Hatma ya Katiba Mpya: Kikwete na Karata ya Kisiasa Kuangamiza Taifa 2011

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,190
Si Kikwete wala CCM waliowahi kuamini katika kuandikwa upya Katiba yetu. Hivyo wao kuzalisha Tume ya Katiba IKULU badala ya BUNGENI tayari ni safari ya maafa kwa taifa letu kama washikadau wote wa katiba hawatahusika na kila hatua tangu mwanzo.

Watanzania, tukidanganyika katika ahadi za ajabu ajabu kukumbatia wachafu na mipango yao kuuteka nyara nia njema ya raia wa Tanzania kujiandikia katiba wapendavyo,

Na kwamba huku tukijua fika kuwa watu hao ni wachafu kwa mienendo yao tangu kwenye uchakachuaji wa uchaguzi mkuu wetu na ufugaji mzuri wa ufisadi nchini,

Na kwamba wachafu hao baadaye kwa ghiliba zao wakaja wakaambukiza huo huo uchafu wao kwenye kutuchafulia na kutia masizi ya kifisadi nia yetu njema ya kujiandikia katiba mpya baada ya zaidi ya miaka 50 nchini,

Na baada kwa uchafu wao huo au ghiliba tukaishia ama na mchezo mchafu au katiba mpya chafu, basi moja kwa moja kila mmoja wetu ajiandae kuhukumiwa vibaya mno na historia ya taifa hili.

Maggid, Mwanakijiji na wengine wengi wenye uwezo wa kuona haya lakini mkaamua kuyafumbia macho, zingatieni haya ninayoyasema hapa kwa leo na kesho.

Siwezi nikawa shetani jana na kuwaibieni haki yenu ya kuchagua hapo 2010 halafu mwaka unapogeuka 2011 na mimi sasa nikageuka malaika wa kuwapiganieni walalahoi HAKI ya kupata katiba mpya niliyoshindwa miaka kuamini miaka yote kukubali kubadiliswa.

Hoja yangu ni kwamba Kikwete kama mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa tayari ni INTERESTED PARTY ambaye hawezi akaaminiwa na kujikabidhi hata sehemu moja ya hatua mbalimbali za kupatikana kwa katiba mpya.

Laa sivyo, tujaribu kupanda basi hili HATARI na hapo baadaye kidogo wananchi waje wagundue WAMECHEZEWA SHERE na kikundi fulani kuibuka na kusema 'CCM, Ushindi ni LAZIMA' baada ya ghiliba nzima, dalili zote zinaonyesha kwamba kutakua HAPATOSHI tukiingia uchaguzi 2015 bila katiba mpya iliozaliwa kwa ushirikishwaji wa wananchi wote kwa kila hatua tangu mwanzo!!!
 
Nia na harakati za wananchi kujiandikia katiba mpya ikitekwa na mtu yeyote, aanze kufanyia kazi chumbani kwake peke yake na wale waalikwa wake pasipo kupitia bungeni na kushirikisha wananchi wote tangu hatua za awali, na kwamba CCM ichezee juhudi hizi hata uchaguzi mkuu 2015 ikafanyika bila katiba mpya ya kuandikwa moja kwa moja na wananchi, basi Maafa yajayo kitaifa tusijesema yametushwa kitu wakati sasa hivi tunaliumba wenyewe.
 
Nia na harakati za wananchi kujiandikia katiba mpya ikitekwa na mtu yeyote, aanze kufanyia kazi chumbani kwake peke yake na wale waalikwa wake pasipo kupitia bungeni na kushirikisha wananchi wote tangu hatua za awali, na kwamba CCM ichezee juhudi hizi hata uchaguzi mkuu 2015 ikafanyika bila katiba mpya ya kuandikwa moja kwa moja na wananchi, basi Maafa yajayo kitaifa tusijesema yametushwa kitu wakati sasa hivi tunaliumba wenyewe.

Na nyinyi hamuna wema kwa lolote lile analofanya JK. Mulitaka katiba mpya mumeambiwa itaandikwa, sasa si musubiri huo utekelezaji wake ndiyo museme?
 
Jamani, watanzania we deserve consistent leadership. This country can't be run knee jerk style, where decisions are driven more by exigencies of the moment than by a principled policy frame! Kwani policy frame ya kutaka kufanya marekebisho au kutunga katiba mpya haipo? Tukibakia hivi miaka yote we will forever be stuck in the swampy ponds of the few fisadis!
 
