Ruto kajifunza Maridhiano the hard way, nasi hatuna budi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,827
Waswahili walisema kusikia kwa kenge ni tofauti sana na viumbe wengine wote:

Hata sisi hatuna namma nyingine kama ni nia yetu ya dhati kusikika.

FtAMUyLWcAMbElo.jpeg

Kwamba ni ripoti za CAG? Kwamba ni wahalifu sugu kuachiwa lakini si wanaoshikiliwa kisiasa?

FtAMUyMXwAAZf2I.jpeg

Bado tungependa tunayosema kucha kutwa yaweze hatimaye kusikika? Kwa namma hii ya kupiga makelele tu? Kwa hakika kama ni magonjwa, tutakuwa na Magonjwa Mtambuka!

--------------

Ruto anapojifunza maridhiano kwa maandamano​

ruto-pic.jpg

Jumapili, Aprili Pili, 2023, jua la Magharibi, Rais wa Kenya, William Rutto, alitoa hotuba ya kumwomba Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga na timu yake ya Azimio la Umoja One Kenya, kusitisha maandamano.

Wakati Ruto akitoa ombi hilo kwa Raila na Azimio, tayari hali ilishakuwa mbaya. Watu watatu walishapoteza maisha kutokana na maandamano yaliyoitishwa na Raila. Mali za watu ziliharibiwa na kuporwa na waandamanaji bandia. Biashara zilisimama na kuharibiwa.

Nyumba za ibada zilichomwa moto, kuna watu waliteka gari la polisi na kutokomea nalo Oyugis, Homa Bay. Watu zaidi ya 400, waliripotiwa kujeruhiwa, wengine majeraha yakiwa mabaya mno. Tamko lilikuwa maandamano ya amani, ila vitendo havikuakisi amani. Polisi walipotaka kutumia nguvu kudhibiti, machafuko yakawa makubwa. Polisi walikufa na kujeruhiwa.

Ombi la Ruto kwa Raila lilikuwa, maandamano yasitishwe ili kuruhusu mazungumzo ya vyama bungeni katika madai ambayo aliyatoa na kuyatumia kushawishi maandamano nchi nzima, vilevile na yeye (Ruto), milango yake ipo wazi kukutana na kiongozi huyo wa upinzani.
Saa moja baadaye, Raila alijibu hotuba ya Ruto kwa kutoa tamko la kusitisha maandamano ili kuruhusu mazungumzo ya vyama kuchukua nafasi. Vilevile kuheshimu mfungo wa mwezi wa Ramadhan, Kwaresma na ujio wa Pasaka.

Raila alisema, kama mazungumzo hayataleta matunda, watarudi tena kwenye maandamano baada ya wiki moja. Hivyo, aliomba wananchi wasiendelee na maandamano kupisha nafasi ya mazungumzo.
Kiini cha maandamano; Raila alikuwa na hoja mbili. Mosi, ikiwa ni manung’uniko ya kutotendewa haki kwenye Uchaguzi Mkuu Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022 na mazingira yake. Pili, ni kupaa kwa gharama za maisha.

Awali, Raila alitoa muda wa siku 14, Ruto kushughulikia malalamiko hayo. Kipindi hicho alichokitoa kilipopita pasipo maombi aliyoyatoa kushughulikiwa, ndipo aliitisha maandamano na yakaitikiwa.

Nyakati za mwanzo za maandamano, ungemwona Ruto akihutubia makundi ya watu, akicheka na kufanya mzaha kuwa Raila amwache arekebishe nchi kwa sababu mapatano yake na Rais mstaafu, Uhuru Kenyatta, ndiyo yaliyoharibu nchi.

Naibu Rais, Rigathi Kachagua, alikuwa mkali. Alisema, Raila aliitisha maandamano kumtisha Ruto ili waketi na kugawana mamlaka ya kuongoza, kama ilivyokuwa wakati wa Rais wa pili, Daniel Moi, Rais wa tatu, Mwai Kibaki na Uhuru.

Rigathi alisema, Ruto na yeye sio watu wa kutishwa. Aliongeza kuwa Uhuru, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, amekuzwa kwa virutubisho vya kiwandani (cerelac), ndio maana alipotishwa na Raila, aliketi wakazungumza.

