Hatimaye Pinto alamba dume kwa jina la kuitangaza Tanzania UK

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
KUANZIA wiki ijayo Serikali ya Tanzania itazindua mpango wa kuitangaza Tanzania kwa kuweka matangazo yake kwenye mabasi ya abiria na uwanja maarufu wa ndege wa Heathrow. Mpango huo utakuwa wa miezi sita na umeigharimu Serikali Sh milioni 600.

Mkurugenzi wa Jambo Publication, Juma Pinto, alisema uzinduzi wa matangazo hayo utafanyika katika ubalozi wa Tanzania uliopo Bond Street, katikati ya jiji la London.

Pinto alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar, lakini pia Wizara ya Utalii itawakilishwa na Katibu Mkuu, Blandina Nyoni na maofisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Alisema uzinduzi huo utakuwa matangazo manne yatakayokuwa katika sehemu ya kuchukulia mizigo na inatarajiwa kwamba watu milioni 4.6 watayaona wakati kampeni hiyo itakapokamilika.

“Heathrow kuna sehemu nyingi za kuweka matangazo, lakini kampuni ya JC Decaux ilitushauri tuweke matangazo yote manne sehemu hiyo, kwani ndiyo sehemu ambayo imekuwa nadra kupata nafasi ya kuweka matangazo,” alisema Pinto.

Alisema pia sehemu hiyo ipo karibu na idara ya uhamiaji ambayo abiria wanaweza kuyaona matangazo hayo hata wakiwa sehemu ya uhamiaji, jambo ambalo linaweza kuleta mvuto mkubwa kwa watumiaji wa uwanja huo.

Mbali na Heathrow, pia katikati ya London kutakuwa na mabasi 100 yatakayokuwa na matangazo hayo na inakadiriwa zaidi ya watu milioni 30 watakuwa wakiyaona kila wiki.

Kwa mujibu wa Pinto, matangazo hayo yatakuwa yakionyesha mlima Kilimanjaro, simba, swala, chui na tembo anuani ya mtandao wa TTB na Wizara ya Utalii, huku yakiwa na maneno The Land of Kilimanjaro and Zanzibar, Discover the wonders of the world na Have you been there?

Pinto amesema mwaka ujao wa fedha kuna uwezekano mkubwa kuweka matangazo kwenye treni za chini ya ardhi na kwenye viwanja vingine vikubwa vya ndege vya Gatwick, Manchester na Birmingham.
 
Taasisi ya jambo publication ltd inayomilikiwa na watanzania(wengi wakiwa wamejilipua na sasa wanafungua matawi ya ccm london)wamtajwa ktk ripoti ya CAG kuhusiana na deal lao la matangazo ya ujanja ujanja walioweka hapa london,soma ripoti hiyo....!

