SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,125
- 7,889
Mimi huwa ni mfuatiliaji wa mada mbalimbali zinaziobukaga humu ndani kuhusiana na maendeleo ya mikoa mbalimbali ikiwemo ya Kagera.
Pamoja na kwamba mada nyingi huwa zinaishia katika mabishano ya kuwashutumu wanaKagera kwa majivuno, na wengine wakisema ni wavivu lakini kuna mambo fulani huwa yanasemwa huwa yanafikirisha sana.
Wakati huo huo kuna wengine wanakujaga kuwatetea wenyeji wa Kagera kuwa wamekuwa target ya kuwadhoofisha kimkakati kwa miaka mingi. Pia nakumbuka kuna mtu akipinga hoja ya umasikini wa Kagera alisema si kweli kuwa Kagera ni masikini, akatolea mfano kuwa route za ndege za Bukoba huwa zinajaa muda wote. Hii comment naikumbuka vizuri.
Tukio la hivi karibuni la ajali ya ndege linafikirisha sana. Response ya mamlaka za uokoaji na zile za usalama zinatia shaka siyo tu ufanisi wa taasisi hizi lakini pia dhamira ya serikali dhidi ya mkoa huo.
Kwa mtazamo wangu, na uko huru kutofautiana na mimi katika hili, wenyeji wa mkoa ule wamelitumikia taifa hili kwa uadilifu mkubwa kwa miaka mingi. Toka nimeanza kufuatilia mambo ya nchi hii, nimewasikia wenyeji wa mkoa ule wakifanya kazi za kiuongozi na kitaaluma.
Ukiacha shutuma dhidi ya watu wachache kipindi cha IPTL, nachelea kusema wenyeji wa mkoa ule hawastahili mambo yanayosemwa au kufanywa dhidi yao au mkoa wao. Inawezekana pia usomi na uwezo wa kufanya vizuri katika elimu wa wenyeji wa mkoa ule umezaa chuki au aina fulani ya husda kutoka kwa baadhi ya watanzania wenzao dhidi yao.
Sijui nini kitakuja kutokea kubadili dhamira ya serikali ila nikitazama naona ni wajibu wa wenyeji wa mkoa huu kutambua kuwa hatma ya mkoa huu ipo mikononi mwao wenyewe.
Kama kuna mtawala walimkosea, ingekuwa vizuri waambiwe ili ikibidi wazee wa mkoa waombe radhi ili adhabu yao ifikie ukomo.
PS. Mimi ni mwenyeji wa Nyanda Juu Kusini, nimeguswa tu na jambo hili. Hii mada nilitaka kuileta mapema nikaifuta maana sidhani kama itabadilisha chochote. Inaweza kuishia katika majibizano kama yale ya siku zote.