Si hivyo tu, Rigathi aliahidi kuwa hata siku ambayo Ruto angekubali kukutana na Raila, yeye (Rigathi), angekwenda Ikulu ya Kenya na kuzuia mageti yote, kuhakikisha kiongozi huyo wa upinzani, hapati nafasi ya kupeana mkono na bosi wake.

Kinachotokea sasa, ni tofauti mno na mtazamo wa Ruto na tambo za Rigathi. Dirisha la mazungumzo limefunguliwa. Muhimu zaidi, aliyeomba ni Ruto. Kisha Raila akapokea. Rigathi akampongeza bosi wake kwa uamuzi wake wa busara.

Source: Mwananchi

"Ruto anapojifunza maridhiano kwa maandamano"
 
Tatizo letu tunaendeshwa kwa matakwa ya mtawala, anaanza kuharibu yeye, halafu badala sisi tumjibu kwa kuchukua hatua, tunamsubiri yule aliyeharibu aje kusawazisha kwa kutaka mazungumzo nae.

Hii tabia yetu imesababisha tumekuwa watu wa kuchezewa sana na watawala, ndio maana anaweza kuja yule asiyetaka mazungumzo, kwa sababu anajua hatuwezi kufanya chochote, au akaja wa mazungumzo lakini mwisho wa siku nae akaenda kinyume na yale waliyokubaliana, sababu nae anatujua tulivyo kondoo.

Hali ni tofauti na huko Kenya, wakenya wanajua kumshughulikia mtawala asiyesikia, mpaka mtawala mwenyewe anaamua kukaa chini na kuongea nao. Hapa pana uwezekano mkubwa kile kinachozungumzwa kikafanyiwa kazi 100% na mtawala ili alinde nafasi yake.
 
Kulikuwa na uzi huu:

Ni Tanzania tu, tunakotaka mabadiliko bila vitendo

Kama si Tanzania tu ingependeza kupata mfano wa nchi nyingine.

Kwa hakika yawezekana kelele zinazopigwa mitandaoni ni kubwa kuliko kelele za vyama vya siasa.

Yako wapi hata matamko tu ya vyama hivi hata kuhusu:

1. Maandamano Kenya?
2. Ripoti hii ya CAG?
3. Kuachiwa kwa Sabaya?
4. Watu kuendelea kuzuiliwa kisiasa?
5. Nk

Kwenye hali ambayo vyama vya siasa ni organized kuliko mwananchi mmoja mmoja, vikwepe vipi lawama vyama hivi?

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Angalizo: "yetu" kwa maana yake kamili.
 
Hayo mawili ya Ripoti ya CAG na kuachiwa Sabaya naamini ni suala la muda tu, uchambuzi utakuwa unaendelea kufanyika ndani ya vyama.
 
Biashara asubuhi. Kumbuka hata watu kama kina Pascal Mayalla wangali wamefichama. Hii inaleta mashaka ya kuwa kunavutwa subira kuona kwanza Mama ataelekea wapi, ili labda nao waelekee huko. Hao huwa hawapingani na mama hata kama akiamua kuwacharaza viboko kila siku asubuhi

Ubaridi huu hautusaidii.

Zingatia yapo mengi kwenye orodha kama mfano, nwe umeangazia mawili tu. Na hayo mengine vipi mkuu? Kwani nqko Nini kinasubiria? Au Yale Yale ya kupima upepo kwanza? Kwani hatuwezi kuwa wenyewe na kusimama na mawazo yetu kwa wakati kutegemeana na wapi tunaona haki imeegamia?

"Can't we just be ourselves?" -- Beberu.
 
Biashara asubuhi. Kumbuka hata watu kama kina Pascal Mayalla wangali wamefichama. Hii inaleta mashaka ya kuwa kunavutwa subira kuona kwanza Mama ataelekea wapi ili nao waelekee huko.

Ubaridi huu hautusaidii.

Zingatia yapo mengi umeangazia 2 tu. Na hayo mengine? Au Yale Yale ya kupima upepo kwanza? Hatuwezi kuwa wenyewe tu na kusema mawazo yetu kwa wakati kutegemeana na wapi tunaona haki imeegamia?