MAKATO ya fedha za mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi nchini kwa ajili ya michango inayowasilishwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imebainika kuwa na dosari kadhaa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya waajiri kuwasilisha katika shirika hilo noti bandia.
Mbali na hatari hiyo, fedha hizo wanazokatwa wafanyakazi kila mwezi pia zimebainika kufujwa na uongozi wa shirika hilo na hivyo usalama wake kuwa mdogo.
Hali hiyo ya shaka kuhusu mwenendo wa NSSF imewekwa bayana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kupitia Ripoti yake ya mwaka kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2007/2008.
Katika taarifa yake, CAG anaeleza kuwa michango ya wafanyakazi huwasilishwa NSSF kwa njia ya benki au kwa fedha taslimu na kwamba imekuwa ikiambatanishwa na fomu namba 15 inayochanganua taarifa za mwajiri na mfanyakazi husika.
“Ukaguzi umegundua mapungufu katika kupokea michango tawi la Morogoro kuwa mashine ya kuhesabia noti haifanyi kazi vizuri na kuweza kugundua noti ambazo ni bandia,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya CAG kwa kurejea mifano halisi.
Akitoa mfano wa kuthibitisha kasoro hiyo kubwa ya kupokea noti bandia, CAG katika ripoti yake anaeleza kuwa Januari 4, mwaka jana, mashine ilishindwa kugundua noti mbili bandia za shilingi 10,000 kila moja.
Kutokana na ugunduzi huo, CAG anaeleza; “…kwa maana hiyo basi kama mapungufu hayo yasiporekebishwa yanaweza kuleta hitilafu katika makusanyo ya mapato ya shirika.
Mbali na kasoro hiyo, NSSF pia pamoja na mashirika mengine ya umma likiwamo Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), CAG amebaini upungufu katika baadhi ya mashirika ya umma licha ya ukweli kwamba mashirika hayo yamekuwa na vitabu vya hundi katika kufanya malipo.
Katika kasoro hiyo inayohusisha hundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini kuwa baadhi ya hundi zilitolewa bila kusainiwa na mlipaji.
Kwa mujibu wa ripoti, katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) hundi za Sh milioni 318.9 zililipwa bila kusainiwa na mlipwaji, wakati katika NSSF yenyewe hundi zenye thamani ya Sh bilioni 1.6 zililipwa kwa walipwaji ambayo hawakutia saini zao.
Hivyo basi, ripoti ya CAG inabainisha kuwa fedha zilizolipwa kwa njia ya hundi bila waliolipwa kutia saini ni takriban Sh bilioni 1.9.
Aidha katika kuonyesha matumizi ya fedha yenye shaka ndani ya NSSF, ripoti hiyo ya CAG inaeleza kuwa mfuko huo ulinunua gari lenye thamani ya Sh milioni 120 kinyemela bila kutangaza zabuni kama ambavyo Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 inavyotaka.
Taasisi nyingine iliyobainika kuwa na kasoro ya kiutendaji na hususan katika matumizi ya fedha kwa kuzingatia utaratibu rasmi ni Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA). TANAPA imekutwa na kasoro hizo katika mkataba wake wa kupatiwa huduma ya utangazaji kupitia Shirika la Utangazaji la Cable News Network (CNN) la Marekani na taasisi ya Jambo Publications, ingawa mchakato mzima wa un ununuzi wa huduma hiyo ulifanywa na wizara husika.
“Mikataba husika ilisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi hiyo wakati huo akiwa Kanali mstaafu, Emmanuel Balele lakini mchakato wote wa kupata huduma hiyo ulifanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kinyume cha taratibu za sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004.
“Mkataba huo wa matangazo na CNN kwa mwaka wa fedha 2007/2008 ulikuwa wa thamani ya Dola za Marekani 750,000 (zaidi ya Sh milioni 750),” inaeleza ripoti ya CAG na kufafanua kuwa;
Baadaye TANAPA ilisaini mkataba mpya wa Dola za Marekani 800,000 kwa mwaka wa fedha 2008/2009 kwa ajili ya huduma ya matangazo lakini mikataba yote miwili haikuonyesha muda wa matangazo hayo kama yanatolewa kwa siku, kwa wiki au kwa mwezi na kwa muda gani ili kuweza kufuatilia kama matangazo hayo yanatolewa kwa wakati na kwa kiwango kulingana na makubaliano ya malipo.
Lakini pamoja na hayo yote, imebainika pia kwamba Oktoba, mwaka 2007, TANAPA ilifanya malipo ya Sh bilioni 1.08 kwa CNN bila malipo hayo kuambatanishwa na vithibitisho vya kufanya matangazo au viambatanisho vyovyote vinavyoonyesha kuwa matangazo hayo yalirushwa hewani na CNN.
Kwa upande wa taasisi ya Jambo Publications Ltd, ya London nchini Uingereza, TANAPA ilifanya malipo ya Dola za Marekani 272,006.45 ikiwa ni ada ya kutoa huduma ya matangazo kwa miezi sita, kuanzia Januari, mwaka jana hadi Juni, mwaka huo huo.
“Matangazo yaliyofanywa katika uwanja wa ndege wa Heathrow Terminal 4 uliopo London yaligharimu Dola za Marekani 68,373.23 ambapo huduma ya matangazo kupitia mabasi 100 ya mjini London yaligharimu Dola 203,633.20 (zaidi ya Sh milioni 203) na mikataba hiyo ya matangazo hayo haikuweza kupatikana kwa ajili ya ukaguzi,” inaeleza ripoti ya CAG.
CAG anaeleza kuwa hata hivyo, ankara ya malipo ya Desemba 18, mwaka 2007 kuhusiana na malipo yaliyofanyika ilikuwa na anwani ya Bodi ya Utalii Tanzania ingawaje malipo yalifanywa na TANAPA, lakini pamoja na hayo yote hapakuwa na ushahidi wowote ulioonyesha kwamba matangazo hayo yalifanyika.
Kutokana na dosari hizo zote, CAG anatoa maoni yake akisema ingawaje nia ya matangazo hayo ilikuwa nzuri na kwa manufaa ya taifa, utaratibu uliotumika haukuwa sahihi na hivyo kufanya upatikanaji wa thamani ya fedha kwa huduma zilizotolewa kuwa shakani
.
my take;serikali lazima ichunguze hii wizara ya maliasili,inaonesha kuna vigogo wa kufanya deal pale,hili la matangazo ya hapa london inabidi uchunguzi ufanywe ili kujua jambo publication ltd walilipia kwa muda gani,sababu si kweli kuwa matangazo yalidumu kwa miezi sita,mi ni mkazi wa london na shughuli zangu lazima nipande mabasi na treni kila siku,niliyaona hayo matangazo kwa kipindi ambacho hakizidi miezi 4
 