Hilo ndilo hasa litakuwa pigo kwa wananchi. Chama cha CCM muda wote halikuwa na mpango na katiba mpya kwa sababu hilo litakuwa pigo kwao. Kujitokeza kwa JK kuunda Tume itakayoratibu Katiba ni mkakati wa kuteka hoja za msingi za wananchi na hatimaye tufike 2015 tukiwa katika mchezo wa kuigiza kuhusu katiba. Siamini kama JK ana nia ya dhati ya kutuletea katiba mpya. Wala sikubaliani na suala la kuunda katiba kama ni majukumu yake. Yeye mwenyewe kama rais ndiye chanzo cha matatizo kwa sababu katiba inambeba.
 
Na nyinyi hamuna wema kwa lolote lile analofanya JK. Mulitaka katiba mpya mumeambiwa itaandikwa, sasa si musubiri huo utekelezaji wake ndiyo museme?

Sisi siyo mazezeta. Jk asifanye suala la katiba mpya kama ufadhili wake kwa wananchi. Wananchi tunataka katiba mpya lakini vile vile iwe kwa utaratibu tunaoutaka siyo anaoutaka JK. Yeye ana maslahi binafsi na katiba hawezi kusimamia tena katiba. Tume anayounda yeye kwa mipango yake ni kutuhadaa wananchi ili atuingize mkenge
 
Siwaelewi wale waliokuwa wanapinga kuwa na katiba mpya halafu wamebadirika ghafla na kutaka katiba mpya ! Hiyo hekima ya kuona umuhimu wa katiba wameinunua wapi?Kwani hawakuwa nayo siku chache za nyuma.Hatuwezi kuwa na imani na ndumilakuwili hawa,wakae pembeni.
 
Katiba si ufadhili wa mtu jamani! Tujitambue wananchi wote wenye nia njema kwa nchi yao!
 
hakuna kitu kibaya kama kumtisha adui na kusita! ule moto wa CDM ungekuwa mkali zaidi tungekuwa mbali sana na hili swala, kwa sasa CCM wameisha-ichukua na kuwa ajenda yao, hata tuseme nini we did mistake and we are reaping! Ab imo pectore... CCM WILL DO NOTHING IN THIS MATTER..NOTHING , just blaha blaha
 
Binafsi siafiki kabisa jambo kubwa na sensitive kama hili kuratibiwa na tume ambayo ni hand-picked by JK!

I simply dont trust him...kuna viwingu vingi ambavyo hadi sasa ameshindwa kuviondoa (EPA, Richomond/Dowans, etc) huku tuhuma dhidi yake kutoka wikileaks zikiwa bado ni kitendawili.

An independent institution (eg the Bunge, etc) must be at the helm to oversee this process!
 
Loh, jamani mie naona hata hii kauli ya utashi na kukubali kuwa Katiba ibadilishwe inatufaa. Sasa kinachobaki ni kuhakikisha kuwa mchakato unakuwa inclusive kwa makundi yote muhimu. Naelewa hasira waliyonayo wanaharakati lakini tunaanza step by step. Angalia mchakato ulivyoanza.

1. Shinikizo kutoka kwa wanaharakati juu ya mabadiliko ya katiba
2. Tamko la aliyeshikiria rungu la nchi(JK) kuwa ni sawa mabadiliko yatokee( Hii ni hatua muhimu hata kama kuna mapungufu)
3. Tupige kelele kama tulivyoshinikiza mabadiliko juu ya muundo na jinsi ya kuunda tume ya kuendesha mchakato
4. Na penyewe tusubiri tuone response inakuwaje then tusonge mbele.

WAJIBU WETU NINI?

