Hats off to Jenerali Twaha Omar Ulimwengu

Jenerali amesema kitu nilichowahi kusema hapa, watwawala wetu si kweli kwamba hawawezi kuondoa umasikini wetu, bali hawana nia hiyo tu.
 
RWANDA ya KAGAME. Mimi naishangaa Tanzania yetu. Nchi kama Marekani ina raia wa nchi zote duniani na imeendelea kwelikweli tena kwa kuzitumia mbongo na vipaji vya raia hawa "wakuja"!

Wildcard; you have a point!
Na ukijiuliza vizuri, ni yupi anayetufaa, mtu asiye raia ila productive kwetu au mtu ambaye ni raia ila fisadi?
 
Mmmmh, kumbe Kitine ndiye aliyeanzisha ishu ya uraia wa Jenerali...
 
Wapendwa huwa sipendi kuweka nakala za gazeti hapa kwa sababu naona kama si kuwatendea hako wenye gazeti ila kwa hii nakala naona nivunje mwiko hapa hiyo para ya mwisho
Shalom aksante kwa makala hii imetulia sana...!
 
Mmmmh, kumbe Kitine ndiye aliyeanzisha ishu ya uraia wa Jenerali...


ningependa kuongelea kitu kimoja tu hapa, Pamoja na Tanznaia kuwa ni kama nchi isiyo na misimamo na ufisadi mkubwa, lakini ni ukweli usipingika kuwa idara ya usalama kitengo cha kuwafatilia watu kina dat za kutosha sana, hii issue ya kuwa huyu ni raia na huyu sio, sidhani kama hawa jamaa huwa wanakurupuka tu, wana evidence za kutosha katika haya mambo, na kuna kitu kingine ambacho watu wengi tunashindwa kukijua kuhusu hizi sheria za uraia au ni vipi mtu anakuwa raia na vipi anakuwa sio raia,
mfano mdogo tu ambao ndio nahisi uliomtokea Ulimwengu ni kuwa, kama wazazi wake hawakuwa raia wa Tanganyika say ni wa Rwanda, na walikuwa Tanganyika wakati wa wakati wa kuform Tanzania, basi automatically nao wanakuwa raia wa Tanzania (kWA MUJIBU WA SHERIA) LAKINI WAKITAKA SIO KWA KUWALAZIMISHA, KAMA WAZAZI WAKE HAWAKUKUBALI KUCHUKUA URAIA WA TANZANIA BASI WALIKUWA WANAKAA TANZANIA KAMA WAGENI JAPO WALIKUWEPO WAKATI KUFORM TANZANIA, sasa mtoto atakaye zaliwa atakuwa na haki ya uraia wa nchi mbili ama tatu kutokana na asili za wazazi wake, kama baba na mama yake ni wa nchi moja basi mtoto anakuwa na uraia wa nchi mbili, nchi ya wazazi wake na nchi aliyozaliwa, kama wazazi wake wanatoka nchi tofauti basi mtoto anakuwa na uraia wa nchi tatu (baba, mama, ya kuzaliwa), LAKINI MTOTO ANAPOFIKISHA UMRI WA MIAKA KUMI NANNE NI LAZIMA AKANE RAIA ZINGINE NA KUBAKI NA URAIA WA NCHI MOJA, HAPA NDIPO KWENYE TATIZO KUBWA, WATU WENGI HUWA WANAJISAHAU NA KUJIONA NI RAIA WA KUZALIWA BILA KUCONSIDER URAIA WA WAZAZI WAKE
NA WATU WENGI WANAISHI HIVYO NA TUNAO MITAANI, TATIZO KUBWA LINAKUJA UNAPOTAKA KUINGIA KWENYE SIASA NA SIO KUINGIA TU BALI KUFUKUNYUA NA KUTAFUTA HAKI KUTOKA KWENYE SIASA, HAPO NDIPO MAKABRASHA YATAKAPOENDA KUFUNGULIWA NA KUAMBIWA WEWE SIO RAIA
 
Bravo Jenerali Ulimwengu!! You dare speak openly!!! Ila I am afraid nchi yetu haina uhuru wa habari, na sitashangaa wakikuandikia barua za kukuonya eti usiandike masuala ya kuwachanganya wananchi na kuleta vurugu!! Nchi kama Rwanda inatamani sana iwapate watanzania waende kule kufanya kazi hata zile sehemu nyeti, na Kagame alishatangaza hilo. Alisema atafurahia sana hii Federation maana atafaidi sana vichwa vya kutoka nchi nyinginezo!! Vijembe vijembe ndani ya chama. Je tutafika!!
 
Wapendwa huwa sipendi kuweka nakala za gazeti hapa kwa sababu naona kama si kuwatendea hako wenye gazeti ila kwa hii nakala naona nivunje mwiko hapa hiyo para ya mwisho

Nimeisoma ile habari nikapata picha halisi kuwa CCM ni chama cha kihuni yaani wanakuvictimise just kwa kuwa hutakiwi ndani ya chama. Na nimeipenda statement ya kuwa kama Bashe si raia mbona Mkulo hakujatolewa tamko lolote kuhusu uraia wake. Ikiwa Bashe msomali mbona kuna wanachama waandamizi ni wasomali na hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa (i.e. Kinana). Hizi ni zama za anguko la CCM wananchi tunaanza kuona uozo wa ndani ya CCM na inasikitisha kwa kweli
 

Hivyo bwana Kituko unataka kutwambia kuwa wazazi wa Bashe walikuwa hawalijui hilo? Au unataka kujistify decision ya Kamati kuu ya chama? Na je kama hakuwa raia mbona CCM walikuwa wakimpa vyeo lukuki tu inamaana ndani ya CCM hakuna mtu aliyeliona hilo akaliweka sawa kabla haijafika huku? Huu ni unafiki tu acha kutuzingua.
 
