Hatma ya ACT Tanzania 25 Machi, 2015

Hatma ya ACT Tanzania 25 Machi, 2015

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,463
CHAMA kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) sasa kimetinga mahakamani.

Lucas Kadavi Limbu, mmoja wa waasisi na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, amefungua shauri Na. 17 la mwaka 2015 dhidi ya Samson Mwigamba ambaye ni katibu mkuu wa muda na Peter Mwambuja na Masange M. Masange.

Katika shauri hilo la madai, lililofunguliwa Mahakama Kuu, kanda ya Dar es Salaam, Limbu anataka mahakama itoe amri ya kumzuia Mwigamba na "mawakala wake," kujihusisha na chama hicho; kukiongelea katika vyombo vya habari na kutoa maelekezo yoyote yale kwa wanachama na viongozi wake.

Wadai wengine katika shauri hilo, ni naibu katibu mkuu (Bara); Grason Nyakarungu, katibu mwenezi na mwenyekiti wa vijana taifa; na Ramadhani Suleiman, makamu mwenyekiti (Zanzibar).

Kesi hii imetajwa kwa mara ya kwanza leo na imepangwa kusikilizwa tarehe 25 Machi mwaka huu, ambako mahakama itasikiliza maombi ya kuzuia mkutano mkuu wa chama.

Kabla ya kujiunga na ACT-Tanzania, Mwigamba alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Arsha. Alifukuzwa uanachama mwaka mmoja uliopita.
 
Wasaliti ni wasaliti, watazidi kusalitiana daima.

Mabadiliko ni mpango wa Mungu, yeyote atakayekwenda kinyume nayo lazima laana imfike.

CHADEMA NGUVU YA MABADILIKO.
 
Job true true, wasaliti hawawezi ishi pamoja.....dhambi ya usaliti ni sawa na kula nyama ya mtu



Wasaliti ni wasaliti, watazidi kusalitiana daima.

Mabadiliko ni mpango wa Mungu, yeyote atakayekwenda kinyume nayo lazima laana imfike.

CHADEMA NGUVU YA MABADILIKO.

Hili neno maana yake nini? Naona naliona sana hapa JF ni neno KICHAGA ama?
 
Maisha ya Zitto ni mahakamani, inawezekana hata kadi aliyopewa juzi ni feki na Limbu akishinda hatoitambua hiyo kadi itabidi Zitto aende tena mahakamani kutetea uanachama wake.

Tamu hiyo. Any way mi ninachoamini dhambi ya kuusariti umma na kujiamini kwa kuwa umechanja itakoma tu. miungu haijawahi mshinda Mungu wa kweli. Zzk tunakuombea kama ulionewa utashamiri ila kama uliyafanya haya hutamaliza mwaka ktk siasa bila anguko.
 
Maisha ya Zitto ni mahakamani, inawezekana hata kadi aliyopewa juzi ni feki na Limbu akishinda hatoitambua hiyo kadi itabidi Zitto aende tena mahakamani kutetea uanachama wake.

Since mahakama na sehemu ya serikali ya ccm Limbu has a narrow chance to win na Zitto na kundi lake waliopo kazini kuhakikisha wanaisambaratisha CHADEMA kuendelea kupeta..... Let's keep watching..... Where is my popcorn bag!!
 
Duh, kazi imeanza sijui nani ni mmiliki halali wa nyumba ndogo ya ccm!

Hati halisi (original title deed) anayo Abrahaman Kinana. Yeye kama CEO wa ccm hayo ndiyo majukumu yake kutunza nyaraka muhimu hata za taasisi zao ndogondogo
 
Back
Top Bottom