"Can't we just be ourselves?" -- Beberu.
Hayo mawili mengine niliyoyaacha nimefanya hivyo kwasababu naona moja liko kwenye mchakato wa maridhiano [watu kuendelea kushikiliwa] hivyo nalo inawezekana ni suala la muda tu hao jamaa wataachiwa..

La pili kuhusu Kenya, hapa sijui unataka jamaa waseme kitu gani kuhusu, kwamba tujifunze kutoka kwao kwa kile wanachofanya au una mtazamo gani mwingine?

Kama ni issue ya kujifunza kutoka kwao, kwangu naona mwenye macho haambiwi tazama, kila mmoja wetu anakiona kinachotokea Kenya, na sababu yao kufanya hivyo inajulikana na haitofautiani na kinachoendelea hapa kwetu, naona ni suala letu kuamka tu... sio tuendelee tusubiri kuamshwa mpaka lini..
 
Tatizo letu tunaendeshwa kwa matakwa ya mtawala, anaanza kuharibu yeye, halafu badala sisi tumjibu kwa kuchukua hatua, tunamsubiri yule aliyeharibu aje kusawazisha kwa kutaka mazungumzo nae.

Hii tabia yetu imesababisha tumekuwa watu wa kuchezewa sana na watawala, ndio maana anaweza kuja yule asiyetaka mazungumzo, kwa sababu anajua hatuwezi kufanya chochote, au akaja wa mazungumzo lakini mwisho wa siku nae akaenda kinyume na yale waliyokubaliana, sababu nae anatujua tulivyo kondoo.

Hali ni tofauti na huko Kenya, wakenya wanajua kumshughulikia mtawala asiyesikia, mpaka mtawala mwenyewe anaamua kukaa chini na kuongea nao. Hapa pana uwezekano mkubwa kile kinachozungumzwa kikafanyiwa kazi 100% na mtawala ili alinde nafasi yake.
Tafauti ya Kenya na Tanzania si jinsi ya wananchi wanavyogughulika na "watawala", tofauti yetu kubwa ni Ukabila.

Kenya wana serkali ya Majimbo, essentially ya makabila. Raila Odinga ni Mjaluo, kwao ni njimbo la Nyanza, makao yake makuu Kisumu. Gavana (Rais) wa Nyanza ni Okot Nyongo, Mjaluo. Mbunge wa Kikabila (Senator) ni James Orengo, Mjaluo. Kila mtu ni O, O, O, wote wajaluo. Idadi yao si wengi sana, ni kama 19% ya Kenya. Kabila zingine hivo hivo:Waluhya 23%, Wakikuyu 20% Kalenjin 21%. Unahitaji kabila 3 walau ili utawale kikabila kama hii Orange au Azimio in Wajaluo na wengine kwa majina (Kalonzo Mkamba; Martha Karua Kikuyu, na Oparanya mluhya lakini O na mabaki ya Waarabu wachache Mombasa).

Siasa za Kenya pia ni za kimila, kuchanjiana damu, liwalo na liwe, hatutaki hatutaki, wako tayari kufa. Rais wa kwanza wa Kenya alikuwa Jomo Kenyatta, Mkikuyu, baba yake Uhuru aliongoza mapambano dhidi ya wakoloni kwa kundi la MAUMAU, kwa kuchanjiana. Makamu wake alikuwa Jaramogi Oginga Odinga, Baba yake Raila, walikuwa hivi hivi. Wajaluo wako hata Tanzania, wachache zaidi ni wagomvi wagomvi, kila mji mkubwa mkubwa utawakuta na kota zao, Nairobi wako Kibera na Mathare. Kwa vile amri ni ya kikabila na amri imeshatolewa tangu zamani za Oginga mkubwa, Kenya hakuna amani hadi leo. Nia yao ni kuungana na makabila jirani makubwa kama Waluhya au madogo kama Wadigo wa Pwani.

Ndiyo maana Raila si msumbufy tu bali kweli anaweza kuleta vurugu asipothibitiwa, nadhani ndiko kunakoenda, itabidi nguvuvza kijeshi zitumike na Jeshi la Marekani liko Pwani likisubiri.

