Hatimaye pumzi imekata, nilijua tu

mwananyaso

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
2,995
Reaction score
3,402
Serikali au dola kwa ujumla ina mkono mrefu sana, na kwa muundo wake haijawahi kushindwa, huwa ni suala la muda tu.

Hivyo ni vyema unapotaka kuitunushia misuli lazima utafakari kwa kina sana, kwa maana ya madhara utakayoyapata wewe binafsi, familia yako na jamaa zako kwa ujumla.

Unaweza pata umaarufu wa muda mfupi lakini madhara yake ni ya muda mrefu.

Na kwa kawaida ukiona serikali ina deal na wewe ujue imejiridhisha kwa asilimia zote toka vyanzo vyake ya kua unaikosea.

Ni vigumu sana serikali kuonea raia wake wema, nasema haiwezekani. Nashauri wale mnaojiita wapambanaji dhidi ya dola mtafakari kwa kina sana kabla ya kutenda.

Mwisho kosoeni kwa staha mkiweka hadharani njia au mawazo mbadala, yatafanyiwa kazi ,hii ni imani yangu.

Kutusi, kudhihaki, kukejeli, kuonyesha dharau kwa mamlaka kwa kisingizio cha kukosoa haikubaliki hata kidogo, mtaumia kwani kila zama na kitabu chake, someni alama za nyakati.

Dua la kuku halimpati mwewe. Tulilia mpendwa wetu apelekwe mahakamani, ona sasa.

Tukutane tarehe 07/01/2020, safari ndio kwanza imeanza.

Narudia tena serikali haishindwi, ni suala la muda tu, ukiona mwenzako ananyolewa tia maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongea utoto gani? Naona unajaribu kupandikiza uoga. Kama huna hoja sio lazima ianzishe uzi.

Unasema watu wakosoe kwa staha na maoni yao yatafanyiwa kazi.

Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi inadaiwa zaidi ya miaka 20 na bado hazijapatikana, je ni busara gani mnahitaji zaidi ya uvumilivu wote huo?
 
ElBashir yupo wapi?
 


..serikali na dola zinaundwa na watu.

..na wamekabidhiwa nyenzo wazitumie ktk kutenda kazi zao.

..sasa siyo vizuri kutumia nafasi mlizopewa kuonea na kuumiza wenzenu.
 
Huko jela wanaweza kutuweka wote tukaenenea?????.... Kila wanapo jaribu kutunyamazisha ndipo tunazidi kuongezeka....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe endelea.kujificha nyuma a keyboards,ukweli ndio huo hutaki acha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
The gaverment should fear about the people and not the people should fear about the gaverment

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema serikali haijawahi kushindwa? Mbona imeshindwa kuondoa umaskini?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapenda kusakizia wenzako, wewe kama si mwoga anzisha vagi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…