Wewe ulie London ungeanza kuchunguza ingekua vizuri sana.
Wenzetu wapo wawazi zaidi,hivyo itakusaidia kuipa nyama hoja yako
Takukuru wapo bize na faili la Mengi
 
Nchi hii tuna hela nyingi sana na kwa kadiri wafadhili wanazidi kutumwagiia mabilioni hatuna sababu ya kuhakikisha kuwa tunazisimamia vyema fedha zetu.. why should we?
 
Wewe ulie London ungeanza kuchunguza ingekua vizuri sana.
Wenzetu wapo wawazi zaidi,hivyo itakusaidia kuipa nyama hoja yako
Takukuru wapo bize na faili la Mengi

wanaonufaika na pesa za kifisadi utawajua tu...huna hoja hulazimishwi kuchangia!
 
Mafisadi mko wengi tu, pamoja na kujilipua bado mnatuibia kumbe alafu mkikaa huko mnaanza kuilaumu nchi yetu pamoja na mafisadi wenzenu kumbe na nyie mnatuibia, ZA MWIZI ZENU ZINAKARIBIA, tutawakamata mpaka mliojificha uvunguni. KAZA BUTI Bwana Utouh
 
we umeshamsikia fisadi akiilaumu serikali?fisadi siku zote wanaimba nyimbo za kuisifu serikali,hawa jamaa wa jambo wamemkamata balozi majaar kiasi kwamba huyu mama hafurukuti kwao,kazi yao ni kufungua matawi ya ccm kila kona ya london
 
Taasisi ya jambo publication ltd inayomilikiwa na watanzania(wengi wakiwa wamejilipua na sasa wanafungua matawi ya ccm london)wamtajwa ktk ripoti ya CAG kuhusiana na deal lao la matangazo ya ujanja ujanja walioweka hapa london,soma ripoti hiyo....!

Kwa upande wa taasisi ya Jambo Publications Ltd, ya London nchini Uingereza, TANAPA ilifanya malipo ya Dola za Marekani 272,006.45 ikiwa ni ada ya kutoa huduma ya matangazo kwa miezi sita, kuanzia Januari, mwaka jana hadi Juni, mwaka huo huo.
"Matangazo yaliyofanywa katika uwanja wa ndege wa Heathrow Terminal 4 uliopo London yaligharimu Dola za Marekani 68,373.23 ambapo huduma ya matangazo kupitia mabasi 100 ya mjini London yaligharimu Dola 203,633.20 (zaidi ya Sh milioni 203) na mikataba hiyo ya matangazo hayo haikuweza kupatikana kwa ajili ya ukaguzi," inaeleza ripoti ya CAG.
CAG anaeleza kuwa hata hivyo, ankara ya malipo ya Desemba 18, mwaka 2007 kuhusiana na malipo yaliyofanyika ilikuwa na anwani ya Bodi ya Utalii Tanzania ingawaje malipo yalifanywa na TANAPA, lakini pamoja na hayo yote hapakuwa na ushahidi wowote ulioonyesha kwamba matangazo hayo yalifanyika.
Kutokana na dosari hizo zote, CAG anatoa maoni yake akisema ingawaje nia ya matangazo hayo ilikuwa nzuri na kwa manufaa ya taifa, utaratibu uliotumika haukuwa sahihi na hivyo kufanya upatikanaji wa thamani ya fedha kwa huduma zilizotolewa kuwa shakani.
my take;serikali lazima ichunguze hii wizara ya maliasili,inaonesha kuna vigogo wa kufanya deal pale,hili la matangazo ya hapa london inabidi uchunguzi ufanywe ili kujua jambo publication ltd walilipia kwa muda gani,sababu si kweli kuwa matangazo yalidumu kwa miezi sita,mi ni mkazi wa london na shughuli zangu lazima nipande mabasi na treni kila siku,niliyaona hayo matangazo kwa kipindi ambacho hakizidi miezi 4

