Hivi karibuni tumepigwa mabomu na kusambaratisha mikutano yetu au kutuwekea vizuizi kama kule Mwanza, Kahama, Dar na Dodoma. Baadhi tumefikishwa mahakamani kwa makosa ya kufanya mikusanyiko isiyo na kibali na kukaiadi amri za polisi. Hili si jambo jipya sana na hapa chini ntawakumbusha matukio kama haya yalivyotunufaisha kisiasa huko nyuma
Kila mtu anakumbuka mabomu ya Mtwara wakati wa gesi na vurugu hizo zilisambaa mpaka Lindi. Kaulize leo maeneo hayo ambayo mwanzoni yalikuwa ngome madhubuti ya Ccm yako mikononi mwa nani? Kumbuka vurugu za Nyamongo Tarime ambapo polisi wamepambana na raia kwa miaka zaidi ya 10 leo majimbo yote ya Tarime yako mikononi mwa Chadema.
Kumbuka matukio ya Arusha, mpaka Lema akapachikwa sifa ya kuuvuruga mji wa Arusha. Mauaji ya Soweto ayatosahaulika, lakini lilipokuja suala la uchaguzi Ccm walibaki na diwani mmoja Arusha. Kumbuka kipigo walichopata wakulima na wafugaji ktk mkoa wa Morogoro, ulipokuja uchaguzi wakayapeleka majimbo manne Chadema. Mnakumbuka alivyokandamizwa Sugu na Msigwa majimboni kwao, ulipokuja uchaguzi wananchi hawakuwachagua wao tu bali waliwakabidhi na majiji kabisa kwa kuwapa madiwani wa kutosha.
Hakuna sehemu ambapo demokrasia inakandamizwa kama Zanzibar lakini ukweli ni kwamba nchi hii hakuna sehemu upinzani umeshamiri kama Zanzbar. Wanatumia jeshi la polisi kutuzuia na kuminya uhuru wetu kabla ya kufanya utafiti jeshi hilo linaonekanaje mbele ya jamii. Haliwezi likawa linatupandisha? Yetu macho, haturudi nyuma.