Pohjois Haaga
Member
- Jun 29, 2015
- 47
- 16
1. Kampuni ya LUGUMI inasajiliwa mwaka 2008 ikiwa na mtaji wa Shilingi milioni 50 tu.
2. Miaka mitatu baadaye inapata Tenda ya thamani ya shilingi Bilioni 30 (Milioni 1000 x 30) kutoka Jeshi la Polisi.
3. CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali) amekagua na kubainisha kuwa kuna mabilioni yameibiwa, Lugumi imelipwa asilimia 99 ya fedha zote lakini imefanikisha asilimia 10 tu ya kazi husika.
4. PAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali) imekagua na kuielekeza POLISI ilete mkataba kamili kati ya POLISI na LUGUMI.
5. Polisi imesema haiwezi kutoa mkataba huo na kuipa Kamati ya Bunge ambayo haihusiki na masuala ya Ulinzi na Usalama.
Spot on mzalendo!!! hivyo ina maana hili jambo tutayayushwa tu au kweli sharia itachukua mkondo wake...? Vinginevyo hawa wakina Msamaki wataonekana wamewajibishwa simply kwa kuwa walikuwa kama watoto yatima kwenye mfumo wetu huu wa Tanzania ambao ulijaa/umejaa selective justice (haki pendelevu/chaguzi).
6. Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya Ulinzi na Usalama imetupa mpira kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, yenye dhamana na polisi.
7. Polisi imejitoa katika ufuatiliaji wa suala hili ili kuepusha conflict of INTEREST (Mgongano wa Maslahi),
8. TAKUKURU sasa imeingilia suala hili...
9. Dash……Dash……Dash…..Dash!!!! (Tunga sentensi ya hatua namba 9 ikiwa na maneno “Mtumbua Majipu…..”)
10. MY TAKE; Mifumo na Taasisi zinazopaswa kusimamia nchi zote zimeoza na ziko likizo,Bunge nalo halina meno na haliwezi kuihoji serikali.
Anasubiriwa MTU MMOJA aje kutoa maelekezo ya nini kifanyike! Kamwe nchi
haitaendeshwa kwa kumtegemea mtu mmoja.
Kama TAASISI na MIFUMO yetu imekufa, Taifa litapiga hatua 3 mbele wakati huu,baada ya miaka mitano litarudi nyuma hatua 100!
Usininukuu.