Heshima kwenu wakuu.
Nikiwa natokea Dar es salaam kuelekea Dodoma jana mchana, tayari kwa kufuatilia mjadala wa bunge juuya Ripoti ya CAG kuhusu account ya ESCROW inayotarajiwa kusomwa siku ya jumatano, kuna taarifa nilizipata kutoka kwa moja ya washauri wakubwa wa Edward Lowassa ambaye nilibahatika kupanda naye gari moja (kwa sababu za kiusalama naomba nisitaje jina lake). Inasemekana kuwa Edward Lowassa na kambi yake wamegundua kuwa mipango yake ya kutaka kutumia Ripoti ya IPTL kuiangusha Serikali na hasa kumuhusisha Waziri Mkuu kwenye kashfa hili Imegonga mwamba baada ya kibaraka wake Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kuondolelewa katika kuongoza vikao vya Bunge na kupewa likizo ya muda wa siku 14 nchini Ufaransa. Taarifa zinasema kuwa baada ya maamuzi hayo Lowassa amekuwa kwenye wakati mgumu sana kwani hiyo ndiyo ilikuwa Karata yake ya Mwisho katika kujitengenezea njia ya Urais mwakani 2015.
Kambi ya Lowassa inaamini kuwa uwepo wa Spika Anne Makinda ni pigo kubwa kwake kwani Spika huyo amekuwa imara mara zote anapoendesha vikao vinavyojadili mambo mazito yanayogusa maslahi ya Taifa bungeni na haingiliki kirahisi tofauti na Job Ndugai ambaye wazi ameonyesha mahaba yake kwa Lowassa kwa kuahidiwa Uspika pindi Lowassa atakapokuwa Rais.
Tayari kuna taarifa kuwa mwanamkakati mkubwa na Master Mind wa Safari ya Matumaini ya Lowassa, Mtemi Andrew Chenge ametajwa kuhusika kwenye kufanikisha dili la IPTL wakati akiwa Mwanashria Mkuu wa Serikali. Hili linathibitishwa na Chenge mwenyewe ambaye amekiri kupokea zaidi ya Bilioni Moja na nusu kama Consultancy fee. Hali hii imepelekea kambi ya Lowassa kuandaa mikakati mizito ya kumnasua Chenge katika sakata hili. Tayari hadi muda huu takribani bilioni 4.5 imetumika kwa ajili ya kushawishi wabunge wa CCM na upinzani kushinikiza Pinda ajiuzuru kwa kashfa hii.
Kufuatia kuondolewa kwa Ndugai kuendesha vikao vya bunge vinavyoendelea Dodoma na kuelekea Ufaransa, tayari Waziri Mkuu alijiuzuru kwa kashfa ya Ufisadi ya Richmond jana alifanya safari ya ghafla nje ya nchi kuelekea Ujerumani lakini taarifa za ndani zinasema, Lowassa haendi Ujerumani anaenda Ufaransa kufanya kikao na Job Ndugai kuona ni kwa namna gani wanaweza kufanikisha Waziri Mkuu anadondoka na kashfa hii.
Hali ni tete hadi muda huu Mjini Dodoma wabunge wanaonekana kujipanga makundi huku kundi linalompigia Chapuo Lowassa wakiwa na hofu kubwa kuwa mkakati wao umevuja na wamegonga mwamba wakati wabunge wengi wa CCM wameonyesha kuchoshwa kwa kuyumbishwa na wasaka Urais wenye tuhuma za ufisadi na wafanya biashara walionyimwa vitalu na wabunge wengi wamejipanga kesho kutema nyongo na kusema ukweli kuhusu IPTL.
Wakuu naomba niwasilishe kwenu, nahidi kuwaletea yote yatakayojiri Dodoma Kesho. Ahsanteni

Huu no utunzi wa hovyo sana hivi kwa mini watu wanazushiana hivii.kosa LA kumuangusha pinda liko wapi
Kumekucha. Laana ya kumwonea Pinda inaweza fika mbali.
Hana lolote huyu. PINDA hakurupuki!!!!!!!!!
Je, siyo huyu aliyetoa tamko kwa kuwaruhusu POLISI kupiga raia wasio na hatia!!!!!
Je, si huyu anayetoa msimamo wa Serikali kisha kesho yake anabadilika. Mfano suala la Mgomo wa Madaktari!!!!
Je, Si huyu ambaye hivi majuzi ameonyesha dhahiri kuwatetea walioiba ESCROW!!!
Nk nk nk.
Ndugu acha kutetea uozo. Na huyo uliye safiri naye wote hana la maana kutueleza Wananchi. Hatupo katika kufikiria mbio za Uraisi muda huu. Tunatafakari pesa za ESCROW zitarudi vipi ili at least zitumike kwa madhumuni hata ya madawa katika Hospitali zetu na siyo wachache kugawana!!!!!
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!