Pre GE2025 Polisi kushindwa kuchukua hatua dhidi ya aliyekuwa DC wa Longido, wanatupatia ujumbe gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,982
47,887
Nchi yetu, na hasa Jeshi la Polisi, kwa vitendo vyake, linadhihirisha kuwa halipo kwaajili ya kuutumikia umma, halipo kwaajili ya kusimamia sheria, wala kulinda haki za msingi za raia na binadamu kwa ujumla.

Nchi hii kumekuwa na matukio ya kishetani kabisa, matukio ya kuteka, kutesa na kuua watu, ambayo yamekuwa yakifanyika dhidi ya raia wasio na hatia yoyote kwa mujibu wa sheria za nchi. Washukiwa wakuu wa uovu huo, ambao wamekuwa wakinyoshewa vidole, kwa mtazamo wa wananchi wengi na ushahidi wa kimazingira wamekuwa ni Polisi na UVCCM.

Wakati watu wakiendelea kutekwa na kupotezwa, na vyombo vya usalama vikiendelea kunyoshewa vidole na wananchi, anatokea kiongozi mwandamizi wa Serikali, mkuu wa Wilaya, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya, na mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM ya wilaya, anatoka hadharani na kutamka kwa uwazi kuwa ushindi wa CCM wajati wa uchaguzi huwa hautokani na kura za wananchi bali kwa uharamia ambao Serikali huwa inafanya dhidi ya wapinzani huko maporini, halafu polisi wapo kimya!! Kama polisi hawahusiki kabisa na huo uharamia, na imekuwa ikinyoshewa vidole kuhusiana na huo uharamia, huyu aliyejitokeza wazi na kutamka kuwa yeye ni miongoni mwa maharamia hao wa kuwapeleka watu porini, bila shaka ni kuwateka, kuwaua na kuwatupa porini, Polisi si wangekuwa wamepata pa kuanzia? Mbona polisi wapo kimya? Au polisi huwa ni sehemu ya huo uharamia ambao wapinzani hufanyiwa huko porini ndiyo maana wanashindwa kuchukua hatua?

Na kuna yule kiongozi wa UVCCM mkoani Kagera, alitamka wazi, akiwaagiza polisi kuwa endapo kuna mtu yeyote atanayemkosoa Rais au Serikali atapotea, Polisi wasimtafute, akimaanisha kuwa wao UVCCM watakuwa ndio wamempoteza. Na kwa sasa kuna vijana viongozi wa BAVICHA na wanaharakati wametekwa na kupotezwa, kama Polisi siyo wahusika, na hawawajui wahusika wa huo ushetani wa kuteka watu, mbona huyu aliyetamka wazi kuwa ni mhusika, hajawahi kukamatwa na kuhojiwa mpaka leo?

Rais Samia amechukua hatua za kiutawala dhidi ya haramia aliyekuwa DC wa Longido. Ilitegemewa baada ya huyu bwana kuondolewa kwenye nafasi ya uongozi, vyombo vingine, ikiwa ni pamoja na polisi, vingefuatia katika kuchukua hatua dhidi yake, LAKINI cha ajabu, tunashuhudia hakuna hatua zozote?

Je, umma tuamini kuwa ushetani aliokuwa anaufanya aliyekuwa DC wa Longido, ulihusisha pia jeshi la polisi, ndiyo maana hawawezi kuchukua hatua? Je tuamini pia kuwa Polisi inafuata maagizo ya kiongozi wa UVCCM kuwa wakosoaji wa Serikali wakitekwa na kupotezwa Polisi hawatakiwi kuwatafuta kwa sababu ni CCM kupitia UVCCM ndiyo itakuwa imewateka na kuwapoteza?

kwa kweli kama Taifa tupo kwenye laana kuu, maana tuna Jeshi la Polisi ambalo lipo haraka sana kuchukua hatua dhidi ya watu wasio na hatia lakini lipo kimya dhidi ya uovu mkubwa kama wa upotezaji wa uhai wa binadamu? Je, wao ni washiriki katika uovu huo? Kama siyo washiriki, kwa nini wanashindwa kuchukua hatua dhidi ya uovu huu wa kuwateka na kuwaua raia huku kuna watu wanajitokeza na kutamka kuwa wao ni sehemu ya washiriki?

PIA SOMA:
 
DC alitumikia waliomtuma hivyo hawawezi kumfanya lolote kwa sababu wao ndio watawala hamna wakuwahoji.
 
