Hatma ya Katiba Mpya: Kikwete na Karata ya Kisiasa Kuangamiza Taifa 2011

Sitaki kuamini wala siami kama ccm na kikwete wao watajaribu kubana hili,wakifanya hivyo wamekwisha
 
Kwa mtaji wa walichokitangaza kwenye gazeti rasmi la serikali kama muswada inaonyesha wazi kwamba haswaa ndio lengo la Kikwete na CCM. Na kwa kujua kwamba kuna uwezekano wa kuzuka wakati wowote maandamano kwa nchi nzima sasa ndio maana wametuma ujumbe mzito wa siri kwa Kibaki kuomba msaada wa vyobo vya dola pindi mambo yakiharibika.

Hadi sasa Makamu Mwenyekiti wa CCM taifa, Mzee Msekwa, hivi sasa anaoongoza timu hiyo ya wakataa mabadiliko juu ya agenda huko Nairobi.

Sitaki kuamini wala siami kama ccm na kikwete wao watajaribu kubana hili,wakifanya hivyo wamekwisha
 
Na nyinyi hamuna wema kwa lolote lile analofanya JK. Mulitaka katiba mpya mumeambiwa itaandikwa, sasa si musubiri huo utekelezaji wake ndiyo museme?
we shoga bitmkongwe umechakachuliwa akili hauko sawa kabisa jamani kuna mwenye CV ya uyu binadamu anipe niipitie?
 
Jiulize Kwanza, nashukuru sana kwa kunisaidia kwa kumzuilia mbali huyo mwenzetu aliyechelewa kidogo kuamka au tusema anayeshiba kutokana na mfumo wa kifisadi wa hivi sasa na kuchukulia tu kimzaha kwamba akishiba yeye basi Watanzania wooote nasi tushajishibia tu.

Nadhani rekodi zote nchini zitatutetea kwamba wananchi hata siku moja hatukusema kwamba tunahitaji bora katiba toka kwa serikali ya Kikwete bali letu mpaka kesho ni kutafuta katiba bora ilioandikwa moja kwa moja na sisi wananchi huku serikali ikijichukulia tu kiti cha abiria wa kawaida na wananchi tukishika usukani.

Na hilo ndilo jambo tunalolitetea mpaka darini bila kuchoka, kutetereka, kutishika wala kufumba macho kwa lolote lile; leo na kesho - Uwezo Tunao na Mungu yupo upande wetu, vita kutafuta haki mbeeeele kama tai kaka!!!!!!!!!!

we shoga bitmkongwe umechakachuliwa akili hauko sawa kabisa jamani kuna mwenye CV ya uyu binadamu anipe niipitie?
 
Ulaghai wa Kikwete na mchezo wa karata tatu kuliangamiza azma yetu wananchi kutaka katiba mpya niliokua nikiwatahadharishe hapo Mwezi Januari ndio huu hapa.
 
East African Law Society inajikomba kwa Serikali ili ipate tu kiwanja cha kujenga au inajikomba zaidi ya hivyo. Na kwanini iwe ni baada ya UDASA kuendesha kongamano la katiba mpya juzi?
 
KWA makusudi ya toleo hili la waraka huu tunapenda kuweka msisitizo kwamba kutokana na ukweli kuwa wanawake ndio wanaoteseka zaidi ya wanaume nchi hii iwe ni katika kilimo, kuchota maji, kubeba mizigo, usafiri na uchukuzi, malezi ya watoto, tiba na afya, masomo na kazi ni lazima wanawake washirikishwe kikamilifu katika uandikaji wa katiba mpya.

Ushiriki wa wanawake hauwezi kamwe kuwa kamilifu na timilifu, mpana na wa kina na unaokusanya maoni ya wanawake wote, wale wa mjini kama vile ilivyo kwa vijijini, wakulima kwa wafanyakazi, wanafunzi kwa wasio wanafunzi, walioolewa na wasioolewa, matajiri kwa masikini, wake wa wakubwa kwa wake wa wadogo, wasichana wasio na matumaini ya kesho achilia mwakani na watoto wa vizito ambao wameandaliwa kila kitu tayari mezani na ingawa hawajavunja ungo mipango yao ya masomo hadi chuo kikuu na ndoa zao zimeshakamilika NI LAZIMA BASI KUWE NA CHOMBO MARIDHAWA NA CHENYE NAFASI TOSHA na chombo hicho hakiwezi kamwe kuwa TUME YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA kama inayotaka kuundwa na Mheshimiwa Rais bali MKUTANO AU BARAZA LA KATIBA MPYA 2011 ambalo ndilo litakalotoa hadidu za rejea kwa Tume shirikishi itakayoundwa na Baraza hilo ambalo baadhi ya wajumbe wake pia watakuwa wanatume.