Sisi hatuna ukabila kama huo. Hiyo ndiyo tafauti yetu. Hatuna kitu kinachoitwa "wananchu" wala kinachoitwa "watawala" kwa misingi ya kikabila kama hizo O O O O za Raila. Watawala wao ni mwendelezo huo O O O katika serkali za kikabila wakiita majimbo.

Sisi ni Watanzania, Taifa kubwa lililoungana tangu Bukoba hadi Mikindani, tangu Pemba hadi Rukwa, Tangu Arusha hadi Meya, Kigoma hadi Bagamoyo. Watawala wetu ni Wazanzibari na Wahehe na Wahaya na Wachagga. Hatubaguani.

Sisi tuna Wakristu rasmi, Waislamu na Wapagani lakini tunapendana, Mufti wanafunga na Kardinali kuombea gonjwa la Covid Kenya wana makanisa ya mfukoni, kila mtu ana Askofu wake au Nabii wake, Raila ana ya kwake na Kenyatta ana yake kila mtaa na kila mkutano kuna Askofu mwanamke au mwanaume.

Cha kuogopa sisi ni hawa CHADEMA na siasa zao za Kenyakenya. Ukabila wao utaukuta diaspora kila mji wafanya biashara wa hardware na bar lakini ni wachache - kwao wachache na miji mikubwa ni wachache.

CHADEMA wangependa kabisa wawe kama Raila kwa vikundi vikundi vya kikabila wanataka kila kitu lakini idadi haitoshi.

Hata kwao nyumbani wameshajulikana nia, wamekataliwa hawana Mbunge hata mmoja, hadaa hadaa za mwanzo walikuwa 100% ndipo wakajiuliza kulikoni.

Kwa hiyo usitulinganishe na Kenya, ni sawa na mchana kutwa kweupe ni usiku wa kiza kweusi.
 
Biashara asubuhi. Kumbuka hata watu kama kina Pascal Mayalla wangali wamefichama.
Mimi mbona nipo sana tuu sijafichama
Hii inaleta mashaka ya kuwa kunavutwa subira kuona kwanza Mama ataelekea wapi, ili labda nao waelekee huko.
Unaanisha sisi ni ma bendera fuata upepo?
Hao huwa hawapingani na mama hata kama akiamua kuwacharaza viboko kila siku asubuhi
Karibu mitaa hii Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Na hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Hayo ni mabandiko ya bendera fuata upepo?.
P
 
Hayo mawili mengine niliyoyaacha nimefanya hivyo kwasababu naona moja liko kwenye mchakato wa maridhiano [watu kuendelea kushikiliwa] hivyo nalo inawezekana ni suala la muda tu hao jamaa wataachiwa..

La pili kuhusu Kenya, hapa sijui unataka jamaa waseme kitu gani kuhusu, kwamba tujifunze kutoka kwao kwa kile wanachofanya au una mtazamo gani mwingine?

Kama ni issue ya kujifunza kutoka kwao, kwangu naona mwenye macho haambiwi tazama, kila mmoja wetu anakiona kinachotokea Kenya, na sababu yao kufanya hivyo inajulikana na haitofautiani na kinachoendelea hapa kwetu, naona ni suala letu kuamka tu... sio tuendelee tusubiri kuamshwa mpaka lini..

Ukipenda boga wanasema upende na ua lake. Siyo Siri hatuko vizuri. Mengine tunayolalama ya nani kutochukua hatua ni mwendelezo ule ule wa kukosekana mwenye uthubutu wa kumfunga paka kengele.

Angalia haya:

1. Maandamano Kenya - Kila mtu takribani ana msimamo wake kulingana na anavyolielewa sakata lile. Ila sisi kama vyama tuko kama CCM tu hatuna msimamo. Hatuna kauli ya kuunga mkono au kulaani. Kwamba hilo tunaona sawa.

2. Ripoti ya CAG. Tangia imetoka vyama vyetu vinaifanyia kazi. Kuna rindima mitandaoni hadi CCM huko. Vyama vyetu kimya. Hadi sasa vinaifanyia kazi.

3. Kaachiwa Sabaya kwenye mazingira haya. Vyama vyetu kimya. Ni sehemu ya Maridhiano.

4. Kina George Sanga na wengi wengine wakiwamo masheikh bado wanashikiliwa kwa kesi hata zisizoanza. Sehemu ya maridhiano.