Ukisoma kwa undani hii makala ni Jenerali yeye anataka kumlipua KITINE period, kwani hajaongelea kabisa mapungufu ya sheria kama yapo. Kingine anachoongelea ni kuwa mbona wengine hawachunguzwi uraia wao? Sasa inanipa shida hapa tunaanza kusheherekea kuwa kintine alikuwa ndo amemmaliza, kwa nini tusiombe waandishi wengine wamfate KITINE wamuulize ili tupate upande mwingine. N ni kwa nini Twaha hataki kueleza kwa undani, wakati ule si aliambiwa sheria huwa hivi, kama kuna mahali unaona umeonewa basi nenda mahakamani, sasa kwa nini alivyata? Hili swala liko open saana kwa nchi kama yetu ambayo watu hawako registered ni rahisi saana kuwa mamluki, lakini inapofikia unaingia kwenye nafasi nyeti na watu wakaja kuhoji uraia wako ni lazima watu wafuatilie, na hii ndo imemkuta Bashe.
 

Hapana...nia haikuwa hivyo ndio maana makala nzima hakuna pahala jina la Kitine kutajwa....ni sisi tumeelewa hivyo....nia ya Jenerali ni kumwonya Chiligati asifananishe suala la utata wa uraia wa uchaguzi wa 2010 na la kwake kwa kuwa yeye alipopata matatizo ya uraia hakuwa anagombea cheo na nyakati na mazingira ni tofauti...angetaka kumuumbua au kumlipua kama utakavyo wewe Kitine angefanya hivyo years ago.....Kama Kitine nae anayake ya kusema aseme na wala si jukumu la JF kufanaya hivyo kwa sababu Jenerali hakumtaja Kitine kwenye makala yake...Tusitoke nje ya mada
 
Safai_ni_safari
Naomba urudi ukaisome tena mtu anyetajwa hapo ni Kitine, ametumia fani yake tu kumzunguka na kutumia kauli ya Chiligati ili amlipue KITINE. Sasa mimi nakuomba wewe hebu muulize ni kwa nini aligoma kwenda mahakamani?
 

hao wawili ni spent forces mkuu...

kuna mmoja msomali kamtaja... he is still in force...

unamjua? ni ofisa mstaafu wa jeshi...

yupo kila pahala nyeti... kamati kuu.. halmashauri kuu...

na hata kwenye kamati ya mwinyi nae alikuwemo.........
 

hapo kwenye bold mkuu...

mimi najitoa katika wenye kusikitika kuona CCM ikianza kujichinja yenyewe kwani ni kawaida kuwa milki zote za kidunia hatimaye huanguka na milki mpya kunyanyuka..

nenda CCM kale ugali na mwalimu
 
Safai_ni_safari
Naomba urudi ukaisome tena mtu anyetajwa hapo ni Kitine, ametumia fani yake tu kumzunguka na kutumia kauli ya Chiligati ili amlipue KITINE. Sasa mimi nakuomba wewe hebu muulize ni kwa nini aligoma kwenda mahakamani?

Hapana..hata pamoja na sourness ya hiyo paragraph inayomlenga Kitine,the main issue kwake kwa uelewa wangu ni kwa nini Chiligati ameunganisha issue ya Bashe na ya Kwake...kama angalitaka kumlipua Kitine kwa nini wakati huu amabapo yeye na Kitine hawana mgongano wowote uwe wa kimaslahi au kiitikadi? KITINE mwenyewe kwishney kwa sasa
 
hapo kwenye bold mkuu...

mimi najitoa katika wenye kusikitika kuona CCM ikianza kujichinja yenyewe kwani ni kawaida kuwa milki zote za kidunia hatimaye huanguka na milki mpya kunyanyuka..

nenda CCM kale ugali na mwalimu

Kaka humo mie simo nimeamua ni bora nikae sina chama chochote kwani CCM kumeoza na upinzani siwaamini nawaona kama opportunist wanakuwa na hidden ajenda behind nilishasema tangia zamani. Nasikitikia wale walamba miguu wanaokubali kula kila kitu nawatakia kila la kheri
 
Jenerali T.K.O. Ulimwengu alikuwa prefect wa bweni fulani pale Tabora School mwanzoni mwa miaka ya sitini, nadhani ilikuwa ni kati ya mwaka 1963 au 1965 hivi- watu walioko TS wanaweza kunikumbusha kama bado ile list majina ya maprefect wa zamani imetundikwa pale dining hall. Niliposikia kuwa eti yeye siyo raia wa Tanzania, nilishangaa sana kwani wakati ule tulikuwa na serikali ambayo ilikuwa inafanya kazi zake sawasawa kiasi kuwa isingekuwa rahisi kwa raia wa nje kusoma kwenye sekondari za serikali bila kufahamika.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…