Hatimaye Wanaanga waliokwama angani Miezi 9 warejea duniani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,481
Reaction score
14,858
Wanaanga wawili wa Shirika la Marekani la Sayansi na Teknolojia ya Angani (NASA), Butch Wilmore na Suni Williams, pamoja na Mmarekani mwenzao Nick Hague na mwanaanga wa Urusi Aleksandr Gorbunov, hatimaye wamerudi duniani usiku wa kuamkia leo baada ya kukwama angani kwa miezi tisa.

1742393129519.png
Wanaanga hao walitua salama katika Bahari ya Florida huku wakishangiliwa na umati wa watu. Safari yao ya awali ilikusudia kuchukua siku chache tu, lakini chombo kilichowabeba kilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kutokuwa salama kwa kurejea duniani.

1742393175651.png
Hali hiyo iliwalazimu kubaki angani kwa kipindi kirefu cha miezi tisa. Safari yao, ambayo ilianza mwezi Juni mwaka jana, ilitumbukia katika matatizo makubwa baada ya chombo walichokuwa wakisafiria kushindwa kurejea salama duniani.

Hata hivyo, kwa sasa, baada ya kukamilika kwa kipindi hicho cha changamoto, wanaanga hao wamerudi salama nyumbani.

Mungu ni mwema sana,sijui walikuwa na hali gani baada ya kupata taarifa kuwa chombo hakitaweza kurejea duniani salama.
 
Wanaanga wawili wa Shirika la Marekani la Sayansi na Teknolojia ya Angani (NASA), Butch Wilmore na Suni Williams, pamoja na Mmarekani mwenzao Nick Hague na mwanaanga wa Urusi Aleksandr Gorbunov, hatimaye wamerudi duniani usiku wa kuamkia leo baada ya kukwama angani kwa miezi tisa.

Wanaanga hao walitua salama katika Bahari ya Florida huku wakishangiliwa na umati wa watu. Safari yao ya awali ilikusudia kuchukua siku chache tu, lakini chombo kilichowabeba kilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kutokuwa salama kwa kurejea duniani.

Hali hiyo iliwalazimu kubaki angani kwa kipindi kirefu cha miezi tisa. Safari yao, ambayo ilianza mwezi Juni mwaka jana, ilitumbukia katika matatizo makubwa baada ya chombo walichokuwa wakisafiria kushindwa kurejea salama duniani.

Hata hivyo, kwa sasa, baada ya kukamilika kwa kipindi hicho cha changamoto, wanaanga hao wamerudi salama nyumbani.
Wenzetu wapo angani sisi tuko busy kabandika mabango ya samia mpaka airport.
 
Kuna raia hawaamini hili, wanasema ni hadithi ya kutengeneza.

Mathanzua
 
Back
Top Bottom