5. Kwenye nk. Yapo mengi yenye ukakasi Ikiwamo katiba mpya ambayo inakoelekea wengine inawaacha midomo wazi.

Kwa hakika yapo mengi, ila nyuzi hizi hapa zinawakilisha:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa
 
Tafauti ya Kenya na Tanzania si jinsi ya wananchi wanavyogughulika na "watawala", tofauti yetu kubwa ni Ukabila.

Kenya wana serkali ya Majimbo, essentially ya makabila. Raila Odinga ni Mjaluo, kwao ni njimbo la Nyanza, makao yake makuu Kisumu. Gavana (Rais) wa Nyanza ni Okot Nyongo, Mjaluo. Mbunge wa Kikabila (Senator) ni James Orengo, Mjaluo. Kila mtu ni O, O, O, wote wajaluo. Idadi yao si wengi sana, ni kama 19% ya Kenya. Kabila zingine hivo hivo:Waluhya 23%, Wakikuyu 20% Kalenjin 21%. Unahitaji kabila 3 walau ili utawale kikabila kama hii Orange au Azimio in Wajaluo na wengine kwa majina (Kalonzo Mkamba; Martha Karua Kikuyu, na Oparanya mluhya lakini O na mabaki ya Waarabu wachache Mombasa).

Siasa za Kenya pia ni za kimila, kuchanjiana damu, liwalo na liwe, hatutaki hatutaki, wako tayari kufa. Rais wa kwanza wa Kenya alikuwa Jomo Kenyatta, Mkikuyu, baba yake Uhuru aliongoza mapambano dhidi ya wakoloni kwa kundi la MAUMAU, kwa kuchanjiana. Makamu wake alikuwa Jaramogi Oginga Odinga, Baba yake Raila, walikuwa hivi hivi. Wajaluo wako hata Tanzania, wachache zaidi ni wagomvi wagomvi, kila mji mkubwa mkubwa utawakuta na kota zao, Nairobi wako Kibera na Mathare. Kwa vile amri ni ya kikabila na amri imeshatolewa tangu zamani za Oginga mkubwa, Kenya hakuna amani hadi leo. Nia yao ni kuungana na makabila jirani makubwa kama Waluhya au madogo kama Wadigo wa Pwani.

Ndiyo maana Raila si msumbufy tu bali kweli anaweza kuleta vurugu asipothibitiwa, nadhani ndiko kunakoenda, itabidi nguvuvza kijeshi zitumike na Jeshi la Marekani liko Pwani likisubiri.

Sisi hatuna ukabila kama huo. Hiyo ndiyo tafauti yetu. Hatuna kitu kinachoitwa "wananchu" wala kinachoitwa "watawala" kwa misingi ya kikabila kama hizo O O O O za Raila. Watawala wao ni mwendelezo huo O O O katika serkali za kikabila wakiita majimbo.

Sisi ni Watanzania, Taifa kubwa lililoungana tangu Bukoba hadi Mikindani, tangu Pemba hadi Rukwa, Tangu Arusha hadi Meya, Kigoma hadi Bagamoyo. Watawala wetu ni Wazanzibari na Wahehe na Wahaya na Wachagga. Hatubaguani.

Sisi tuna Wakristu rasmi, Waislamu na Wapagani lakini tunapendana, Mufti wanafunga na Kardinali kuombea gonjwa la Covid Kenya wana makanisa ya mfukoni, kila mtu ana Askofu wake au Nabii wake, Raila ana ya kwake na Kenyatta ana yake kila mtaa na kila mkutano kuna Askofu mwanamke au mwanaume.

Cha kuogopa sisi ni hawa CHADEMA na siasa zao za Kenyakenya. Ukabila wao utaukuta diaspora kila mji wafanya biashara wa hardware na bar lakini ni wachache - kwao wachache na miji mikubwa ni wachache.

CHADEMA wangependa kabisa wawe kama Raila kwa vikundi vikundi vya kikabila wanataka kila kitu lakini idadi haitoshi.

Hata kwao nyumbani wameshajulikana nia, wamekataliwa hawana Mbunge hata mmoja, hadaa hadaa za mwanzo walikuwa 100% ndipo wakajiuliza kulikoni.

