Hatutaki Tabia hizi za wanaJF mibaba!

kila mtu ana uhuru wa kujieleza anavyojisikia, asipo sema wewe utajuaje? swala la democrasia ni pana sana linagusa maisha binafsi ya kila mtu kwa namna yoyote ile, kudhihirisha tabia na hisia, misukumo na tamaa za mwanadamu.
 
mapenzi ya moyoni hayaangalii chochote. Unapenda tu ukiulizwa umependea nini hujui sababu. Ni nadra sana hayo.
OFF TOPIC: nikuruhusu kurudi dar kwani mi nimekuzuia?
Kwani upo wapi?

Good. saved.
 
hivi hiyo mikutano ya kukutana ni ya lazima..?
mi sioni umuhimu wake...............
 
Katiba inasemaje kuhusu kutongozana?

Sidhani kama ina kifungu chochote kuhusu kutongozana. Labda tuliingize na hili kwenye madai ya katiba mpya?. Kifungu kitakuwa: Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu ana haki ya kutongoza na kutongozwa..........
 
Sidhani kama ina kifungu chochote kuhusu kutongozana. Labda tuliingize na hili kwenye madai ya katiba mpya?. Kifungu kitakuwa: Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu ana haki ya kutongoza na kutongozwa..........

Njia nyingine mbadala ni kupiga marufuku kabisa suala la kutongozana, tena kwa mujibu wa katiba ya nchi...Hapo sasa sijui wahanga watakuwa akina nani!
 
WanaJF tuna mawazo mazuri sana ya kukutana na kufahamiana, ila kinachosikitisha ni kwamba ndani ya mikutano hii majibaba mengine inatumia kutufataki! Inatongoza kila mdada!! Tuwafanyaje hawa? tuanzishe wikleaks kwa ajili yao?

Mmhh!! Wrong channel. Mie kijana mbichi, msomi na mtanashati. Contacts pls, za kiganjani na elektroniki.
 
mkitongozwa mnalalamika, usipotongozwa unalalamika, which is which? kwani unalazimiswa, ni maongezi tu, unasema hutaki basi,
au unasema nina wangu period, ww ni matured i hope, vp? that's nature ndio maana watu wanaoana, atajuaje kama hujaolewa au umeolewa? au mbona ukikubali mkila raha unasherehekea kwa miguno na full shangwe?
tena unaanza kusema sikujua kama JF ningempata mwanaume mzuri kama ww.
vitu vya kawaida sana hivi

No comment. True 100% kwa nyekundu, naongeza suala la kutukanana na binti takayeingilia kukupora hata kama penzi lenu ni kupatana kwa miezi tu!!
 
Unataka watu waandamane?

Sasa ndugu yangu tuwashaurije hawa wajukuu?

Naona wanataka kupigana na nguvu za Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na hii nchi ya hovyo kama Tz! Mimi nilidhani kila kitu kinaachwa kiende organically. Sasa kwa vile wajukuu hawakubaliani na sisi wababu, basi ngoja tuwatungie sheria na kuweka kwenye katiba yetu tukufu mpya tunayoisubiri kwa hamu.

Baaada ya hapo...No Kutongoza kwa mjibu wa katiba. Kinyume chake ni kuvunja katiba na sheri za nchi. Nadhani hapo nidhamu itarejea mahali pake!
 
Back
Top Bottom