Hatua kumi za kukua kwa Lugumi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,073
114,571
1. Kampuni ya LUGUMI inasajiliwa mwaka 2008 ikiwa na mtaji wa Shilingi milioni 50 tu.

2. Miaka mitatu baadaye inapata Tenda ya thamani ya shilingi Bilioni 30 (Milioni 1000 x 30) kutoka Jeshi la Polisi.

3. CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali) amekagua na kubainisha kuwa kuna mabilioni yameibiwa, Lugumi imelipwa asilimia 99 ya fedha zote lakini imefanikisha asilimia 10 tu ya kazi husika.

4. PAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali) imekagua na kuielekeza POLISI ilete mkataba kamili kati ya POLISI na LUGUMI.

5. Polisi imesema haiwezi kutoa mkataba huo na kuipa Kamati ya Bunge ambayo haihusiki na masuala ya Ulinzi na Usalama.

6. Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya Ulinzi na Usalama imetupa mpira kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, yenye dhamana na polisi.

7. Polisi imejitoa katika ufuatiliaji wa suala hili ili kuepusha conflict of INTEREST (Mgongano wa Maslahi),

8. TAKUKURU sasa imeingilia suala hili...

9. Dash……Dash……Dash…..Dash!!!! (Tunga sentensi ya hatua namba 9 ikiwa na maneno “Mtumbua Majipu…..”)

10. MY TAKE; Mifumo na Taasisi zinazopaswa kusimamia nchi zote zimeoza na ziko likizo,Bunge nalo halina meno na haliwezi kuihoji serikali.

Anasubiriwa MTU MMOJA aje kutoa maelekezo ya nini kifanyike! Kamwe nchi
haitaendeshwa kwa kumtegemea mtu mmoja.

Kama TAASISI na MIFUMO yetu imekufa, Taifa litapiga hatua 3 mbele wakati huu,baada ya miaka mitano litarudi nyuma hatua 100!

Usininukuu.
 
Jibu lipo wazi pesa zimetolewa 99% kazi imefanyika 10%. Hizo fedha taslimu 89% zimekwenda wapi.

Kama zipo hawajazitumia basi wazirudishe zikafanye kazi nyingine. Tena wazirudishe zote ndani ya masaa 48.

kama wanaleta porojo ni dhahiri wamekula hakuna kesi ya kusikilizwa wafungwe kifungo cha maisha.

Namba siku zote hazidanganyi warudishe pesa za wananchi.
 
Escrow Account Tuliambiwa Siyo Pesa Ya Umma
Lugumi Tutaambiwa Hakuna Ubadhirifu Wowote
 
11. Hakuna fedha ya Serikali iliyoibiwa wananchi wasidanganywe na vyama vya upinzani
Huo msemo si ndio pia uli tumika kwenye ile Scandal mama kupozea wananchi umesha hamishiwa kwenye hili nalo? Kumbe hiyo hela ya kununulia hizo mashine ili zuka toka wapi vile?
 
Jibu lipo wazi pesa zimetolewa 99% kazi imefanyika 10%. Hizo fedha taslimu 89% zimekwenda wapi.

Kama zipo hawajazitumia basi wazirudishe zikafanye kazi nyingine. Tena wazirudishe zote ndani ya masaa 48.

kama wanaleta porojo ni dhahiri wamekula hakuna kesi ya kusikilizwa wafungwe kifungo cha maisha.

Namba siku zote hazidanganyi warudishe pesa za wananchi.
Pesa zipo na ndizo zinatumika kuwapa Rushwa kamati ya Bunge na wachunguzi wengine ili wamsafishe kitwanga asitumbuliwe JIPU , pesa ingine wameiandaa kuwalipa mawakili endapo kesi itapelekwa Mahakamani, na pesa zingine kalipwa January Kwa ajili ya kuwaletea Utitiri wa Sangoma toka Gambia na wachakachuaji wa mikataba waliobobea vyema.
 
Escrow Account Tuliambiwa Siyo Pesa Ya Umma
Lugumi Tutaambiwa Hakuna Ubadhirifu Wowote
Nchi hii ni shamba la bibi Thamani ya mashine haifiki hata bilion 1 lakini wajanja wakapiga bilion 37 wakagawana wengi sasa Zigo limemwangukia Lugumi lazima atafichwa Kama Balali ili asije kuwataja wote waliozitafuna pesa za umma.
 
Sasa wanahamishia akili za wananchi kwenye mradi wa DART eti mafisadi yalita kuuchuku, (haya mafisadi mbona hayasemwi kwa majina yao? anapata wapi kusema kuwa fulani na fulani ndio waliokuwa wanataka huu mradi uwe mali yao? Huyu LUGUMI mbona hamzungumzii ina maana hajasikia? Magufuli nae bwana, ni ileile soon, miluzi na vigelegele vitatoweka apitapo hawajui watanzania huyu!
 
Kweli nchi hii inategemea kichwa cha Magufuli. Hakuna nchi duniani inaendeshwa na mtu mmoja. Tuliposema mfumo hamkutuelewa!
Wacheni upotoshaji wa wazi, suala hili liko kwenye mhimili wa bunge mpaka Sasa, na bunge halijakaa na kulijadili na hatimae kutoa mapendekezo yake kwa serikali,
Sasa unapotoa ka mchango Kako mistari mitatu kama dakika tano za hotuba za Lowassa maana yake unaongelea jambo usilojua taratibu zake kisheria.. Ni vema kukaaa kimya kama huelewi jambo kuliko kukimbilia kuandika bila ufahamu
a0a010b846251bd3ed5f65406a00a110.jpg

By the way acheni magufuli afanye kazi, wengine waliahidi kwamba wakishindwa kupata urais watarudi monduli, lakini nashangaa bado wamebanana hapa hapa dsm na wamebaki kutumia watu msiojitambua Kuja humu majukwaani kurusha taarab.
 
Sasa wanahamishia akili za wananchi kwenye mradi wa DART eti mafisadi yalita kuuchuku, (haya mafisadi mbona hayasemwi kwa majina yao? anapata wapi kusema kuwa fulani na fulani ndio waliokuwa wanataka huu mradi uwe mali yao? Huyu LUGUMI mbona hamzungumzii ina maana hajasikia? Magufuli nae bwana, ni ileile soon, miluzi na vigelegele vitatoweka apitapo hawajui watanzania huyu!
Wewe binafsi unaijua mihimili ya dola au unakurupuka tu,
Hii mambo ya lugumi yako hatua ya bunge wewe unalazimisha Rais atoweIMG]https://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/c81a190c5d43245d11cb0056e7af595f.jpg[/IMG]e tamko halafu iweje?
Ni Ili mpate kick ya kumsema Rais kwamba haheshimu mihimili kama bunge na mahakama au?
 
bunge halina meno ni km mbwa anaebweka lakini angati. unatwgemea nini km mzee wa madili yote nyoka wa mdimu ndio yupo kwenye kiti lazima bunge lioze. kwa sasa hakuna bunge bali ni wapiga dili tu.
 
Back
Top Bottom