Hatuna budi kumpongeza Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatuna budi kumpongeza Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPAMBANAJI.COM, Oct 28, 2011.

 1. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Kama umfuatiliaji makini wa viongozi basi utakubaliana nami kuwa Rais wako ni mtendaji mzuri sana katika suala la Utawala bora hususani katika vipengele vya uwazi na uhuru kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama JF.

  Pia ametoa uhuru mkubwa sana katika watu kujieleza.Hii ni tofauti kabisa na ngwe zilizopita.Nachofikiria happa sasa ni nani anayefaa kwa Tanzania ya miaka 5 baada yake.

  Hatuna haja ya kuangalia chama ila mtu atakayefaa kusimama kwa niaba ya watanzania wote. Kwa Dr. Slaa anawezafaa ila amegubikwa na lundo la mambo mengi ambayo yanampa emotion sana azungumziapo masuala ya kitaifa, kwa MAGUFULI nahisi anaweza asifanye tunachokitegemea.

  Kwa Sitta nahofia interest za Makundi.Kwa mgombea binafsi ndo hivyo serikali haikubali. sasa nani wa afadhali kuiongoza Tanzania baada ya Kikwete?. Je ni mimi au wewe? na kwani ni unayempendekeza?
   
 2. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Sio lazima ubandike thread hapa. Bandiko lako halina mashiko kabisa zaidi ya wewe kujipendekeza kwa Kiwete wako. Watanzania wapo milioni 40, wewe unawataja kadhaa tu, je watanzania wengine walipewa lini fursa za kuonyesha uwezo wao wa uongozi?

  Bado miaka 4 tufikie uchaguzi mwingine sasa kunasababu gani kuanza kuteseka kujadili wagombea ambao hata hawajatangaza nia ya kugombea?

  Mijadala kama hii inawafa wanamagamba ambao wameanza kuumana meno kwa uchaguzi wa 2015 kwa sababu ya imani zao za kifisadi kwamba mgombea yeyote anayewekwa na CCM nilazima ashinde.

  Kuparurani kote tunakokushuhudia sasa hivi ndani ya CCM kunatokana na imani hiyo. Subiri uone kama tutakuwa na katiba mpya ya wananchi, tume sahihi na huru ya uchaguzi na vijana wapewe fursa ya kuonesha vipaji vya uongozi walah mijadala ya kipuuzi kama hii haitakaa itokee.
   
 3. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Magamba nawasikitikia, yani kati ya miaka aliyotawala, umechanganua weeee hujaona kitu ukaona bora uje na hiyo point ?
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Uhuru wa vyomba vya habari na haki ya kuongea vinalindwa na sheria. Kwa maana basi raisi hatoi uhuru kwa vyombo vya habari (yani siyo maamuzi ya raisi atoe uhuru au laa) bali ni sheria. Kinyume na hapo ni kuvunja sheria. Maana unavyo ongelea ni kama vile raisi ndiyo mwenye maamuzi ya uhuru wa vyombo vya habari au laa.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa hili lazima Kikwete apewe credit. La urais baada ya miaka mitano unatania maana katiba yetu ambayo rais huyu inaiheshimu sana inazuia hilo.
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  hivi si kulikuwa na azimio la msekwa kuanzisha magamba forum? Kungekufaa kule na ungepata wanazi kibao
   
 7. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  JK hajui madhara ya kitu chochote alichoamua jana, anachoamua leo wala atakachoamua na kusema kesho. Hili alifikiri lingempa sifa kwa watanzania na jumuiya ya Kimataifa, ila madhara yake kulingana na madhambi yao halikuwa kwene akili yake. Sasa hivi naamini anatamani anafikiria namna ya kuvibana vyombo vya habari lakini haiwezekani tena, kwa taarifa yako ukombozi wa nchi hii utapatikana kwasababu watanzania wote wamepata na wataendelea kupata habari kuhusu ubazazi wote unaofanywa na viongozi wa Taifa hili.

  Serikali inapanga mengi kuhusu namna ya kuzuia taarifa kuwafikia wananchi kama huu mfumo wa digital tv unaokuja. Sio mfumo mbaya, kibaya ni jinsi huo mfumo unavyowekwa-wekwa kuipa serikali uwezo wai kuhakikisha wanazuia taarifa mbaya kuwafikia watanzania pale itakapobidi. Huu sio wakati wake wala hiyo njia haitofanya kazi tena maana kimsingi tayari ule uozo umeshakuwa wazi, nenda hata vijijini sasa wazee wale wakongwe kabisa wameshajua CCM ni wezi na wabadhirifu.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nadhan azimio la msekwa la magamba forumz ni baada ya kuchunana ngozi
   
 9. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Jifunze kuandika heading.
   
 10. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  hii post ni kinyesi, kawaambie waliomsaidia kampeni hao ndo wanaweza kumpongeza.
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,136
  Likes Received: 3,328
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha kumpongeza, Kwa mfumuko wa bei, maisha magumu na kukosekana kwa ajira.
   
Loading...