Kwa hiyo usitulinganishe na Kenya, ni sawa na mchana kutwa kweupe ni usiku wa kiza kweusi.
Sidhani kama linapokuja suala la kudai haki yako kuna nafasi ya ukabila, wakenya wanaandamana kwa sababu ya ukali wa gharama za maisha, hili linawaumiza wote bila kujali makabila yao, sisi tumezubaa tusidanganyane na upole wetu au mchanganyiko wetu wa makabila, tunaumia lakini tumelala tu, siku zote tunaendeshwa na mtawala.

Ukweli wakenya wamechangamka, na kigezo cha ukabila kisitumiwe kwenye kila jambo, ndio maana wakaipata Katiba waliyonayo sasa kwa mtindo huo.

Nimekusoma nimeona ulichokiandika hapo juu ni muendelezo wa fikra mgando zilizotufikisha hapa tulipo, unataka tuendelee kuzubaa tu kwa kisingizio kwamba kudai haki zetu ni kufanya vurugu kunakosababishwa na ukabila, this is not right!.
 
Mkuu umetoa utetezi wenye nukuu zako za 2021 na 2022, ambazo aghalabu nazo comments za mwisho kwenye nyuzi hizo ni kabla ya:

1. Report ya CAG
2. Maandamano Kenya
3. Kuachiliwa Sabaya
4. Maridhiano nchini

Manne haya yamekuwa yakirindima vilivyo mitandaoni.

Kufichama kwako ni kutokusikika kwa sauti yako isiyokosa uwepo wa "maslahi ya taifa."

Ipo tofauti kubwa baina ya bendera kufuata upepo na kujipanga kimkakati zaidi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ukipenda boga wanasema upende na ua lake. Siyo Siri hatuko vizuri. Mengine tunayolalama ya nani kutochukua hatua ni mwendelezo ule ule wa kukosekana mwenye uthubutu wa kumfunga paka kengele.

Angalia haya:

1. Maandamano Kenya - Kila mtu takribani ana msimamo wake kulingana na anavyolielewa sakata lile. Ila sisi kama vyama tuko kama CCM tu hatuna msimamo. Hatuna kauli ya kuunga mkono au kulaani. Kwamba hilo tunaona sawa.

2. Ripoti ya CAG. Tangia imetoka vyama vyetu vinaifanyia kazi. Kuna rindima mitandaoni hadi CCM huko. Vyama vyetu kimya. Hadi sasa vinaifanyia kazi.

3. Kaachiwa Sabaya kwenye mazingira haya. Vyama vyetu kimya. Ni sehemu ya Maridhiano.

4. Kina George Sanga na wengi wengine wakiwamo masheikh bado wanashikiliwa kwa kesi hata zisizoanza. Sehemu ya maridhiano.

5. Kwenye nk. Yapo mengi yenye ukakasi Ikiwamo katiba mpya ambayo inakoelekea wengine inawaacha midomo wazi.

Kwa hakika yapo mengi, ila nyuzi hizi hapa zinawakilisha:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa
Anyway, hapa naweka mawazo yangu sitaki kujigeuza msemaji wa vyama.

Nionavyo, namna ambavyo chama kinatakiwa kutolea ufafanuzi uozo ulioanikwa kwenye ripoti ya CAG kwa mfano, ni tofauti nasi tunavyoandika huku mitandaoni.

Sisi huku tutaokoteza mawili matatu tuyazungumzie hayo, mengine tunaweza kuyaacha, lakini kwa upande wa vyama hali ni tofauti, wao wanawajibu wa kuichambua ile ripoti kwa undani zaidi, waguse kila angle, ili waje na majibu yanayojitosheleza, hivyo kwangu hawa wanahitaji muda zaidi.

Hata mengine kama ya kina Sabaya, nayo yanaweza kujumlishwa wakati utakapofika, wakizungumzia ripoti ya CAG, basi wanaweza kulizungumzia la Sabaya pia, hawabanwi na yeyote kutofanya hivyo.
 
Hayo mawili ya Ripoti ya CAG na kuachiwa Sabaya naamini ni suala la muda tu, uchambuzi utakuwa unaendelea kufanyika ndani ya vyama.
La Sabaya ni sawa na la Mbowe, zote chanzo chake ni tofauti kuwa Sabaya kashinda kesi yake, imesikilizwa mwanzo hadi mwisho.