Baada ya sisi wachache wenye uelewa kuvoive out our view na kusikika, turudi kwa wananchi, maana ni wachache sana wenye uelewa kuhusu katiba ukiachilia mapungufu yaliyopo. Wananchi wengi hawajui kwa nini mabadiliko. Wao wapo tu wanasubiriwa kuelezwa wapi wanapunjika, wapi katiba inawaonea. Tukifanya hivyo itakuwa rahisi kusema kuwa wananchi nao watoe maoni yao. Binafsi nimefanya informal research tene kwa baadhi ya watu wenye upeo kiasi (Primary and Secondary school teachers) kama wanaelewa wapi katiba ya nchi ina mapungufu na wapi wanadhani marekebisho yafanyike, asilimia 98% walidai wao hawajui mambo ya katiba wanachotaka waboreshewe mshahara. Kwa wananchi kule kijijini kwetu (Karibu na kiwanda cha Kagera Sugar) wao mambo ya katiba hawajui bali wanaomba bei ya kilo ya sukari ipungue waweze kunywa angalau chai yenye sukari!!!!. Sasa hofu yangu ni kuwa Jk na wenzie wakishtuka na kuelewa kuwa mahitaji ya wananchi ni vitu vidogo vidogo na si Katiba ambayo ki msingi ikirekebishwa ndicho chanzo cha wao wote kufaidi raslimali za nchi hii badala ya kufaidiwa na wachache. Jamani tufanye mpango wa kuwanoa wanchi kwa sasa baada ya angalau kufukunyua kwa president part of response. Nawasilisha.
 
yani mimi mwenyewe nilijiuliza sana swala la katiba kwa nini ajalipeleka bungeni kwa nini ajichukulie maamzi peke yake kuhusu kuundwa kwa katiba?
 
yani mimi mwenyewe nilijiuliza sana swala la katiba kwa nini ajalipeleka bungeni kwa nini ajichukulie maamzi peke yake kuhusu kuundwa kwa katiba?

mkuu.... JK nanatafuta legacy.....very selfish
 
KATIBA YA WANANCHI KWA NJIA YA BUNGE, MENGINEYO UCHAKACHAJI MPYA:

Mhe Kikwete kukubaliana na Nguvu ya Umma kupatikana KATIBA MPYA apongezwe; Kujichagulia kushughulikia jambo asiloliamini AKATALIWE.

Katiba ya Wananchi itapatikana kwa njia ya Bungeni kule Dodoma na wala si Chumbani Ikulu pale Magogoni.

Utaratibu huu wa 'Wananchi kujiandikia katiba' badala ya 'Serikali kutuandikia Katiba' ukipuuzwa, kuna shida kubwa 2015.

Bado kuna nafasi la kulinusuru taifa na maafa hapo 2015 endapo BUNGE litasikia na kushughulikia matakwa ya Umma kama alivyoahidi Spika Mama Anna Makinda na ofisi yake juzi.
 
Binafsi siafiki kabisa jambo kubwa na sensitive kama hili kuratibiwa na tume ambayo ni hand-picked by JK!

I simply dont trust him...kuna viwingu vingi ambavyo hadi sasa ameshindwa kuviondoa (EPA, Richomond/Dowans, etc) huku tuhuma dhidi yake kutoka wikileaks zikiwa bado ni kitendawili.

An independent institution (eg the Bunge, etc) must be at the helm to oversee this process!


MBUNGE NA UHAKIKA WA UBUNGE WAKE 2015 UTATEGEMEA JINSI KILA MMOJA WAO ATAKAVYOSHUGHULIKIA 'HOJA YA KATIBA MPYA' DODOMA MWEZI FEBRUARI:


Kutokana na Tume za Raisi za miaka iliopita fundisho tunalolipata ni ghiliba kwa kila kimojawapo na wala hamna nafasi ya sauti ya mwananchi kusikilizwa zaidi ya SERIKALI KUPELEKA MAONI YAKE YENYEWE kwa matawi ya CCM na kuja kuzipitia baadaye kwa njia ya Tume ya Raisi ya kukusanya maoni ya wananchi.

Endapo mtu hajui kilichotufikisha hapa mpata tukawa tunadai KATIBA MPYA YA KUANDIKWA MOJA KWA MOJA NA WANANCHI KWA KUMILIKI, KUSIMAMIA NA KURATIBU HATUA ZOTE ZA MCHAKATO MZIMA basi ataweka matumaini yake kwa Tume ya Mhe Kikwete.

Jibu sahihi liko na wabunge kule Dodoma mwezi Februari ambapo wananchi watawasimamia kwa karibu sana na kuona wanavyoshughulikia hili jambo muhimu sana kwetu.

Pia ni dhahiri kwamba uhakika ba mbunge yupi atarudi bungeni tena 2015 itategemeana sana na jinsi atakavyojihusisha na kushughulikia HOJA YA KATIBA MPYA BUNGENI.
 