Kwa taadhima na heshima zetu tunamkumbusha rais na serikali yake kwamba sio wao WALIO JUU YA WANANCHI BALI NI WANANCHI TULIO JUU YAO. UKUBWA TULIOWAPA SIO TIKETI YA KUTUBURUZA KATIKA JAMBO AMBALO KWA UUNGWANA WAKE Rais ameshakubali kuwa ni shughuli inayohitajika kufanyika kulifaa taifa hili kwa miaka zaidi ya hamsini (50) kama kweli hakuwa mnafiki wakati anatoa kauli hiyo.



Wabunge wasikubali mswaada huu wa marekebisho ya Katiba

Waheshimiwa wabunge,

MUSWAADA wa marekebisho ya katiba ya JMT iliyopo nimeuchukulia kama mzaha au utani mkubwa toka kwa wale waliouandaa ambao wanatia mashaka kama ni Watanzania wenye uchungu na jinsi nchi yetu inavyoendeshwa kwa udhaifu na mapungufu makubbwa na kama kweli wanakitakia mema na bora kizazi chetu kijacho.

Baada ya kuzungumza na wazee wawili watatu waliokuwa wameshika nyadhifa za juu katika masuala ya sheria nchini nikafunguliwa macho na masikio na kugundua kwamba muswada huo ni hila makusudi ya CCM katika kujinunulia muda na kurefusha mchakato wa katiba bila kujali gharama inazozidi kuwabebesha wananchi ikiwemo zile za Richmond, Dowans, Ufisadi Benki Kuu, IPTL, leseni za madini na mikatba mingine bomu kama hiyo.

Rais na chama chake imedaiwa kwamba wana malengo mawili. Lengo hilo ni kuwa kwa kuleta muswaada mbovu bungeni na kuwatumia watu wasio wataalamu kuuandaa waliamini kuwa wanasheria na vyama vya upinzani watakwenda mahakamani. Na watu walio ndani kabisa ya chama tawala na serikali wanasema hayo ndiyo yaliyokuwa matarajio yao. Kwa bahati mbaya, wanakongamano na wanasheria wote kwa ujumla walio na mapenzi ya nchi na watu wake na siyo mapenzi na chama fulaani cha kisiasa wakagutukia hili. Wamekataa kwenda mahakamani. Na wanatafuta njia mbadala ambazo mchakato pamoja na kuchelewa kidogo lakini utaendelea kuliko kusimamishwa kabisa.

Lingine ambalo CCM na kiongozi wake wanaomba litokee kwa kupeleka muswaada mbovu bungeni ni kuwa wabunge na wanaharakati wanaoipenda nchi yao na wanaotaka haki ya wananchi kuwa na katiba waliyoshiriki kuiandaa wataukataa nayo itapata sababu ya kuurejesha ulikotoka na hivyo kuendelea kupata nafasi ya kupumua na kuuchelewesha muswaada huo ili katiba mpya isipatikane kabla ya uchaguzi mkuu.

CCM ina uhakika kuwa katiba iliyopo hivi leo ndio katiba tu itakayoweza kuwasaidia kuiba kura tena mwaka 2015 na kurejea tena madarakani na kwamba katiba hiyo ikikatishwa muda wake kabla ya mwaka 2015 CCM haitakuwa na muda wa kujijenga upya na kurejesha kuaminiwa na kukubalika kwake nchini kama baadhi ya vyama vya upinzani vinavyoaminiwa na kukubalika sasa bila hata ya kwenda kwa babu!

CCM imeshindwa kuamini kwamba matatizo ya nchi hii hayaruhusu wao kulazimisha kubaki madarakani na kama watafanya hivyo na huku chama hicho kikianza kutafuta msaada wa dini fulani nchini tayari watakuwa wamepanda mbegu ya kuleta vilio na misiba Tanzania mwaka 2015 kwani haitakuwa rahisi kwa watu na vyama vyao na wagombea kukubali kuibiwa kura kwa mara nyingine tena.

Ni mzaha kwa hiyo viongozi wa CCM wanapoongelea amani na umoja nchini humu na huku wanawatumia viongozi wa dini fulani kuwaunga mkono; wanachezea mchakato wa katiba na ujio wa sheria mpya; wanagombana wenyewe kwa wenyewe; wanaifilisi hazina; wanawatumia watu wasio hata na elimu ya sekondari kuwashauri; wanabagua watu, wilaya na mikoa na uongozi umeanza kugeuka wa kibabe kwa kukaripia na kuwakosoa watumishi wa umma hadharani kudhani kuwa chama hicho kweli kinataka amani na umoja uendelee kuwepo hapa Tanzania na kama chama hicho kitaondoka bila kufanya vituko, fujo na ghasia endapo kitashindwa katika uchaguzi mkuu ujao. Ielweke kwa wapenda amani wote Tanzania kwamba CCM kwa kuleta muswaada kama huu bungeni imetangaza kwamba ni ADUIA WA AMANI NA UMOJA WA WATANZANIA!