Balozi Maajar ni mwanasheria mzuri tu kwenye sheria za biashara tangu akiwa Tanzania. CAG kutokuonyeshwa mkataba ni dalili za ufisadi wa wazi kabisa. Inatia kichefuchefu kuona watanzania tunaiibia nchi yetu kila kona.
 
Da huyu jamaa hatari anacheza guu la kulia na hapohapo guu la kushoto du!! napita masheikh du ngoma drawooo!TUNA NGUVU TENA WAUNGWANA
 
Swali!
Huyu Juma Pinto ni yule aliye wapeleka/aliyewasindikiza kina Masogange airport?
 
KUANZIA wiki ijayo Serikali ya Tanzania itazindua mpango wa kuitangaza Tanzania kwa kuweka matangazo yake kwenye mabasi ya abiria na uwanja maarufu wa ndege wa Heathrow. Mpango huo utakuwa wa miezi sita na umeigharimu Serikali Sh milioni 600.

Mkurugenzi wa Jambo Publication, Juma Pinto, alisema uzinduzi wa matangazo hayo utafanyika katika ubalozi wa Tanzania uliopo Bond Street, katikati ya jiji la London.

Pinto alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar, lakini pia Wizara ya Utalii itawakilishwa na Katibu Mkuu, Blandina Nyoni na maofisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Alisema uzinduzi huo utakuwa matangazo manne yatakayokuwa katika sehemu ya kuchukulia mizigo na inatarajiwa kwamba watu milioni 4.6 watayaona wakati kampeni hiyo itakapokamilika.

“Heathrow kuna sehemu nyingi za kuweka matangazo, lakini kampuni ya JC Decaux ilitushauri tuweke matangazo yote manne sehemu hiyo, kwani ndiyo sehemu ambayo imekuwa nadra kupata nafasi ya kuweka matangazo,” alisema Pinto.

Alisema pia sehemu hiyo ipo karibu na idara ya uhamiaji ambayo abiria wanaweza kuyaona matangazo hayo hata wakiwa sehemu ya uhamiaji, jambo ambalo linaweza kuleta mvuto mkubwa kwa watumiaji wa uwanja huo.

Mbali na Heathrow, pia katikati ya London kutakuwa na mabasi 100 yatakayokuwa na matangazo hayo na inakadiriwa zaidi ya watu milioni 30 watakuwa wakiyaona kila wiki.

Kwa mujibu wa Pinto, matangazo hayo yatakuwa yakionyesha mlima Kilimanjaro, simba, swala, chui na tembo anuani ya mtandao wa TTB na Wizara ya Utalii, huku yakiwa na maneno The Land of Kilimanjaro and Zanzibar, Discover the wonders of the world na Have you been there?

Pinto amesema mwaka ujao wa fedha kuna uwezekano mkubwa kuweka matangazo kwenye treni za chini ya ardhi na kwenye viwanja vingine vikubwa vya ndege vya Gatwick, Manchester na Birmingham.

Huyu jamaa si niliona jina lake kwenye ile list ya wazee wa sembe?
 
Kumbe mambo yalianzia huku?
ndiyo maana siku zote nasema elimu ni kujua mbinu na mipango ya kukuwezesha kuishi basi!
 
hapa ndo utaamini hata ikulu watu wapo kupiga dili tuu, wala hakuna kusaidia jamii
 
Back
Top Bottom