Na nyinyi hamuna wema kwa lolote lile analofanya JK. Mulitaka katiba mpya mumeambiwa itaandikwa, sasa si musubiri huo utekelezaji wake ndiyo museme?


Demokrasia ya kweli ambayo JK alidai kuimarika nchini INAKATAA KABISA SOLO-DANCE KIND OF DECISIONS. Na hili hata Dr Benson Bana analifahamu sana na alipashwa kulizingatia alipokua akimshauri raisi.

The backfire of this strategy to seek to play political cards on the constitution is bound to be too dear and very fatal on the sponsors of the 'Ikul Avenue' school of thought over constitution need to change immediately for that of 'Bunge Avenue'.

Kwa nini Mhe Kikwete anawakimbia wabunge, anaogopa nni kule bungeni??? The World is eagerly waiting to see for itself how independent and honourable is the Parliament of the United Republic of Tanzania when it comes to giving direction to an ENTIRELY DEMOCRATICALLY PEOPLE-CENTRED NEW CONSTITUTIONALISATION in our country.
 
Na nyinyi hamuna wema kwa lolote lile analofanya JK. Mulitaka katiba mpya mumeambiwa itaandikwa, sasa si musubiri huo utekelezaji wake ndiyo museme?

Wakati mwingine michango mingine huwa ninapata wasi wasi kama ni kutoka kwenye kiatu ama mtu! Tusubiri hadi mwisho wa dunia?
 
Wakati mwingine michango mingine huwa ninapata wasi wasi kama ni kutoka kwenye kiatu ama mtu! Tusubiri hadi mwisho wa dunia?


REV MASANILO, NA YA MAGGID MJENGWA UMEYAONA???

Mchungaji Masanilo,

Hilo uliloliona hapo halijanistaajabisha sana na jinsi ambavyo Mwandishi wa Habari MCAMBUZI CHIPUKIZI aitwae MAGGID alivyokimbilia kuona USHUJAA WA Mhe Kikwetu kwa katika lengo lake kutaka KUTIA NAJIS nia yetu njema kujiandikia upya Katiba yetu baada ya miako karibia 50.

Mjenga, hata kabla hajatafakari MAANA YA RAIS KUJIFUNGIA CHUMBANI NA WAALIKWA WAKE WACHACHE kwenye Chombo Binafsi atakachokibatiza TUME YA TAIFA YA KATIBA. Mchambuzi huyu hajajali walau hata kujibu baadhi tu ya maswali muhimu kama haya:

1. Siku zote serikali zote za CCM hufanya mambo yao kwa mujibu wa ilani yao ya uchaguzi. Je, ni lini CCM imeketi na kupitisha wazo la katiba kuingizwa kwenye ilani yake (Badala ya Mahakama ya Kadhi) kiasi cha kutuaminisha kwamba kuna NIA YA DHATI serikali yake ya sasa kutekeleza hili wazo murua kwa Umma wa Tanzania?

2. Kitendo cha Mhe Kikwete kuwa Mwenyekiti wa taifa wa CCM tafsiri yake ni kuwa Jemadari wa fikra, hulka na tamaduni wa CCM sawa sawa na Jemadari ya Jeshi lolote duniani.

Je, ni wapi alikowahi Mjengwa kuona hali ya hivi tuseme Jemadari wa Jeshi la Uganda chini ya Nduli Iddi Amin (huko 1978) akigeuka na kuipigania nchi yetu ya Tanzania ili tukawachukue MATEKA WA KIVITA wanajeshi wa nchi yake? Sasa ni kitu gani kinachomuaminisha Mjengwa kumuona SHUJA Mhe Kikwete kujaribu kuteka kwa mlango wa nyuma VITA VYA KUBADILISHA KANUNI ZA MCHEZO ili UMMA WA TANZANIA TUKAWADAKE MAFISADI ambao yasadikiwa yeye ndiye wa kuwafuga na kuwanawirisha??

Ama ndio KIWANGO CHA UCHAMBUZI WA MJENGWA ULIKOFIKIA??