Pia nilishiriki katika kongamano lililofanyika UDSM chini ya UDASA na kwa kweli nimefurahishwa na uzalendo wa wote waliohudhuria pale, pamoja na kuonekana dhahiri kwamba CCM imepuuza kongamano hilo na imemtuma mamluki ambaye kazi yake ni kuhama toka kusiko na maslahi na kwenda kwenye maslahi. Kuwepo kwa wataalamu na wasomi hawa lakini kukosekana kwa CCM kunadhihirisha kitu kimoja tu. Nacho sio kingine lakini namna ambayo serikali yake ilivyowadharau na kupuuza kutumia ushauri wa wataalamu na badala yake kuwa mtumiaji mkubwa wa ushauri wa watoto wa mjini au wakaa vijiweni.

Inaelekea kazi ya kuandaa muswaada huu ilifanywa na watu wa karibu na Ikulu ambao kwa kuwa wananufaisha uongozi uliopo na chama tawala kwa namna moja au nyingine walipewa kazi hii.

Na pamoja na kulipwa mapesa mengi kilichofanyika ni 'kucopy na kupaste' na kama Profesa Shivji angelipewa nafasi katika kongamano la pili la katiba pale mlimani alikuwa na mengi tu ya kukosoa. Haikuwa hivyo. Lakini kilichodhirika hatima ya yote ni kwamba muswaada huo ni mbovu na haufai kukubaliwa na bunge la wabunge wanaowajali na kuwatetea watanzania hata kama watahongwa mabilioni ya fedha kwa maana watakuwa wameichimbia misingi ya maangamizi na upotevu nchi yao na vizazi vyake vyote vijavyo. Wabunge ukataeni muswaada huu.

Ikumbukwe Kenya ilichukua miaka mingi kupita kiasi kutokana na ubishi wa viongozi wa chama tawala. CCM ijue basi kuwa kama inavyowabebesha Watanzania gharama haramu za IPTL, ndege ya rais, ukarabati wa majengo ya wakubwa, kuingilia TANESCO na mashirika mengine katika kazi zao, safari za nje za viongozi wake, Dowans, Ufisadi benki kuu ndivyo pia inavyotaka kuwabebesha Watanzania gharama zisizo na sababu kwa kufanya madudu katika uandaaji wa muswaada wa katiba. Na nia ya chama tawala ni dhahiri: 'inataka kama ikiwezekana katiba mpya wasiwepo na iendelee kuwatawala Watanzania kwa katiba ya viraka milele na milele!'

Hayumkiniki, kama CCM ina nia ya kweli ya kuwapa Watanzania katiba mpya. Maana kinachozungumzwa humo ni marekebisho ya Katiba. Ingawa tunashangaa uungwana wa mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM ulipoishia maana alishawaahidi mengi Watanzania kuhusiana na katiba lakini kaishia pungufu kwa asilimia 75 katika kauli zake na kututia Watanzania wapenda haki na amani wasiwasi mkubwa.

Hili ni pamoja na ule ukweli kwamba katika mfumo wa vyama vingi, uwazi na ukweli hatuna budi kusema kwamba mheshimiwa rais kadiriki KUPORA madaraka ya wananchi kwa kupendekeza kuteua tume ya uchaguzi badala ya kuwaachia wananchi katika makundi yao ya kimaslahi kuchagua baraza la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 20111 kwa utashi na ridhaa yao wenyewe bila kuingiliwa na mkuu yoyote wala chama chochote. Kwa heshima na taadhima, tunamuomba rais awarudishie Watanzania kilicho chao, yaani, mamlaka juu ya uundaji wa Katiba mbadala ya JMT, na yeye abakie na chake, yaani, Chama cha Mapinduzi na serikali iliyoko madarakani.

BARAZA LA KATIBA LA JMT 2011 ambalo litaundwa kwa kuhakikisha kila mkoa, kila kundi la maslahi, watumishi wa serikali, vyama vya kisiasa, viongozi wa dini, wabunge waliopo, wakulima, wafanyakazi, wazee, wanawake, watoto, vijana wote wanapata fursa ya kuwawakilisha wenzao barazani ndilo linalostahili kuunda Tume ya Katiba Mpya ya Tanzania kwa kuchagua miongoni mwa wananchama wake na nje ya baraza hilo watu wa kuiwezesha tume hiyo kufanya kazi hiyo bila upendeleo, kwa haki, ukweli, uwazi, kitaalamu na kiufundi.

