Hawa Mashoga na Wasagaji!!


Ni kitu chema sana kama tutaweza kujifunza KUKUBALI KUTOKUKUBALIANA, ushoga si jambo jema kwa namna yyt ile lakini kwa kuwa nao pia ni binadam na wanamahitaji ya msingi kama binadamu wengine ni lazima tujifunze namna ya kuwapokea kwenye jamii zetu, kuwasikiliza na pia kuwapa nafasi ya kuendelea bila kujali hulka zao.

Inasemekana wapo wanaozaliwa na hulka hizo na huonyesha dalili hizo toka wadogo, wapo ambao huathiriwa na mazingira (kuingiliwa wakiwa wadogo mpaka wanazoea) hawa hawakupata ulinzi wa kutosha wakati wa utoto wao. Hivyo unapomtenga mtu wa aina hii ni nani kati yenu asiefaa kwenye jamii? Kwa nn tunawahukumu bila kujua kilichosababisha wao kuwa hivyo?

Hii jamii inahitaji support, naunga mkono wote wanaowasidia na wanaohakikisha wanapata haki yao ya kuishi kama watu wengine.
 
Hizo ni jamii zilizopotoka. Nikuulize swali: Wewe ukisikia mwanao wa kiume anaingiliwa kingono na wanaume utaona ni sawa tu?

Sitafurahia lakini kamwe siwezi kumkana. Atabakia kuwa mwanangu wa kiume milele daima. Yeye kuwa shoga hakumfanyi awe ni mtu mbaya.

Kama wewe ni shoga utatamani mwanao pia awe shoga?

Mimi siyo shoga hivyo siwezi kujibu swali lako kikamilifu. Ila naamini katika uhuru binafsi na naamini katika watu kufanya yale yawapayo furaha ili mradi tu hawaingilii ya wengine.

Huoni kama role ya uke na ume kwenye ngono ni marufuku tangu uumbaji kuchanganywa?

Hapo sijakuelewa kabisa unachosema.

Sisema kuwatendea mashoga ukatili ni sawa, lakini ni haki ya jamii kuwatenga kwa kua tabia yao haikubaliki na jamii.

Kuwatenga (kuwabagua) ndiyo ukatili wenyewe huo sasa. Kama hupendi ubaguzi wa aina yoyote ile basi hata ubaguzi dhidi ya mashoga kwa sababu ya mwelekeo wao wa kijinsia hautaupenda.

Yapo mambo hayakubaliki na desturi mila na dini zote. Ushoga ni mojawapo. Ushoga ni jambo la aibu na usitarajie jamii popote kukubali kama tabia ya kawaida.

Ushoga haukubaliki kivipi wakati hao watu wa dini nao wanahusika kwenye hayo mambo? Huu unafiki wa dini umepita kiasi sasa. Hao wadini ndiyo wako mstari wa mbele kabisa katika hayo matendo lakini kwa kujifanya wanapinga tu hawajambo. Wanafiki wa kutupwa hao.
 
Hata siku moja hakuna mtu atakayeweza kuzuia jambo hili,hata siku moja huwezi pingana na hisia za mtu,mashoga wanaojionyesha sio wengi ukilinganisha wale wasio jionyesha(closet gays),haya mambo watu wanafanya majumbani mwao tena kwa siri kubwa,utaweza zuia hili??,hiyo ni kazi bure,mungu ndiye atakaye hukumu siku ya mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…