Hatua za Kumuondoa CAG madarakani kwa mujibu wa ibara 144 ya Katiba

Mwanaukweli

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Messages
4,612
Points
2,000
Mwanaukweli

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined May 18, 2007
4,612 2,000
Kumwaondoa CAG madarakani kwa mujibu wa ibara 144 ya Katiba
144.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu yakushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.
(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:
(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.
(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume ita mshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.
(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(7) Masharti ya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyote aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.

img_20190415_215047-jpeg.1072454

Sent using Jamii Forums mobile app
 
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
5,007
Points
2,000
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
5,007 2,000
castieltsar

castieltsar

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2016
Messages
488
Points
1,000
Age
25
castieltsar

castieltsar

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2016
488 1,000
Tatizo sio majaji,tatizo ni mchakato wa kuwapata + uadilifu wao,
nadhani hawa majaji ni freerly kutoka sehemu yeyote since the case ni common kwamba anataka kuondolewa na watu wakubwa sababu kafichua maovu ....mabeberu hawatakagi mchezo kwenye maswala kama haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
5,266
Points
2,000
Age
43
M

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
5,266 2,000
Nina wasiwasi kuwa ndugai haisomagi katiba! Na au katiba haifuatwi na kulindwa katika uongozi wake!

Yambidi ajitafakari kwani raia wanaweza kudai mazingatio ya katiba waliyoapa kuilinda na ukawa mwanzo wa kudai katiba mpya! Anajisahau sana na kudhani watanzania ni wajinga wanaopenda kuburuzwa!

Ushauri kwa wabunge wa ccm kusimama imara na kumpinga huyu spika ili akiachie kiti kwani chaguzi zijazo zinaweza zisiwe na matokeo wanayoyatarajia!
 
Kuna kaulevi ka madaraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
E

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
1,983
Points
2,000
E

ebaeban

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
1,983 2,000
Mnakumbuka SANDURA commission iliyomwondoa jaji Mwakibete? Rais Mwinyi aliwahi kutekeleza hili takwa la kumwondoa jaji tu wa Arusha kwa tuhuma ya kupokea rushwa, ikabidi takwa la kuomba tume ya majaji watatu kutoka nchi nyingine mwanachama wa commonwealth waje wachunguze tuhuma za jaji litekelezwe, wakaja majaji watatu toka Zimbabwe wakiongozwa na jaji Sandura, matokeo ya uchunguzi ikabainika kweli jaji Mwakibete alipokea mlungula toka shirika moja la umma Arusha basi akaondolewa au kwa lugha kali akafukuzwa kazi.

Na hili la CAG linafanana na hilo, sijui wakati wa tume ya Sandura Spika Ngugai alikuwa ameisha zaliwa.
 
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
9,370
Points
2,000
Age
27
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
9,370 2,000
Mnakumbuka SANDURA commission iliyomwondoa jaji Mwakibete? Rais Mwinyi aliwahi kutekeleza hili takwa la kumwondoa jaji tu wa Arusha kwa tuhuma ya kupokea rushwa, ikabidi takwa la kuomba tume ya majaji watatu kutoka nchi nyingine mwanachama wa commonwealth waje wachunguze tuhuma za jaji litekelezwe, wakaja majaji watatu toka Zimbabwe wakiongozwa na jaji Sandura, matokeo ya uchunguzi ikabainika kweli jaji Mwakibete alipokea mlungula toka shirika moja la umma Arusha basi akaondolewa au kwa lugha kali akafukuzwa kazi.

Na hili la CAG linafanana na hilo, sijui wakati wa tume ya Sandura Spika Ngugai alikuwa ameisha zaliwa.
Ili la CAG halifanani na hilo.CAG wa sasa hama loose ends.. ndio maana speaker anapata ugum pa kumshika maana hapaoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Slowly

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Messages
1,701
Points
2,000
Slowly

Slowly

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2016
1,701 2,000
washabiki wa CAG mavi yanagonga chupi yanarudi....twendeni taratibu, ukitaka kumuua nyani usimchek usoni
 
M

m2020

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2016
Messages
919
Points
1,000
M

m2020

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2016
919 1,000
washabiki wa CAG mavi yanagonga chupi yanarudi....twendeni taratibu, ukitaka kumuua nyani usimchek usoni
Watu wa Chadomo wanamtetea CAG aliyekosa adabu. Huwezi kusema bunge dhaifu wakati hukagui bunge. Kwahiyo alitaka bunge limwambie nini rais ambaye yeye ndo muhusika na wasaidizi wake aliyekaguliwa?.
Kwamba rais ameshindwa kuwasimamia wasaidizi wake au?