Kuna kila sababu ya CCM kuogopa ujio wa Katiba Mpya. Hili linaeleweka. Lakini ni dhambi isiyosameheka kwa wabunge, wawe wa upinzani au wa chama tawala kutosa matarajio, matazamio, mustakabali, maslahi na amani ya watoto wao, wajukuu zao na vizazi vyao eti kwa kuikoa CCM na hatari iliyoko mbele yake. Katika suala hili, ni dhahiri tutatambua ni nani anaiwakilisha CCM bungeni na ni nani anawakilisha wananchi wake bungeni. Ni dhahiri, ikiwa mbunge ni mtu mwenye kufaa na manufaa kwa watu wake haijalishi anatokea chama gani. Na hili kwalo sasa Watanzania wameanza kuamka baada ya kugundua wabunge toka upinzani pia wanaweza kufanya makubwa kama serikali na CCM isipowachezea shere katika maamuzi na mipango ya majimbo yao.

CCM ingelikuwa na akili, kwanza ingelijizaa upya na kujipanga kufuatana na katiba maridhawa ambayo pengine itakuwa bora kuliko ile ya Kenya kama sio ile ya Marekani tayari kwa ajili ya Tanzania mpya ambayo mafiga yake yatakuwa demokrasia, haki na usawa na amani na umoja.

Ni makosa kwa hiyo pia kuwa na kifungu chochote katika muswaada huo ambacho kinawatisha wananchi ambao ndio mabwana na waajiri wa serikali na rais kwa lolote lile. Hii itakuwa ni sawa na kumwibia mwananchi haki yake na kisha kumtisha kumtia ndani endapo atalalamika kwamba ameibiwa na anaendelea kuibiwa.

Wananchi kama mabwana na matajiri wa watawala (serikali na rais) kimsingi ndiyo wenye haki ya kuamua juu ya vipi wale wanaotaka kuwatawala watatakiwa kuwatawala, nguvu zao na mipaka yao. Mambo yakienda kinyume cha hivyo ni kuwa waajiriwa (rais na serikali) wameamua wao wenyewe kumwambia tajiri yao watafanya kazi gani, hawafanyi nini na watajilipa kwa uamuzi wao wenyewe mishahara kiasi gani. Hiki ni kichekesho cha mwaka. Tanzania nchi iliyotangulia kukubali demokrasia haistahili kabisa kuwa kichekesho cha nchi nyingine za Kiafrika zilizokuwa za mwisho kabisa kukubali demokrasia na mfumo wa vyama vingi.

Ni baraza la katiba tu linaloweza kufanya kazi hii bila kuingiliwa na rais au mtu yeyote. Maana unapozungumzia kuwa katiba isomwe, ieleweke na itafsiriwe na watu wengi kadri iwezekanavyo kiungo cha kuwaunganisha wananchi na wale watakaowasaidia kuunda sheria zinazotoka kwenye mawazo na mapendekezo yao ni baraza ambalo lina mizizi yake ndani ya vikundi mbalimbali vya kimaslahi, kimaeneo na kijamii.

Bila baraza hatutakuwa na uwakilishi mzuri baina ya makundi yafuatayo: watawala dhidi ya watawaliwa; vya kidini na visivyo vya kidini; kisiasa na visivyo vya kisiasa; mjini dhidi ya vijiini; wanasiasa dhidi ya wasio wanasiasa; wakulima dhidi ya wafanyakazi na wafanyabiashara; raia dhidi ya polisi na jeshi; matajiri dhidi ya maskini; Watanzania walioko nchini na walioko nchi za nje; Washauri toka vijiweni na washauri toka vyuo vikuu; walimu dhidi ya wanafunzi; wagonjwa (waliopo na watarajiwa) dhidi ya madaktari na manesi; wanaonufaika na fedha za hifadhi ya jamii dhidi ya wazee na wastaafu wasionufaika sana na mifuko ya jamii; wachezaji mpira na viongozi wa mpira; wenye nyumba na wasiokuwa na nyumba; wanaonufaika na mfumo uliiopo na wasionufaika na mfumo uliopo; wafungwa na raia huru; wazalshaji dhidi ya walaji; wanawake dhidi ya wanaume; watoto dhidi ya watu wazima; vijana dhidi ya wazee; wafugaji na wasio wafugaji; wawindaji na wasio wawindaji; wachimba madini na wasiochimba madini; wavuvi na wasio wavuvi; wakulima na wasio wakulima; viongozi wa kuteuliwa dhidi ya viongozi wa kuchaguliwa; mikoa yenye vyuo vikuu na mikoa isiyo na vyuo vikuu; mikoa yenye redio na televisheni na mikoa isiyo na redio na televisheni; mikoa yenye benki kata na benki za kijamii na mikoa isiyokuwa benki kata na benki za kijamii; mikoa yenye maji ya uhakika na mikoa isiyo na maji kabisa; makabila makubwa kwa makabila madogo; makabila yanayofaa kuwa rais na makabila yasiyokubaliwa kutoa rais; mikoa dhidi ya nchi (Zanzibar); wenye dini na wasio na dini; mikoa yenye barabara na mikoa isiyo na barabara wala madaraja; na kadhalika. Kwa haraka haraka, haiwezekani kamwe Tume ya Katiba kufikia makundi yote haya wala kuwa na uwakilishi wa makundi yote haya. IT IS IMPOSSIBLE. Turudi kwenye ya msingi (back to basics) mheshimiwa akubali kashauriwa vibaya na kinachohitajika sio tume na wala yeye hastahili kuunda tume hiyo na akubali kwamba WATANZANIA WANA HAKI YA KUCHAGUA BARAZA LA KATIBA 2011 litakalochagua tume na kufanya kazi ya kuiwezesha nchi hii kuwa na katiba mpya, na taasisi zote zikiwa na wataalamu na wasio wataalamu kama wajumbe na ambazo hazitaweza kuingiliwa na rais au mwanasiasa yoyote au chama chochote cha kisiasa au kundi lolote la kidini katika kazi yake.

