Wanaanga wa crew 4 wajiandaa kurudi duniani leo

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Nadhani mara baada ya crew 5 kwenda kwenye kituo cha anga ni wazi kabisa kwamba crew 4 walikuwa washamaliza muda wao wa kukaa katika kituo cha anga za mbali na ilikuwa muda wowote ni lazima warudi duniani

Muda wowote kuanzia sasa wanaanga wa crew 4 wataanza safari yako kutokea katika kituo cha anga za mbali kurudi duniani ambapo waliweza kukaa huko angani kwa muda wa miezi 6 huku wakifanya shughuli mbalimbali za kisayansi na kuhudumia kituo chote

Kjell Lindgren , Bob Hines na Jessica watkins ( Marekani ) huku Samantha christoforrenti akiwa wanaanga wa ulaya katika nchi ya ( Italia )

Wanaanga wote watatumia chombo cha crew dragon ambacho kitawavusha kupita katika eneo hatari la matabaka yanayoweza kuzalisha joto kali linalopelekea moto kama yakipitiwa na chombo chochote kile chenye kasi kubwa sana , kwakuwa chombo cha crew dragon kitapita katika eneo hilo kwa kasi ya zaidi ya mara 5 ya spidi ya sauti ni lazima joto kali litazaliwa sasa crew dragon kina jukumu la kuwalinda

#Gerald
View attachment 2387090
 
Back
Top Bottom