Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,263
- 17,138
RWANDA ya KAGAME. Mimi naishangaa Tanzania yetu. Nchi kama Marekani ina raia wa nchi zote duniani na imeendelea kwelikweli tena kwa kuzitumia mbongo na vipaji vya raia hawa "wakuja"!Hivi Jenerali naye alituhumiwa kuwa raia wa nchi gani?
Nami nimemsoma Jenerali. Lakini angetutendea haki zaidi kama angeeleza alilimalizaje sakata lile. Pengine ingekuwa msaada mkubwa kwa wengine ambao naamini wako wengi wanaokumbana dhahma kama hii. Kuwashambulia Kitine na Mkapa ambao tayari ni "spent forces" hakujatusaidia sana mashabiki na wasomaji wake. Baadhi yetu tulikuwa tunajua waliomwandama.
Wakuu,
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa makala za 'Rai ya Jenerali' toka zilipoanza nadhani 1994(Gazeti la Rai wakati huo)...zinanivutia lakini hizi za toleo lililopita(Na.146 Raia Mwema) na wiki hii (Na.147 Raia Mwema)...zimenigusa sana hasa hii ya leo....huyu bwana alikaa kimya sana kuhusu sakata lake la uraia lililoibuliwa na serekali ya Mkapa....lakini leo kwa upeo wa hali ya juu na kwa utaalamu mkubwa wa kiuandishi amenifanya nimuelewe vizuri sana....nimeshindwa kuiweka makala hii hapa....lakini amemmaliza Chiligati kwa hoja ya kumhusisha yeye Jenerali na suala la Bashe.....laiti waandishi wetu wengine wangeandika kama huyu bwana basi mabanzi ya mbao katika macho yetu,kutu katika bongo zetu na nta katika masikio yetu vingetokomea kabisa.
Thank you Jenerali if you are in the forum!!!
binafsi namkubali kama mmoja wa wandishi sugu katika nchi hii.... utakuwa umanisaidi mimi na wanajamii humu kama utafanikiwa kuiweka makala hii humu ndani!!
Muulize privately (nadhani atapenda hivyo)....... jenerali@gmail.com
Ni kweli ile makala imeanika mambo mengi ambayo wengi hatuwa tunayajua. Kwa mantiki hiyo hiyo ya kuweka mambo hadharani, Jenerali ingefaa akasema alimalizaje kwa njia hii ya makala.
Hii itasaidia kuona mwelekeo wa suala la Bashe ambalo ni msaada kwa Bashe mwenyewe na watanzania wengine ili tupunguze kudhani.
Kama uko Tanzania nunua gazeti lake la Raia Mwema, kama uko nje ya Tanzania bofya hapo chini, gazeti la wiki hii utaliona kwanzia kesho kamasijakosea.
Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo
.
Ahsante kwa kazi nzuri, ila tunaomba ututumbukizie toleo NO 147
.
Ahsante kwa kazi nzuri, ila tunaomba ututumbukizie toleo NO 147
Siri ya Tanzania kuwa na makabila 120+ ni kutokana na biashara ya utumwa zaidi.Njia kuu za kupitishia watumwa kwa upande huu wa Afrika ziliishia Tanzania (Kilwa,Bagamoyo,Pangani na Zanzibar) kwa hiyo makabila mengi sana yalitoka nje ya mipaka yetu ya sasa na kuja ku settle hapa.Ila nadhani ingekuwa haki kuwa watu wote waliokuwepo wakati wa uhuru(1961) na Muungano(1964) pamoja na uzao wao uliofuta baadaye wawe automatically ni raia na sio kundi la watu wachache wenye nguvu za mamlaka kuamaua nani ni Raia,based on muonekano wa sura yake.Binafsi nilipata shida sana kupata passport kutokana na muonekani wangu kwa sura ambao sijui hata ulikotokea.Jamaa wa Immigration walinipa taabu sana kupata hiyo pasi,ati siyo Raia nami nikawaambia basi nirudisheni huko mnakodhani mimi ndio kwetu.
Kimsingi ukiwa focused sana na mambo yanayowafaidisha wakubwa watakutafutia jiwe la kuhangaika nalo kama wanavyomfanya Mtikila. Kama mkapa angeshupaliwa kwamba ni wa Nchumbichi, Nyerere kuwa mtusi na watu wote wa mipakani wakasogezewa nje ya nchi, ni mgogo tu ambaye angebakia kuwa mtanzania halisi kwa kuwa majirani zao wote ni ndani kwa ndani.
Hata Komba n Mzulu! Wabantu wote waende kwao Matebeleland. Mwisho wa siku Tanzania haina wenye nchi, wote ni wahamiaji tu. Kudadadeki. Sasa ndio maana by streets definition ni mchezo mchafu.
Siri ya Tanzania kuwa na makabila 120+ ni kutokana na biashara ya utumwa zaidi.Njia kuu za kupitishia watumwa kwa upande huu wa Afrika ziliishia Tanzania (Kilwa,Bagamoyo,Pangani na Zanzibar) kwa hiyo makabila mengi sana yalitoka nje ya mipaka yetu ya sasa na kuja ku settle hapa.
Ila nadhani ingekuwa haki kuwa watu wote waliokuwepo wakati wa uhuru(1961) na Muungano(1964) pamoja na uzao wao uliofuta baadaye wawe automatically ni raia na sio kundi la watu wachache wenye nguvu za mamlaka kuamaua nani ni Raia,based on muonekano wa sura yake.
Binafsi nilipata shida sana kupata passport kutokana na muonekani wangu kwa sura ambao sijui hata ulikotokea.Jamaa wa Immigration walinipa taabu sana kupata hiyo pasi,ati siyo Raia nami nikawaambia basi nirudisheni huko mnakodhani mimi ndio kwetu.