Eti inasemekana kwamba CCM inapeleka muswaada huu bungeni ulioandaliwa na watoto wa mtaani kwa sababu ilihofia kuwapa wataalamu ambao wengi wao wanatoka dini moja na hivyo kuhatarisha maslahi ya chama tawala ambacho kimeanza kulalia upande fulani kwa makusudi huku kikihubiri hadharani kinyume cha yale inayoyafanya.

MASHARTI YA KUWEZESHA KUPATIKANA KATIBA MPYA BORA, SAFI NA NZURI DUNIANI:

1. Wananchi waitwae haki yao ya kuunda Baraza la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2. Rais na chama chake tawala, CCM, lazima wakubali kuwa ni wadau katika uundwaji wa katiba ijayo;
3. Rais na chama chake tawala, CCM na serikali yao lazima kisalimishe haki ya mchakato wa katiba kwa wananchi wakitambua kwamba wananchi ndio bwana na wao ni watumishi wa wananchi;
4. Baraza la Katiba 2011 liundwe kutokana na makundi ya kimaeneo, kijamii, kimaslahi na kiajira au kikazi;
5. Baraza liwe na angalau mwakilishi mmoja wa kimaeneo kutoka kila wilaya Tanzania, hawa wawe wanajua hofu, matatizo na matarajio ya wilaya zao; kisha kuwe na uwakilishi wa vikundi au vyama vya kisiasa na wanaharakati; kisha kuwe na uwakilishi wa vikundi vya kiimani au kidini; kisha kuwe na makundi ya uwakilishi wa wazalishaji, mathalani, kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji madini, viwanda na kadhalika; kisha kuwe na uwakilishaji wa walimu/wahadhiri, madaktari, manesi, wahandisi, wanateknolojia, watumishi wa umma, watumishi wa sekta binafsi, wafanyabiashara na makundi mbalimbali ya kikazi na kijamii; bila kusahau kuwepo kwa vikundi vingine vyovyote vitakavyochangia ukamilifu na utilimilifu wa katiba tarajiwa;
6. Tume iundwe na Baraza la Katiba kwa kuwachagua baadhi ya wajumbe wake na wajumbe toka nje ya Baraza ili mradi tume iweze kuwa na sura pana, ya kina na ya mitazamo na mielekeo tofauti ili kuweza kuleta changamoto tarajiwa katika mchakato mzima wa kuzaliwa upya kwa katiba tarajiwa;
7. Kila panapopwaya Tume iwe huru kuunda kamati mbalimbali zitakazokidhi matakwa na matarajio yake kwa wakati ili kuhakikisha katiba mpya inapatikana ndani ya miaka 2-3;
7. Uwe wajibu wa baraza na tume kuandaa mikakati ya uelimishaji, ufahamu, uhamasishaji na ushirikishwaji wananchi katika kutoa maoni kwa kufuata utaratibu mzuri wa statistiki wa sampling na uteuzi wa watu wa kuhojiwa ili kitakachopatikana kiwe kinawakilisha kwa kiasi kikubwa mtazamo wa wadau walio wengi;
8. Matokeo ya awali au rasimu itakayoandaliwa na tume itarudishwa barazani kujadiliwa, kuboreshwa au kurejeshwa kwa tume kwa masahihisho au nyongeza au utoaji maudhui zisizostahiki na tume inaweza kuwashirikisha wadau fulani fulani ionapo upo umuhimu wa kufanya hivyo ili kupata kilicho bora zaidi;
9. Wadau wote na ikiwezekana wananchi wote wapate rasimu hiyo kupitia gazeti la bure litakalochapwa na kusambazwa nchi nzima. Baraza na Tume pia ifanye mipango na mikakati itakayowezesha watu majumbani kwao kuizungumzia rasmi hiyo wakishirikiana na redio, televisheni na njia zingine za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi;
10. Baraza na Tume liunde wavuti na kuihimiza serikali kuanzisha vituo vya muda vya kijamii katika maeneo mbalimbali nchini ambako kompyuta na mtandao utapatikana kwa watu kuchangia maoni au mawazo yao na kuisoma rasimu kabla haijapelekwa mbele zaidi;