Mbowe bahati yake ni Rais kaamua amsamehe kwa huruma yake tu.

Ila zote mbili zinamhusu ole Sabaya, ngoja nikupe.

Utakumbuka ushahidi wa tigopesa ulikuta Mbowe karushia makamandoo watatu hela za nauli na posho waende Moshi kumuua Mkuu wa,Wilaya ole Sabaya?

Ukaja ushahidi Afande "Homeboy" Urio aombwe na Mbowe amtafutite kwa siri makomandoo wamuue ole Sabaya?

Ukaja ushahidi wa Afande Jumanne na Kamanda Kingai kuwakamata wauaji wakiwa safarini kwenda kutekeleza misheni yao, wakapita kunywa mbege Rau Madukani ndipo wakakamatwa?

Kwa vile misheni yao haikufanikiwa, ole Sabaya aliponea chupuchupu kuuliwa lakini bado yuko hai. Si ndipo Mama kwa huruma yake kama Mama kuona bora amsaheme Mbowe yaishe ila asirudie tena?

Hii haiongelewi sana lakini ukweli ndiyo huu.
 
Jamaa unafanya nicheke, sasa kwanini Jamhuri hawakutumia huo ushahidi wa "tigopesa" kumtia Mbowe hatiani na baadae kumfunga gerezani, ajabu wakaja kumuachia bila yeye kuwaomba msamaha...

Tofauti na Sabaya, ambaye tuliona ndugu zake pamoja na yeye mwenyewe wakilia kila siku mahakamani kumuomba Samia amuhurumie?!
 
Tatizo letu tunaendeshwa kwa matakwa ya mtawala, anaanza kuharibu yeye, halafu badala sisi tumjibu kwa kuchukua hatua, tunamsubiri yule aliyeharibu aje kusawazisha kwa kutaka mazungumzo nae.

Hii tabia yetu imesababisha tumekuwa watu wa kuchezewa sana na watawala, ndio maana anaweza kuja yule asiyetaka mazungumzo, kwa sababu anajua hatuwezi kufanya chochote, au akaja wa mazungumzo lakini mwisho wa siku nae akaenda kinyume na yale waliyokubaliana, sababu nae anatujua tulivyo kondoo.

Hali ni tofauti na huko Kenya, wakenya wanajua kumshughulikia mtawala asiyesikia, mpaka mtawala mwenyewe anaamua kukaa chini na kuongea nao. Hapa pana uwezekano mkubwa kile kinachozungumzwa kikafanyiwa kazi 100% na mtawala ili alinde nafasi yake.
Kuna gharama katika hilo, umesikia kuna majeruhi 400 humo na vifo viwili.

Ikifikia hapo watanzania wanarudi nyuma na wapo tayari hata kuolewa na wanajeshi ila sio kusimamia haki zao kwa kupambana kwa jasho na damu. Watanzania hawaogopi kuandamana ila wanachoogopa ni kuwa watapigwa na hata wengine kufa. Wanataka ushindi wa mezani kitu ambacho hakipo.

Siku watanzania tukielewa kuwa hakuna maridhiano baina ya mwizi na anayeibiwa bali kuna vita ya haki ndipo tutasogea toka hapa tulipoganda.
 
Ni kweli kila ulichoandika, kasoro kuwa tayari kuolewa na wanajeshi.. labda wengine mimi hapana.
 
Kuna gharama katika hilo, umesikia kuna majeruhi 400 humo na vifo viwili.

Ikifikia hapo watanzania wanarudi nyuma na wapo tayari hata kuolewa na wanajeshi ila sio kusimamia haki zao kwa kupambana kwa jasho na damu. Watanzania hawaogopi kuandamana ila wanachoogopa ni kuwa watapigwa na hata wengine kufa. Wanataka ushindi wa mezani kitu ambacho hakipo.

Siku watanzania tukielewa kuwa hakuna maridhiano baina ya mwizi na anayeibiwa bali kuna vita ya haki ndipo tutasogea toka hapa tulipoganda.
Hahahahaha kuolewa na Wanajeshi??
 
Back
Top Bottom