Mkuu tena nikushauri hakikisha unaandika matumizi yote unayowapa hao kuku kuanzia chakula, dawa na huduma nyingine kisha linganisha na bei ya kuuzia uone. Hapo ndio utajua kwanini watu wako radhi hata kutukanwa kwenye ajira kuliko kwenda kujiajiri kwenye miradi hiyo ya ujasiriamali. Unaweza kukuta gharama ya kuku kuanzia manunuzi, chakula na tiba zao labda kuku 100 mpaka uwauze ndani ya mwaka ni kama 1,500,000 lakini hela utakayopata ni 1,600,000!! Yaani wakati mwingine hata kula kuku huwezi huwezi.