11. Baraza litakaporidhika rasimu hiyo ifanywe muswaada rasmi wa kupelekwa bungeni kujadiliwa na kupitishwa kama sheria halali iliyo. Baraza litafanya hivyo kwa kupigia kura muswaada huo huku ikiwa kiwango cha kukubalika kimeshaamuliwa kabla;
12. Wananchi na wajumbe wa Baraza na Tume wawe huru kumjadili yeyote na kujadili chochote kwa maslahi makubwa ya nchi hii na watu wake na hasa kama kweli tuna nia ya kuwa na katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya Watanzania kwa miaka 50 au zaidi ijayo;
13. Huu ni wakati wa kutumia rasilimali watu na rasilimali zetu nyingine kikamilifu tukijua kwamba kazi tunayoifanya siyo ya miaka 2-3 bali kazi inayohitaji kutufaa sisi na kizazi kijacho hata kwa miaka 100 au zaidi kama The Declaration of Independence ya Marekani linavyoifaa nchi hiyo miaka 240 toka kuandikwa na kutamkwa hadharani.
14. Ionekane na ikubalike kwamba ni dhambi isiyo na mfano kwa kiongozi au mwananchi yeyote kuchukulia suala la kuundwa kwa katiba mpya kama utani au mzaha kwani suala hili linahusu uhai, usalama na ustawi wa taifa letu na watu wake.
15. Watanzania bila kujali vyama vyao vya siasa wasikubali kabisa hatima ya watoto, wajukuu na vizazi vyao vijavyo kuchezewa na watu wachache wasioitakia nchi hii na watu wake katiba safi, bora, nzuri na inayofaa kuwalinda wananchi wa nchi hii kwa miaka 100 au zaidi!

CCM inajua fika kutokana na sera zake mbovu kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiteknolojia na kiutamaduni hivi leo asilimia 70 ya Watanzania ni wajinga. Kutokana na ujinga wa asilimia hii 70 pamoja na kujua kwamba wanaharakati na vyama vya upinzani vikipewa fursa ndani ya miezi michache vinaweza kuwatoa wananchi kwenye ujinga waliomo inataka bado kuendelea na dhamira yake ya kuutumia ujinga wa Watanzania hao ili kutia katiba iliyopo viraka na kuendelea kutawala kwa kuwadanganya, kuwadhihaki, kuwakejeli, kuwaonea, kuwapuuza, kuwanyanyasa, kuwadhalilisha na kuwachimbia kwenye umaskini zaidi baada ya chama hicho kula fedha zote za MKUKUTA chenyewe na vibarakala wake na sasa vinataka kutapanya pia kile kitakachotolewa kama ruzuku na misaada kwa ajili ya MKUKUTA2.

Chama hicho kingelikuwa na nia njema na hatima ya Tanzania kingewalitumia wasomi, wataalamu wa sheria na wananchi wengine waliofunguka macho kuwa ndio kiini cha kuwafungua macho na kuwaelimisha raia wengine ili mwisho wa siku kila MTANZANIA BAADA YA MIAKA MIWILI MITATU AWE KATIKA NAFASI YA KUJIVUNA KWAMBA NA MIMI NILISHIRIKI KUUNDA KATIBA MPYA YA TANZNAIA TUNAYOITUMIA LEO. KATIBA AMBAYO ITANG'ARA AFRIKA NZIMA NA IKIWEZEKANA DUNIANI KOTE NA SIO KATIBA ITAKYOTUFANYA TUCHEKWE, TUKEJELIWE NA KUDHIHAKIWA NA DUNIA NZIMA!

