwa", unamaanisha hili mkuu!? Maana ni kweli tunavyoonekana kwa sasa tumekuwa watumwa katika nchi yetu na hii ni kuanzia yule aliye juukabisa hadi bibi yangu aliye kijijini(japo huyu ana nafuu)
Yani ni aibu watu kuikana asili yao! sijui wanaona aibu gani kusema miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika! shee!
 
Hiki chama kinacho ongoza nchi kinatuchanganya sana, wako tayari hata kuweka wizara ya mke wa rais ilimuradi tu wa meet their interest.
 
unaweza (in red) kuwa unawakilisha Watanzania wengine zaidi ya milioni 40+ ambao kila ukiwauliza kitu hata yale mambo ya msingi kama hili tunadai hatujui.
Uliona hata JK hajui ni nani mmiliki wa DOWANS na si ajabu hata hili pia naye halijui.
Ndio maana tumeamua kutumia mabiliioni ya shillingi kusherehekea uhuru wa nchi tusiyoijua (tusiyotaka kuitaja!!!) ambayo inaonyesha kuwa tunaweza (Watanzania) kuwa miongoni mwa maajabu mapya ya dunia!

Na ukiwabana wanasema serikali ya Tanzania Bara..(non sense)
 
Kuna mambo yananitatiza kidogo, ni kwamba kuna mawaziri ambao wizara zao zimo ndani ya muungano kama ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje n.k na kuna wizara ambazo mambo yake si ya ki muungano kama elimu, michezo n.k. kwakuwa zile wizara za muungano zinaitwa wizara katika serikali ya JMT.

Je hizi ambazo zinashughulikia masuala ya bara tu zenyewe zimo ndani ya serikali ipi? Hii ni kwa sababu kule Zenji kuna wizara ambazo zinahusika tu huko na si bara nazo ni wizara katika SMZ.

Na je baraza la mawaziri linaundwa na mawaziri wa serikali ngapi?

Katiba inasemaje kwenye hili?

Verygood for constructive and logical idea, Ndugu hii nchi yamejaa madudu matupu hata mfumo wa serikali yetu haueleweki kabisa sasa unadhani patakuwa na maendeleo hapo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom