Hatimaye TANESCO wameweza

MZALAMO

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
1,758
1,967
Hadi kufikia oktoba 2019 TANESCO imeweza kuunganisha umeme vijiji 8,102 kutoka vijiji 2,018 mwaka 2015, hili ni ongezeko la vijiji 6,084 sawa na asilimia 301 ndani ya miaka minne pekee.

Tunawapongeza TANESCO na Serikali kwa kuweza kufanikisha hili maana umeme ni chachu ya maendeleo. Tanzania ina jumla ya vijiji 12,423 hivyo basi vimebaki vijiji 4,321kuunganishiwa umeme na kwa kasi hii ifikapo mwaka 2022 vijiji vyote Tanzania vitakuwa vimeunganishwa na umeme.
 
Unaishi wapi mkuu. Sijui kama ulishaenda huko vijijini ukaona huo umeme
Ukikuta kijij kina vitongoji 6, kitongoji kimoja kinapata umeme vilivyobaki hakuna kitu na inahesabika kuwa kijiji kina umeme.
Ni ulaghai tu aka propaganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…