Binafsi, nitashangaa na ninaamini Watanzania wenzangu watashangaa pia kama safari hii Watanzania na wabunge wao watafanywa na uongozi uliopo madarakani kuwa wajinga waliwao na mabwege wa mwisho kabisa duniani. Hata kama ni asilimia 40 tu ya Watanzania wanaosikiliza redio na ni asilimia 15 tu ya Watanzania wanaoona televisheni na asilimia 3 tu ya Watanzania wanaosoma magazeti kila siku bado wanaharakati, wabunge wetu na wananchi wote waliofunguka macho wanaweza kabisa kuwaambia wananchi nini kinachoendelea kuhusiana na katiba hii. Hakika Bwana Reginald Mengi na kituo chake cha Televisheni (ITV) na redio yake ya Radio One wanastahili heshima na shukrani za kipekee kwa kuwa Mtanzania pekee anayewatakia mazuri na mema Watanzania wenzakae na vizazi vyetu vijavyo. Mungu ampe afya na maisha marefu katika kutenda mema na mazuri kwa Watanzania.

Wabunge wetu waheshimiwa, ninaomba kutoa hoja: 'KATAENI MSWAADA HUO, BUNGE LISIMAME KWA MUDA, KUSIWE NA KIKAO CHA BAJETI HADI BARAZA LA KATIBA 2011 LIMEUNDWA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UMEANZA!'

Mungu ibariki Tanzania na wape rehema, huruma na neema zako wale wote wanaoututakia mema Watanzania wa leo na wa kesho na walaani na uwaingize motoni wale wote wanaoitakia mabaya na hasara na gharama kubwa wananchi wa Tanzania kwa kuleta mzaha na kurefusha kazi inayotakiwa kufanywa siku moja ikachukua mwezi, wiki moja ikachukua mwaka, mwezi mmoja ikachukua miaka 10 na mwaka mmoja kuchukua karne! Walaani na watupe katika kaburi la sahau la historia ya nchi yetu na watu wake!

Kuna wanaodai pia katiba serikali CCM inayotaka kutupatia ni ile itakayohakikisha Watanzania wanaendelea kuwa maskini, kuongezeka magonjwa na kuongezeka kwa ujinga na utawala usio wa kisheria na wa kistaarabu kwa miaka mingine mia moja (100). Kweli hili linakubalika? Kuna nchi ambazo zimekuwa zikiendelea kwa miaka 5 tu baada ya kiongozi mwangavu, mbunifu na mchumi na asiye mbabaishaji kuingia madarakani. Lakini Tanzania tunaona watu wakiingia Ikulu na kubadili suti na hakuna nafuu yoyote kwa mwananchi wa kawaida-miaka 10 ingia, miaka 10 toka na hili haliwezi kwisha bila kuwa na katiba mpya. Na katiba hiyo tuzungumzie kila kitu kuanzia rais mpaka Babu Loliondo, kuanzia Muungano mpaka kuwa na mikoa huru inayojitawala yenyewe kiuchumi na tulizuzungumzie pia baraza na tume na kamati zote zitakazoundwa kwa nia njema ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na katiba NZURI ILE MBAAAAYA!!!!



ENGLISH VERSION

Bill for review of Tanzanian constitution wanting...

DESPITE being the first country in East Africa to have a law school the current leadership in Tanzania chose unknown people who went to 'copy and paste' a bill full of mistakes from a neighbouting country.

By choosing non-expert to draft the bill CCM has shown its true colors that it despise and abhor intellectuals and it can do anything to bypass them. Unfortunately, it cannot wish them away for the academics are part and parcel of the ruled or misruled in this country.


This gross shamefula act is a reflection of how the government think over and makes decision that are matter of life or death for a nation. Jokingly, smiling and leave the rest to God and do business as usual.

But this time it was not truly a joke. But a deliberate attempt to derail the new constitution drafting process so that CCM who have most likely been caught with their pants down don't see how they can win the next elelctions if there is a new constitution. For the old constitution used to allow them to ride roughshod over the opponents using the office of the registrar of parties and the Not-Independent Election Commission of Tanzania (NECT).

CCM is deliberately allowing a 'rotten' bill to go to the parliament so that it can be rejected and the constitution reneissance process be nipped in the bud.

Opposition members and academics have uncovered a hidden agenda which prevented them from going to the high court and the non-existing constitutional court because that is exactly the ruling party wants. The opening of a case that will help them manipulate the judiciary and buy all the time they need and most likely spillover to the next phase of government, because by all means the existing constitution will allow the party to rig the elections and win again.

CCM and its leaders have robbed the people the right to decide how the constitution remaking exercise shoudl be managed and run.

Since the president and his party are stakeholders among other stakeholders it amounts to usurping the people power when the president chose an electoral commission instead of the people choosing themselves members to A CONSTITUTIONAL CONFERENCE the rightful body that can appoint a Constitutional commission from its own members and others supposed to help draft the new constitution perfectly, timely and without a hitch.

Sovereignty resides within the people and belonging to the people and it is definitely the people right to have chosen representatives who can represent the myriad of interest groups existing in the nation. An Electoral Commission of 30 members can hardly be representative of the regions themselves which are 30 in total now. And the fact remain that this is not a people chosen tool but a tool chosen by the president who is also the chariman of the ruling party. Which is not just right.