Sio yeye wa kwanzaukiacha huyu katibu hata marehemu alishasisitiza "des nikupe kila kitu alafu umtangaze mpinzani? Hiiii"
Pia mama alishasema hata msipopigia kura ccm.. ila ccm ulitaunda serikali.
Kwahiyo sio la polisi kutochukua hatua kosa ni la sisi watanzania wenyewe
Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
 
Sio yeye wa kwanzaukiacha huyu katibu hata marehemu alishasisitiza "des nikupe kila kitu alafu umtangaze mpinzani? Hiiii"
Pia mama alishasema hata msipopigia kura ccm.. ila ccm ulitaunda serikali.
Kwahiyo sio la polisi kutochukua hatua kosa ni la sisi watanzania wenyewe
View attachment 3087197
Yeah!...halafu hao Polisi mabosi zao ni wanasiasa
 
Sio yeye wa kwanzaukiacha huyu katibu hata marehemu alishasisitiza "des nikupe kila kitu alafu umtangaze mpinzani? Hiiii"
Pia mama alishasema hata msipopigia kura ccm.. ila ccm ulitaunda serikali.
Kwahiyo sio la polisi kutochukua hatua kosa ni la sisi watanzania wenyewe
View attachment 3087197
Hii inadhihirisha kuwa tunaongozwa na watu waovu, wafuasi waaminifu wa shetani!!

Kama ndivyo, je, ni halali kwa watu wema kuwa chini ya shetani? Nasi tumekubali kuwa washirika wa uovu kwa kuuafiki utawala wao? Hata kama mtu ni mnyonge wa kiasi gani, bado una nafasi ya kujitenga na waovu, kwa namna uwezayo, ili usishiriki ujira wa uovu wao.
 
Kabisa unaacha kufikiri mambo ya muhimu, unawafikiria Polisi wafanye kitu kwa mwanaccm?
Kutokufanya kitu kwao kunatupatia uthibitisho uiso na shaka kuwa uovu huu wa utekaji ambao DC wa Longido alikiri kuwa Serikali inafanya, polisi kwa uhakika, ni miongoni mwa mikono inayotumika. Na hivyo jeshi la polisi linakuwa halina uwezo wa kuchukua hatua dhidi yake lenyewe.
 
Ujamaa(ccm) ni breeding ya communism. Na unaposema communism , unamzungumzia stalin.. Na unapomtaja stalin . Unataja kitu kinaitwa nkvd. Na unapotaja nkvd unataja sekeseke la great purge ya 1937.. Nachotaka kusema ni , ngumu sana kumwajibisha huyo.
 
Nchi yetu, na hasa Jeshi la Polisi, kwa vitendo vyake, linadhihirisha kuwa halipo kwaajili ya kuutumikia umma, halipo kwaajili ya kusimamia sheria, wala kulinda haki za msingi za raia na binadamu kwa ujumla.

ni wanashindwa kuchukua hatua dhidi ya uovu huu wa kuwateka na kuwaua raia huku kuna watu wanajitokeza na kutamka kuwa wao ni sehemu ya washiriki?
Tatizo siyo polisi tatizo liko kwenye jamii
 
Nchi yetu, na hasa Jeshi la Polisi, kwa vitendo vyake, linadhihirisha kuwa halipo kwaajili ya kuutumikia umma, halipo kwaajili ya kusimamia sheria, wala kulinda haki za msingi za raia na binadamu kwa ujumla.

?
ALIFANYA KAZI YAKE ALIYOPEWA VIZURI, HANA HATIA KAMA POLISI WETU WANAVYOPATA MAELEKEZO KUTOKA JUU
 
Tlaatlaah, Lucas Mwashambwa na Stuxnet mna lolote la kusema kwenye hili?

Naona "Msiojulikana" na "wachawi/washirikina" sasa mmeanza kujisema wenyewe na kuweka matendo yenu ya kishetani wazi...

Tutawajua mmoja baada ya mwingine..
kama Taifa,
lipo jukumu muhimu sana na zito kwa manufaa na mustakabali wa maendeleo ya waTanzania wote, na Dr Samia Suluhu Hassan, kiongozi wa nchi yetu na kipenzi cha waTanzania wote anatuongoza vizuri sana katika hilo,

nalo ni kuliunganisha Taifa na kuifungua nchi Kimataifa..

wenye nia au dhumuni la tatiza na kuhujumu uelekeo, dhamira na nia njema ya Rais, wataondolewa kwenye nafasi zao bila mbambamba yoyote, na hakutakua na haja nao tena na hatuwez kamwe kubabaika na yeyote, ispokua kuchapa kazi kwa bidii, uadilifu na weledi kuelekea uchaguzi wa kihistoria wa serikali za mitaa baadae Nov 27, 2024, na uchaguzi mkuu wa Oct 2025, ambapo waTanzania wote wameshaamua kuambatana na Dr Samia Suluhu Hassan kwa kishindo, anapokwenda kuhitimisha muhula wake muhimu sana wa pili mamlakani,🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Nchi yetu, na hasa Jeshi la Polisi, kwa vitendo vyake, linadhihirisha kuwa halipo kwaajili ya kuutumikia umma, halipo kwaajili ya kusimamia sheria, wala kulinda haki za msingi za raia na binadamu kwa ujumla.

