Hawa jamaa wanamaanisha nini? kitendawili kigumu.

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,529
196
Je ni udini ulioletwa na serikali ya JK au ndio kusema paka huyu ni mwizi wa kitoweo kiasi kwamba imebidi asulubiwe msalabani?? Sina jibu ila maswali kibao.

252024_203738689671314_100001055534219_581236_7406852_n.jpg
 
aaagh nini tena hii? Ndo nlikuwa najiandaa kulala bana. Ushavuruga kila kitu chalii'angu
 
Hata kama huyo paka ni mwizi kiasi gani, haikuwa busara kumsulubisha namna hiyo, huu ni ukatili kwa wanyama uliokithiri.,lakini pia kwa kutumia msalaba inaweza kuamsha hisia hasi za kidini na kupelekea machafuko kwenye jamii.,upuuzi huu lazima ukemewe kwa nguvu zote.
 
Na Doctor Manyaunyau nae akemewe kuwaua hawa viumbe na kuwanyonya damu. (sidhani kama bado anaendelea)
 
Huyu paka. Ni vitu vya kawaida vijijini. Nakumbuka tulikuwa tunamtega ngedere kisha tunachapa anaomba msamaha hadi anakata roho! had leo inaniuma sana!
 
Duh kama kweli ni paka halisi, kuna haja ya kuwa na Wanaharakati wa Haki za Wanyama pia katika nchi hii. Kwenye Katiba Mpya tuweke kipengere hicho!
 
Lazima ikemewe kwa nguvu zote, sisi tunasema na kuamini msalaba ni njia ya uzima, tunauabudu na kuupigia magoti. Kwa nini wengine waudhalilishee?? alaaniwe kwa jina lipitalo majina yote JESUS!! JESUS!!
 
ni bongo kweli? Mbona imekaa kama Somalia? ni wapuuuzi kweli hawa!
 
Je ni udini ulioletwa na serikali ya JK au ndio kusema paka huyu ni mwizi wa kitoweo kiasi kwamba imebidi asulubiwe msalabani?? Sina jibu ila maswali kibao.

252024_203738689671314_100001055534219_581236_7406852_n.jpg

Ni Bora umetumika msalaba na ndiyo maana wahusika wapo kimyaaaa.......... ingekuwa upande ule mwingine .......THIJUI.........
 
Back
Top Bottom