Hatimaye Yamenikuta

Hatimaye Yamenikuta

Ni miaka 12 sasa tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza,baada ya urafiki wa miaka 3 nikaamua kumueleza hisia zangu,,akasema mambo ya mapenzi mpaka tumalize shule kwa sasa tuendelee kuwa marafiki tu, kwa sababu alikuwa kila kitu kwangu nilikubali alichokisema na urafiki ukaendelea,kwetu pakawa kwao na kwao pakawa kwetu kila aliyetujua hakuuamini urafiki wetu kuwa ni wa kawaida tu.Miaka ikapita hatimaye tukamaliza kidato cha 6 na hapo tukaanza rasmi mahusiano yetu.Nilikiwa mwanaume wa kwanza kwake,na hapo ndipo aliponikamata kabisa kwani ata pale nilipokuwa najipoza wakati naendelea kumsubiri huyu nikaachana napo,amebaki peke yake.Msichana wa kwanza kumpenda na natamani awe wa mwisho.
Baada ya miaka yote hiyo lile tatizo ambalo mwanzoni tuliliona la kawaida limekuwa kubwa.Dini inaenda kututenganisha,niliona ni rahisi kwangu kubadili dini sababu nimekuwa kwenye misingi ya dini yake kwa muda mrefu,(shule pia ilichangia kwani nimesoma boarding katika shule za dini tangu primary adi advance) lakini kila nikikumbuka mzee alivyotengwa na familia yake baada ya kubadili dini kisa bi mkubwa na huu ugomvi uliotokea siku ya kifo chake akili yangu inagoma kabisa.Sijui natokaje hapa..
Routine Spirit- Roho Nyemelezi Makosa ya Baba na Laana ya Baba yako inaanza kukufuata na soon utaifuata kwa kusingizia Mapenzi.... Pole yako hivi vitu kweli vinarithi ukoo wa kwanza hadi Uzao wa Nne wa ukoo husika
 
Huyo demu ni mkristo ila wewe muislamu, acha na hizo mambo demu ndiye anabadili dini kwa kumfuata mwanaume.
 
maisha ndio yatakavyokua ivyo hope ushaelewa
 

Attachments

  • 2015_11$largeimg113_Nov_2015_232755047.jpg
    2015_11$largeimg113_Nov_2015_232755047.jpg
    21.7 KB · Views: 36
Ukishindwa kuamua sasa wewe kama wewe hata ndani ya ndoa itakuwa jipu,uliona na ulijua, moyo wako upo wapi? Upendo ni pamoja na sadaka,sometime you need to sacrifice something to get something na better kuwa mkweli mapema kuliko ukamdanganya bi dada wa watu akauvaa mkenge baadaye huwa Majuto tu.
 
Kuna mtu anaefungisha ndoa zilizoshindikana ana cheo cha 'DC' hakuna cha biblia wala qur an mtashika katiba ya Nchi.
Asante kwa ushauri wako lakini siwezi kufanya hilo kosa
 
Routine Spirit- Roho Nyemelezi Makosa ya Baba na Laana ya Baba yako inaanza kukufuata na soon utaifuata kwa kusingizia Mapenzi.... Pole yako hivi vitu kweli vinarithi ukoo wa kwanza hadi Uzao wa Nne wa ukoo husika
Kuna wakati naliwaza hili lakini nilishafunga na kutubia sana kuhusu baadhi ya makosa ambayo aliyafanya mzee na yanaoneakana kujirudia kwenye familia
 
Muoe bana.........kwani ukiwa hiyo dini yake kuna nini....ukikufwa umekufwa......wenye hasara ni hao wanaokuzika.........
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]na kweli...akifa ameshakufa tu...
 
Mkuu mbona binafs sion mahal patakapo leta shida ukisema we ni mwisilam na yeye ni RC au kinyume chake?

Nb.mwanaume kubadili dini kwenda ya mwanamke ni tatizo,mwanamke ndio wanasema hana dini so mwambie aje kwenye dini yako..ukipofuka mapema kwenye mapenz utaumia baadae kijana

Ila na wewe sikiliza moyo wako unavyosema mm nmechangia kama wengine!
Mwanamke hana dini?? Hebu kuwa Mwanaume Mkatoliki halafu kaoe Muisilamu au Mlokole!
 
Kuwa maelezo yako huna dini ndani ya moyo wako. Hiyo dini uliyoivaa achana nayo ili uoe alau upate heri duniani mbingu/pepo waachie wenyewe.
 
Hawa wanaume wa sasa wengi wao maamuzi yao wanayajua wenyewe wanashindwa kusimama kama mwanaume yani,
Hahaaa. Mwanaume kubadili dini kumfuata mwanamke kuna walakini. Binafsi nilishindwa kubadili dhehebu kumfuata my first fiancee tukaachana, mpaka leo ananililia
 
Back
Top Bottom