Hatimaye Siri ya Ziara ya Lowassa Nje ya Nchi yabainika

Hatimaye Siri ya Ziara ya Lowassa Nje ya Nchi yabainika

Queen P

Member
Joined
Nov 7, 2014
Posts
6
Reaction score
19
Heshima kwenu wakuu.

Nikiwa natokea Dar es salaam kuelekea Dodoma jana mchana, tayari kwa kufuatilia mjadala wa bunge juuya Ripoti ya CAG kuhusu account ya ESCROW inayotarajiwa kusomwa siku ya jumatano, kuna taarifa nilizipata kutoka kwa moja ya washauri wakubwa wa Edward Lowassa ambaye nilibahatika kupanda naye gari moja (kwa sababu za kiusalama naomba nisitaje jina lake). Inasemekana kuwa Edward Lowassa na kambi yake wamegundua kuwa mipango yake ya kutaka kutumia Ripoti ya IPTL kuiangusha Serikali na hasa kumuhusisha Waziri Mkuu kwenye kashfa hili Imegonga mwamba baada ya kibaraka wake Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kuondolelewa katika kuongoza vikao vya Bunge na kupewa likizo ya muda wa siku 14 nchini Ufaransa. Taarifa zinasema kuwa baada ya maamuzi hayo Lowassa amekuwa kwenye wakati mgumu sana kwani hiyo ndiyo ilikuwa Karata yake ya Mwisho katika kujitengenezea njia ya Urais mwakani 2015.

Kambi ya Lowassa inaamini kuwa uwepo wa Spika Anne Makinda ni pigo kubwa kwake kwani Spika huyo amekuwa imara mara zote anapoendesha vikao vinavyojadili mambo mazito yanayogusa maslahi ya Taifa bungeni na haingiliki kirahisi tofauti na Job Ndugai ambaye wazi ameonyesha mahaba yake kwa Lowassa kwa kuahidiwa Uspika pindi Lowassa atakapokuwa Rais.

Tayari kuna taarifa kuwa mwanamkakati mkubwa na Master Mind wa Safari ya Matumaini ya Lowassa, Mtemi Andrew Chenge ametajwa kuhusika kwenye kufanikisha dili la IPTL wakati akiwa Mwanashria Mkuu wa Serikali. Hili linathibitishwa na Chenge mwenyewe ambaye amekiri kupokea zaidi ya Bilioni Moja na nusu kama Consultancy fee. Hali hii imepelekea kambi ya Lowassa kuandaa mikakati mizito ya kumnasua Chenge katika sakata hili. Tayari hadi muda huu takribani bilioni 4.5 imetumika kwa ajili ya kushawishi wabunge wa CCM na upinzani kushinikiza Pinda ajiuzuru kwa kashfa hii.

Kufuatia kuondolewa kwa Ndugai kuendesha vikao vya bunge vinavyoendelea Dodoma na kuelekea Ufaransa, tayari Waziri Mkuu alijiuzuru kwa kashfa ya Ufisadi ya Richmond jana alifanya safari ya ghafla nje ya nchi kuelekea Ujerumani lakini taarifa za ndani zinasema, Lowassa haendi Ujerumani anaenda Ufaransa kufanya kikao na Job Ndugai kuona ni kwa namna gani wanaweza kufanikisha Waziri Mkuu anadondoka na kashfa hii.

Hali ni tete hadi muda huu Mjini Dodoma wabunge wanaonekana kujipanga makundi huku kundi linalompigia Chapuo Lowassa wakiwa na hofu kubwa kuwa mkakati wao umevuja na wamegonga mwamba wakati wabunge wengi wa CCM wameonyesha kuchoshwa kwa kuyumbishwa na wasaka Urais wenye tuhuma za ufisadi na wafanya biashara walionyimwa vitalu na wabunge wengi wamejipanga kesho kutema nyongo na kusema ukweli kuhusu IPTL.

Wakuu naomba niwasilishe kwenu, nahidi kuwaletea yote yatakayojiri Dodoma Kesho. Ahsanteni
 
acha kumchafua EL mbona mnamchokonoa wakati yupo kimya?
 
Huu ni upuuzi mtupu kawaambie wanaccm wezako. Pambaneni hukohuko ndwni ya ccm msituhusishe wana ukawa. Hayo hayatuhusu. Cha msingi hela zirudi na watu wawajibishe na si kufukuzwa tu.
 
Hayo unayosema mleta mada ni mawazo yako,vita ya wagombea uraisi ni ishue ingine kabisa haihusiani na hili la IPTL,je kuna mtu aliwatumwa kuiba?????USITUTOE NJE YA MADA!!!!hela irudi kwanza mengine yatafuatia.Hivi unataka kumdanganya nani hapa na je kashfa ya RICHMOND,EPA zilisababishwa na makundi ya kugombea uraisi????kama ni hivyo bora vita iendelee ili tuwabaini wanaotuibia hela sisi wananchi masikini wa taifa hili.

NB:BRING BACK OUR MONEY!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtahangaika sana mwaka huu kila kona lowasa lowasa,bao mmeshapigwa tafuteni wimbo mwingine,jamaa ni mbunge wa kawaida na ni raia wa kawaida hana uwezo wa kufanya any loobing mbona mnamchokonoa na kwa taarifa yenu hataongea kitu ameamua kuwa bubu,mkichoka mje mwakani mtamkuta state hause atafunguka vizuri
 
Lowassa sasa anakimbia kivuli chake. Asubiri ashuhudie anguko la mkakati wake. Tumechoshwa na wezi hawa wa rasilimali zetu
 
sasa wewe ndo mwehu wa kupindukia. Unamsifia makinda kwamba anatetea mafisadi unasema anasimamia maslahi ya nchi. hata kama Lowasa ni muovu hili la escrow halina mjadala. wamegawana hela kama za urithi wa babu yao unaleta propagana za kishenzi humu. kawaongopee wajinga.
 
Wanataka kumchafua Pinda, mtu ambae aliaminiwa na mwalimu Nyerere tangu alipomaliza chuo kikuu. Mtu muadilifu ambae hakurupuki katika kufanya maamuzi. Mtu ambaye ameonekana kuwapiku katika mbio za urais. Hili halikubaliki. Kila mtu abebe mzigo wake wa uchafu
 
Naomba akirudi apande ndege ya Malaysia na ifanye kama zile.mbili.. huyu mzee anazeeka vibaya. Aliwapinza Ccm wakakosa jimbo la Arumeru kipindi flani kwa kutumia ubabe wa pesa kufanya anaotaka sasa amedhamiria kuvunja serikali ila kwa hili broo lowasa umedoda. Msalimie ndugai huko ufaransa mwambie Makinda anataka kubadili upepo ili akuzidi kete. Shuwain zako.
 
acha kumchafua EL mbona mnamchokonoa wakati yupo kimya?

hakuna anayemchafua Lowassa, alishajichafua mwenyewe tangu miaka hiyo. Kinachofanyika hapa ni kuuleza umma ukweli kuwa hiyo ndiyo rangi yake halisi na sio kumchafua.

Dada Queen pia ahsante kwa kutuhabarisha. Mwenye macho haambiwi tazama
 
we pinda wako kalale naye na hao wenye mahaba na EL wambebe lkn wazalendo tunawataka wezi tuwashughulikie pumbav kabisa
 
Back
Top Bottom