Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Kumwaondoa CAG madarakani kwa mujibu wa ibara 144 ya Katiba
144.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu yakushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.
(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:
(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.
(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume ita mshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.
(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(7) Masharti ya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyote aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.
Sent using Jamii Forums mobile app