Nchi hii kumekuwa na matukio ya kishetani kabisa, matukio ya kuteka, kutesa na kuua watu, ambayo yamekuwa yakifanyika dhidi ya raia wasio na hatia yoyote kwa mujibu wa sheria za nchi. Washukiwa wakuu wa uovu huo, ambao wamekuwa wakinyoshewa vidole, kwa mtazamo wa wananchi wengi na ushahidi wa kimazingira wamekuwa ni Polisi na UVCCM.

Wakati watu wakiendelea kutekwa na kupotezwa, na vyombo vya usalama vikiendelea kunyoshewa vidole na wananchi, anatokea kiongozi mwandamizi wa Serikali, mkuu wa Wilaya, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya, na mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM ya wilaya, anatoka hadharani na kutamka kwa uwazi kuwa ushindi wa CCM wajati wa uchaguzi huwa hautokani na kura za wananchi bali kwa uharamia ambao Serikali huwa inafanya dhidi ya wapinzani huko maporini, halafu polisi wapo kimya!! Kama polisi hawahusiki kabisa na huo uharamia, na imekuwa ikinyoshewa vidole kuhusiana na huo uharamia, huyu aliyejitokeza wazi na kutamka kuwa yeye ni miongoni mwa maharamia hao wa kuwapeleka watu porini, bila shaka ni kuwateka, kuwaua na kuwatupa porini, Polisi si wangekuwa wamepata pa kuanzia? Mbona polisi wapo kimya? Au polisi huwa ni sehemu ya huo uharamia ambao wapinzani hufanyiwa huko porini ndiyo maana wanashindwa kuchukua hatua?

Na kuna yule kiongozi wa UVCCM mkoani Kagera, alitamka wazi, akiwaagiza polisi kuwa endapo kuna mtu yeyote atanayemkosoa Rais au Serikali atapotea, Polisi wasimtafute, akimaanisha kuwa wao UVCCM watakuwa ndio wamempoteza. Na kwa sasa kuna vijana viongozi wa BAVICHA na wanaharakati wametekwa na kupotezwa, kama Polisi siyo wahusika, na hawawajui wahusika wa huo ushetani wa kuteka watu, mbona huyu aliyetamka wazi kuwa ni mhusika, hajawahi kukamatwa na kuhojiwa mpaka leo?

Rais Samia amechukua hatua za kiutawala dhidi ya haramia aliyekuwa DC wa Longido. Ilitegemewa baada ya huyu bwana kuondolewa kwenye nafasi ya uongozi, vyombo vingine, ikiwa ni pamoja na polisi, vingefuatia katika kuchukua hatua dhidi yake, LAKINI cha ajabu, tunashuhudia hakuna hatua zozote?

Je, umma tuamini kuwa ushetani aliokuwa anaufanya aliyekuwa DC wa Longido, ulihusisha pia jeshi la polisi, ndiyo maana hawawezi kuchukua hatua? Je tuamini pia kuwa Polisi inafuata maagizo ya kiongozi wa UVCCM kuwa wakosoaji wa Serikali wakitekwa na kupotezwa Polisi hawatakiwi kuwatafuta kwa sababu ni CCM kupitia UVCCM ndiyo itakuwa imewateka na kuwapoteza?

kwa kweli kama Taifa tupo kwenye laana kuu, maana tuna Jeshi la Polisi ambalo lipo haraka sana kuchukua hatua dhidi ya watu wasio na hatia lakini lipo kimya dhidi ya uovu mkubwa kama wa upotezaji wa uhai wa binadamu? Je, wao ni washiriki katika uovu huo? Kama siyo washiriki, kwa nini wanashindwa kuchukua hatua dhidi ya uovu huu wa kuwateka na kuwaua raia huku kuna watu wanajitokeza na kutamka kuwa wao ni sehemu ya washiriki?

PIA SOMA:
ambae yuko kinyume na dhamira, nia njema na uelekeo wa kiongozi mkuu wa nchi, atawekwa kando na kazi ya kufikia azma ya Rais ya kuliunganisha Taifa na kuifungua nchi Kimataifa lazima ifikiwe katika muda na wakati muafaka...

changamoto ndogo ndogo, visirani, mihmko, makasiriko, uzishi wa tuhuma mbalimbali dhidi ya Taasisi za umma vitaendelea kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria,
Lakini kamwe kazi ya kuwaleta waTanzania wote pamoja, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa Nov.27,2024 na uchaguzi mkuu ujao baadae Oct 2025, hazita simama hata kidogo..

waTanzania wanataka maendeleo, na hayo lazima yawafikie huko wa lipo chini ya uongozi madhubuti sana wa kipenzi chao Dr.Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Back
Top Bottom