3. Je, Maggid Mjengwa alipata japo kujisumbua akili yake kujiuliza kwamba katika SUALA NYETI NA ZITO KAMA KATIBA ilivyokwetu hivi sasa, kati ya JUHUDI ZA KUITAFUTIA HATIMA NA MWELEKEO WA KILA HATUA YA MCHAKATO KUANDIKWA KATIBA MPYA ni wapi kati ya IKULU KWA Mhe Kikwete mtu mmoja na BUNGENI DODOMA kuliko na wawakilishi wa wananchi karibia vichwa 400, ni wapi hasa ambapo Kilio Cha Katiba Mpya KITAWEZA KUTENDEWA HAKI ZAIDI kwa faida ya taifa letu??

Kwa nini Mjengwa anataka kutufanya tukumbatie MAAMUZI YA MTU MMOJA kwa maana ya Raisi Kikwete peke yake chumbani kwake ikulu yetu ya Magogoni kuliko maamuzi ya wachaguliwa wa wananchi karibia 400 ambapo wananchi tuna-usemi nao zaidi kuliko rais wa Tume ya Uchaguzi? Maana ya maamuzi kwa misingi ya ki-demokrasia inamgusa vipi hapa Mchambuzi wetu Mjengwa?

4. Kwa kasi aliokimbia nayo Maggid Mjengwa kumtangaza Shujaa Mhe Kikwete kwa wazo ambalo wala hajui litapokelewa vipi nchini na ukizingatia ukweli kwamba maoni ya Mchambuzi Maggid Mjengwa karibia yametoka muda sawa na maoni ya MSHIKADAU MWINGINE MHE KIKWETE AKIZUNGUMZIA CCM sawa sawa na jinsi Mzee Makamba alivyotuahidi kwamba ni Kikwete ndiye atakayetoa msimamo wa chama chao kama MDAU MOJAWAPO WA KATIBA, ndio tuelewe Maggid Mjengwa alikua ni kama askari wa kukodi kufanyia kazi ya UMENEJA MASOKO wazo binafsi la CCM na Mhe Kikwete ili itafsiriwe kuwa ndio wazo la wadau wote wa katiba katika nchi hii??

Sasa wanaharakati watakapoanza KULIPONDA WAZO LA Mhe Kikwete na kuonyesha kupendelea zaidi Tume ya Taifa ya Katiba ikiundwa kutokea kule bungeni Dodoma na wala si Ikulu Magogoni ndipo Mchambuzi Maggid Mjengwa atakapozinduka na kurekebisha UCHAMBUZI WAKE WARU WARU na kumpa jina halisi Mh Kikwete kuwa ni ADUI WA MCHAKATO MZIMA WA KUANDIKWA KATIBA MPYA KUMILIKIWA moja kwa moja ma Umma wa Tanzania na kuudhibiti watakavyo au?

Siku zote Mchambuzi mzuri ni sharti awe mtulivu, kutokufumbia majo baadhi ya hoja yaliowazi katika mada fulani na kubwa zaidi ni katika kujibidisha zaidi kama MCHAMBUZI siku zote kuwatangulia mbele zaidi wasomaji wake ki-fikra na mpevuko wa hoja.

Katika hili Rev Masanilo na wengine wengi tu hapa JF mtakubaliana na mimi kwamba pindi tunapomstahili kumpa CHAMBUZI WA HABARI chipukizi kijana mwenzetu Maggid Mjengwa kwa kuvutiwa kwake na kazi hii akaongeze juhudi zaidi ili baadhi ya wasomaji wake tusionekane kama kukimtangulia mbele zaidi katika kuona mambo na JICHO LA TATU.

Vile vile si vibaya tukamsisitizia haja ya kuonyesha mfululizo wa nguvu za CONNECTED THINKING, KUHABARIKA ZAIDI na juu ya yote kwake yeye mwenyewe Maggid Mjengwa kutafuta KUJIJENGA ZAIDI kama chambuzi toka kwa magwiji wetu tunaowafahamu nchini bila kutia baadhi ya hoja kifungoni huko akizichagulia zile hoja azipendazo jinsi gani zicheze uwanjani.

Kama Maggid Mjengwa ni mkweli na jasiri hatochelea kutujibu hapa jukwani kwamba umoto wake aliouonyesha haukutumia busara zaidi, uchambuzi wa kina zaidi na kuweka pembeni unazi zaidi.
 
CHADEMA tupeni ufafanuzi kuhusu mwelekeo wa sisi wananchi kushiriki uundwaji wa Katiba Mpya nchini mambo yamefikia wapi????
 
Back
Top Bottom