Maisha ni yako hao wanaokutishia usibadili dini ikitokea leo ukaumwa ugonjwa seriously wakukulaza kitandani huduma zote muhimu hapo hapo kitandani hakuna hata mmoja atakaekuja japo kukugeuza na bado upo kwenye dini hiyo hiyo wanayoamini ni sahihi kwako.
Sisi binadam ni wanafiki sana,mara nyingi huwa tuna machozi ya nyani akiwa anauwawa ila ni hatari sana linapokuja tatizo ktk jamii zinazotuzunguka.nilichojifunza ktk dunia hii na ndicho ninachokiishi ni kwamba:Amani ya kweli haipatikani ktk kuwa na mahusiano mazuri na ndugu tu,hata binadam wengine wanaokuzunguka na marafiki zako tena hawa ndiyo wa muhim zaidi maana wanakuwa wengi kuliko hata hao ndugu na hawa kwenye matatizo ndiyo wanaojitoa kuhangaika.
Unadhani unaposikia mtu akiomba kuchangiwa matibabu na jamii yeye ndugu hana?ndugu anao wanajitenga ila unakuta kwenye masuala mengine yasiyowahusu wanakuwa wa kwanza kureact.ukifa hata akifa mkeo au akifa mwanao wao wakasusa kuna watu wanaokupenda nje yao,kuna watu wanaokujali nje yao tena wakati wakishiriki kinafiki kuna rafiki zako watakuwa na wewe bega kwa bega bila kujali dini yako.muhimu tengeneza marafiki na heshimiana na kila mmoja ktk jamii inayokuzunguka.
Ishi maisha yako,kikundi cha watu wachache kisikukoseshe amani ya moyo.hizo dini zipo tu na haijatokea hata mmoja ktk hao waamini Mungu akamtokea siku moja akamwambia "wewe hapa unaponiabudu ndiyo upo sahihi na yule hayupo sahihi" dini ni jinsi unavyoishi na jamii that's it!!!