Uwesutanzania
JF-Expert Member
- Feb 9, 2019
- 1,602
- 1,864
Leo nitakuja na somo lenye kichwa kikisema kuwa
HAUKUUMBWA NA MUNGU
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️
Ndugu yangu msomaji naomba tumia akili kidogo unaposoma bandiko hili maana litaingia ndani zaidi katika maisha yetu ya kila siku.
Naam ndugu yangu msomaji leo nataka utambue kuwa haukuumbwa na Mungu,
Katika vitabu vya dini izi kubwa tatu tusomavyo viwili vinasema kuwa binadamu aliumbwa siku ya sita na siku ya saba Mungu akapumzika, katika imani ya tatu inasema binadamu mweusi aliumbwa siku ya tano pamoja na wanyama ili awe msaidizi wa binadamu aliyeumbwa siku ya sita.
Basi bwana Mungu baada ya uumbaji akautukuza ulimwengu na kumuweka humo binadamu.
HIVYO BASI HABARI ZA MUNGU NA UUMBAJI ILITAMATIKA SIKU YA SITA (6)
wewe ndugu msomaji ni zao la ufanyaji wa mapenzi wa wazazi wako. Kitu ambacho hata bwana Mungu hakikumfurahisha kwa mara ya kwanza na hii ni kwasababu kuu 3 (KIFO, UZAZI NA UTAFUTAJI)
1. Alijua binadamu wakizaliana na wakawa wengi lazima wafe.
2. Wakizaliana na kuwa wengi watakuwa wanazaliana sana hali itakayowapelekea kupata uchungu.
3. Alijua kila wakiwa wengi ndio liziki yao itazidi kuwa ngumu na kuanza kutafuta kwa jasho na kwa taabu sana.
Hivyo basi kama kuna magumu yeyote unayapitia katika dunia Mungu hapaswi kulaumiwa kwani wewe haukuumbwa na yeye.
Mungu alisha maliza maswala ya uumbaji tokea siku ya sita,
KINACHOENDELEA NI KUWA BINADAMU MNAUMBANA WENYEWE KWA WENYEWE.
Kama binadamu angeacha kuzaa basi binadamu angeshafutika kitambo sana katika ulimwengu.
Uwe na siku njema.