Kwamba Magufuli awajibike kashindwa kazi au? Alitaka nini kifanyike?
 
Z

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,715
Points
2,000
Z

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,715 2,000
At
Mnakumbuka SANDURA commission iliyomwondoa jaji Mwakibete? Rais Mwinyi aliwahi kutekeleza hili takwa la kumwondoa jaji tu wa Arusha kwa tuhuma ya kupokea rushwa, ikabidi takwa la kuomba tume ya majaji watatu kutoka nchi nyingine mwanachama wa commonwealth waje wachunguze tuhuma za jaji litekelezwe, wakaja majaji watatu toka Zimbabwe wakiongozwa na jaji Sandura, matokeo ya uchunguzi ikabainika kweli jaji Mwakibete alipokea mlungula toka shirika moja la umma Arusha basi akaondolewa au kwa lugha kali akafukuzwa kazi.

Na hili la CAG linafanana na hilo, sijui wakati wa tume ya Sandura Spika Ngugai alikuwa ameisha zaliwa.
Atakuwa alikuwa bado kinda, mashavu hayajamvimba. Tangu yamvimbe amekuwa na kiburi na Lugha chafu za kuwaita wenzake "mbwa"
 
bichwa mtoto

bichwa mtoto

Senior Member
Joined
Aug 9, 2018
Messages
172
Points
500
bichwa mtoto

bichwa mtoto

Senior Member
Joined Aug 9, 2018
172 500
Watu wa Chadomo wanamtetea CAG aliyekosa adabu. Huwezi kusema bunge dhaifu wakati hukagui bunge. Kwahiyo alitaka bunge limwambie nini rais ambaye yeye ndo muhusika na wasaidizi wake aliyekaguliwa?.
Kwamba rais ameshindwa kuwasimamia wasaidizi wake au?

Kwamba Magufuli awajibike kashindwa kazi au? Alitaka nini kifanyike?
Duuu hii kasi ya mawazo yako ni 7G kumbe ndo maana mna ovarate mambo kwa kuongeza vitu visivyokuwa na umuhimu wowote na mnamtisha bwana mkubwa kwa kumnywesha mawazo kama haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LexPaulsen

LexPaulsen

Member
Joined
Jul 30, 2018
Messages
45
Points
125
LexPaulsen

LexPaulsen

Member
Joined Jul 30, 2018
45 125
Watu wa Chadomo wanamtetea CAG aliyekosa adabu. Huwezi kusema bunge dhaifu wakati hukagui bunge. Kwahiyo alitaka bunge limwambie nini rais ambaye yeye ndo muhusika na wasaidizi wake aliyekaguliwa?.
Kwamba rais ameshindwa kuwasimamia wasaidizi wake au?

Kwamba Magufuli awajibike kashindwa kazi au? Alitaka nini kifanyike?
Kwa hii comment mkuu nadhani una shida kwenye medula oblangata yako. Kwa sisi ambao ni raia wa kawaida tu hatuna vyama je? Sasa labda nikuulize, kwanza uliskiliza kwa makini mahojiano ya CAG yalivyopelekea kutoa ile statement? Unaijua kazi nyingine kubwa ya bunge kikatiba ukiacha kutunga sheria? Unajua umuhimu wa ofisi ya CAG kwenye uendeshwaji na nchi?

Tafakari mambo kwa akili huru, kama mzalendo, kma mtu mweledi. Mitazamo yako ya kimwinyi hiyo eti "CAG anakosa adabu" ndo inapelekea nchi hii kuendela kubaki hapo ilipo. Palipo na ukweli usemwe, tusilambane miguu wakati inanuka eboo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,285,033
Members 494,367
Posts 30,847,817
Top