If the people will is to be exercised then a CONSTITUTIONAL CONFERENCE OR ASSEMBLY shall be created by the people through their interest groups, regions, profession and other stakeholders in the country. It is the Constitution Conference that will appoint members from within and without to the Constitutional Commission which will also have the right to establish several committees to facilitate its work of writing a new constitution.

When the draft constitution is ready it should be published in a free newspaper in the national lingua france-Kiswahili and distributed nationwide as well as to Tanzanians living abroad and those in prison. They will chirp in all sorts of comments and the national constitutional conference will meet again to incorporate the necessary before the draft constitution goes to the national assembly for scrutiny and approval.

All Tanzanians should be firm on the issue of writing a new constitution and should not allow the government to usurp their powers. Such an action will create a situation that led to people action and revolutions as we are witnessing now in the Middle East and Arab peninsula.

May God give our leaders and CCM the wisdom of accepting the fact that Tanzanians want a brand new constitution that as the President promised can be useful to Tanzanians for the next 50 years or more and not otherwise. Anyone who plays with this noble wish of Tanzanians, that is, to have a new constitution is the TRUE ENEMY OF THE PEACE AND UNITY OF TANZANIANS. Presently, CCM and its leaders stand accused of that ignominous sin!
 
Ulaghai wa Kikwete na mchezo wa karata tatu kuliangamiza azma yetu wananchi kutaka katiba mpya niliokua nikiwatahadharishe hapo Mwezi Januari ndio huu hapa.
Nani kasema watanzania wengi wanataka katiba mpya?Ni poll gani imesema hivyo?Gimme a reputable polling institution ambayo imesema asilimia kubwa ya watanzania wanataka katiba mpya!..mlitulazimisha vyama vingi miaka ishirini iliyopita,mpaka sasa what has been done ni kutuletea CCM leftovers bungeni...Msipende kuforce mambo!
 
Shukrani sana kwamba jibu juu ya hili swala unalolizungumzia tayari unalo. Isitoshe, hebu njoo hapa Karimjee Hall sasa hivi kama uko Dar ili na wewe ukajionee yanayoendelea humu kuliko tu masimulizi.

Nani kasema watanzania wengi wanataka katiba mpya?Ni poll gani imesema hivyo?Gimme a reputable polling institution ambayo imesema asilimia kubwa ya watanzania wanataka katiba mpya!..mlitulazimisha vyama vingi miaka ishirini iliyopita,mpaka sasa what has been done ni kutuletea CCM leftovers bungeni...Msipende kuforce mambo!
 
Watanzania wenzangu, ni miezi minane sasa tangu Rais Kikwete atupe ahadi kemkem kuhusu shauku yake kubwa kwa WALAZWAHOI kujiandikia wenyewe KATIBA MPYA ya taifa letu. Je zile ahadi zote zilikua tu ni nguvu za soda au ghiliba za Mzee Abunuasi?????????????

Na kama majibu ni kwamba mawazo katika maswali yote mawili ni sahihi basi KITU GANI KIFUATE kwetu sisi vijana kufuatia huu usingizi wote wa pono ambao ikulu yetu inaendelea kuuchapa juu ya matakw yetu ya katiba mpya baada ya kuibiwa HAKI YA KUCHAGUA ha Oktoba mwaka jana????????????
 
Na nyinyi hamuna wema kwa lolote lile analofanya JK. Mulitaka katiba mpya mumeambiwa itaandikwa, sasa si musubiri huo utekelezaji wake ndiyo museme?
We nawe mpaka msukumwe kwa vidole vitano ndo mseme, sasa si utulie watu tujadili, you don't have a will at all, kwanza mnafikiria nafasi zenu za burebure mtazipata vipi! Huo ni UKOMA kiakili!
 
Hakika wa TZ tunaitaka CHADEMA isimame imara kama wanavyoungwa mkono na wanchi walio na uelewa
Tena chadema wasifikiri wao ndo bora sana nawakumbusha palikuwa na NCCR mageuzi ikaja CUF ya ukweli sasa ni CHADEMA
tunataka Dr slaa na mbowe Msimame imara tupate katiba mpya sio mfikiri kwenda ikulu kwanza, na yeyote mpiganaji
anatambua nguvu mliyonayo kwa wa TZ, sasa tunataka mtende mnayo yasema ili tuone mwatuelekeza wapi.......
 
Jambo la msingi hao chadema watuhamasishe wananch wote ili tupate katiba mpya mapema
waandae mkutano wa chama watoe maadhimio yao ili wanchi wajue msimamo wa chama chao
na wasisahau tunaotaka mabadiliko ni wote c chadema tu.....
 
Back
Top Bottom