Hatma ya polisi kuuwa wananchi wasio na hatia ni nini hasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya polisi kuuwa wananchi wasio na hatia ni nini hasa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jul 17, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Siku hizi kusikia kwamba mwanachi asiye na hatia ameuwawa na Polisi si jambo la ajabu tena.Polisi nao sasa wanajichukulia sheria mikononi mwao.Matukio ya namna hii yameripotiwa na vyombo vya habari kule Dar es Salam,Arusha,Tunduma,na hivi karibuni kabisa kule Kyela.Nina hakika kwamba yako mengi ambayo kwa bahati mbaya yanapita kimya kimya bila kuripotiwa.Huwa mimi najiuliza kuna nini hasa?

  Binafsi ningependa kujua kwa kina kwa nini hasa matukio haya yanatokea.Kwa bahati mbaya anayejua kwa usahihi kabisa sababu ya mauaji hayo ni muuaji,yaani polisi,lakini mara nyingi sio rahisi yeye kutoa ukweli.Lakini it all boils down to one fact,and that is,ameua.Sasa tutaendelea na mtindo huu wa Polisi kuua wanachi wasio na hatia mpaka lini?

  Sio siri tena kwamba wanachi walio wengi hawana imani kabisa na jeshi la Polisi,nikiwemo mimi mwenyewe.Si jisifu,lakini mimi ni raia mwema kabisa.Lakini sijui ni lini jamaa hawa wataninyemelea na kutaka kunichuna kwa nguvu kama wale jamaa zangu wa Ifakara na hatimaye mauti kunikuta.Au hata sijui ni lini tutagongana mtaani!No,let's be serious we are in a very bad situation indeed.Polisi badala sasa ya kuwa walinzi wa wananchi wamekuwa watesi wao.

  Niseme jambo moja wazi,katika hali kama hii,serikali inategemea wananchi wafanye nini.Wakae chini walie na huku wanaendelea kunyanyaswa na hata kuuwawa?Baya zaidi ni kwamba, kwa wale polisi wanaoua na kunyanyasa wananchi, mambo yanaisha kimya kimya tu,na haya yote wanachi wanaona na wanayajua.Namhurumia sana Zombe,wanaweza kumtoa kafara!

  Naiomba serikali ijue kwamba mateso wanayopata wananchi kutoka kwa polisi ni mengi, tumepoteza imani na jeshi hilo kabisa.Labda ni vema serikali ikaunda tume ya maridhiano,ili kila aliyepata mateso kutoka kwa polisi apate nafasi ya kusema,na polisi aliyetesa aombe msamaha au achukuliwe hatua,vinginevyo tunakoelekea sio kuzuri hata kidogo.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hakika Serikali inabidi ilifikirie hilo na ichukue hatua za haraka sana kulitatua kabla nguvu za umma hazijashika kasi.
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ni kweli wakati mwingine polisi hawako makini kabisa katika utendaji wao wa kazi, labda tuangalie hii inaletwa na nini?

  Polisi kila siku wanapenda kufanya kazi kwa jazba, sijui ni kwa nini wanafanya kazi hivyo, ni wachache mno ambao wakiwa confroted na raia wanaweza kureason na raia na kufikia compromise, ( sina uhakika kama inatokana na training) wanajiona wako above the ordinary citizen and the citizen has to obey hata kama ni wrong.

  Sijui kama hii ni sababu au matokeo, haki za raia polisi hawazijui kabisa na hii ni setback kubwa sana huwezi kuwa kaulimbiu "usalama wa raia" wakati hata haki zao huzijui. Ni uhimu polisi wafundishwa hili, raia hata akiwa mhalifu bado ana haki zake.

  Nyenzo kutumika mahali ambapo sii pake, sidhani kama ni absolutely necessary wakati wa kuzuia maandamano polisi wawe na live ammunition. Mbona wenzetu ulaya kuzuia maandamano hawaendi na AK 47, the same to maandamano ya China, Iran hatuoni silaha kali kwa nini sie.

  Cumulative effect ya vitu hivi vitatu ni kuwa ukitaka kureason na polisi kuhusu haki yako lazima argument itatokea, which will lead to the exessive use of the firearm which is in his possession na mwisho kifo kutokea.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa kiasi kikubwa ni training inagomba!
  Mbona Polisi wa nchi zingine hasa za majuu hawapigi mtuhumiwa kiasi kile?
  Hapa Bongo mara nyingi utakuta katika kumpiga mtuhumiwa, wanajenga mazingira ya kumfanya mtuhumiwa aonekane ni mkorofi sana, na hatimaye wapewe hongo kubwa zaidi.
   
Loading...