Hautapewa leseni ya biashara kama Hauna Hizi Taarifa

Hautapewa leseni ya biashara kama Hauna Hizi Taarifa

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
137
Reaction score
219
Ili uweze kufanya biashara kihalali Tanzania ni muhimu sana uwe na leseni ya biashara.

Sasa Kuna taarifa Tano lazima uwe nazo ili upewe leseni ya biashara;

1. Aina ya Biashara,
Ni lazima uweke wazi ni biashara gani unataka kufanya mf; Vifaa vya simu

2. Wilaya/halmashauri
Ni lazima useme ni wilaya gani biashara yako itakuwepo.
Mfano; nyamagana, ubungo etc

3. Block/plot number
Ni lazima uweke wazi biashara yako ipo block namba ngapi na plot namba ngapi.

4. Title deed/lease agreement
Kama umepangisha frame ni lazima uweke mkataba wa upangishaji, au kama unafanyia nyumbani kwako basi utaweka title deed.

5. TIN

Bonus Tip ni lazima uweke hizi personal information ili kuanza mchakato

-Namba ya NIDA
-Namba ya simu

Hey, naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili biashara na Kampuni.

Kama unahitaji consultation zaidi kuhusu upatikanaji wa leseni unaweza kunitumia ujumbe WhatsApp kupitia namba hizi

0678131068

Your Favorite Lawyer.
 
Watu wanataka kusikia diamond kaachwa wewe unaleta issue za maana hapa. Comments zitakuwa chache sana.
 
Back
Top Bottom